Niliagiza chakula, ilivyokuja bili nusura nikimbie niwaache watoto. Umewahi kukumbana na fedheha hii?

Nilienda kutembea Dar es Salaam kwa dada yangu wakati wa sherehe hizi za christimass.

Basi tarehe 25/12 kama kawaida tulikwenda ibadani na kurudi nyumbani,kilichofuata ni maongezi tu ya kifamilia huku tukichoma nyama jioni na kunywa pombe pamoja na shemeji na marafiki zake.

Tarehe 26/12 nikataka na mimi onyesha msuli wangu kwa shemeji ili asinichukulie poa…Basi bwana nikawaambia leo niachieni hawa vijana nitoke nao out nao waone raha ya kuwa na mjomba,wako watoto wanne na dada wa kazi. jumla watano.

Basi wao wenyewe wakataja mahala wanataka kwenda…ni beach fulani hivi wamejenga vizuri sana na kuna michezo mingi sana ya watoto,vyakula na vinywaji.

Basi tukaondoka tukafika…kiukweli mimi nilidhani ni mahala naweza afford kulipia kila kitu na nilitenga 100,000/= nzima kwa ajili ya kutumbua.

Sasa kufika nikaambia kwanza vijana wapate chakula.Wakaagiza kila mmoja chipsi kavu pamoja na kuku nusu.Pia waliagiza juice freshi na kuna kamoja kiherehere kakaagiza pizza moja ya kushare wote…yule dada wa kazi kwa aibu za kikubwa aliagiza chipsi na mshkaki mmoja tu na juice.

Mahesabu yangu yalikua pale itakata kama 50,000/= hivi pamoja na michezo yao ile…wakamaliza kula,mimi mwenyewe nikaagiza bia zangu 5 pamoja na nyama choma ya mbuzi.

…..sasa game ikaanza karibia wanamaliza kula yule dada ndio akaniletea ile “menu”,lahaulaaaa

chipsi kavu-inasoma 6000/= mara 5
kuku nusu-inasoma 21,000/= mara 4
fresh juice-inasoma glass moja 6000/= mara 5
pizza moja-inasoma 35,000/=
mshkaki mmoja(niligundua wameandika fillet)-3500/=
nyama choma mbuzi—inasoma 25,000/= per portion
bia moja local ni 4000/= mara 5

kwa haraka haraka ilisoma kama 227,500/= kinyume kabisa na matarajio yangu.

Kwanza nilihisi baridi sana imenichapa sababu vitu vyote vishaagizwa na vingine vishaanza kutumika,watoto wanaenjoy sana na huwezi waambia kitu wakakuelewa.

Hapo wanasubiri washibe nikawalipe kila mmoja 5000/= ya kwenda kwenye michezo yao ya watoto…

Mimi bhana nikajitetea nataka kulipa kwa kadi…walete mashine,lengo langu hapa kubahatisha sababu ndio zilikua tarehe bosi anaingiza chochote kwenye account.

Ile kugusa tu pyaaaaa….nakuta sms inaingia umefanikiwa kulipia 227,500/= kwenda Utulivu beach resort,ikaja na sms ya muamala wa makato ya muamala kama 4000/= hivi.

Kwa kweli mood yote ilikata…kwa mshahara wangu hiko kiwango kilikua ni zaidi ya nusu yake mimi nimetumia kulipia watoto kula sehemu ambayo siyo level zangu….ila nikakaza kiume,ile kulipia kwa kadi nikaonekana doni sana pale.

basi na ile laki mkononi nayo nikaibunya mjini…..sahivi niko zangu kwenye katarama narudi zangu mkoani na somo.

Umewahi kutana na dhahama kama hii?!😂
hii hatari sana, mimi niingiaga saluni namaliza kunyoa sikutaka mambo mengi nikaosha. kutoka hapo naambiwa 5000. toka ile siku sigusi kitu bila ya kujua bei. taja bei ndo nifanye maamuzi
 
Siku hiyo nimefuata mwenyewe gari langu Dar (wakati huo nimeajiriwa mikoani). Nilikuwa sina uzoefu wa kuendesha umbari mrefu. Ile nakunja kona ya Morogoro naifuata mbuga ya mikumi usingizi ukaanza. Niliamua kuendesha usiku kukwepa matrafiki kwasababu sikuwa vizuri mfukoni ukizingatia ndo nimenunua ndinga na wese la kunifikisha. Basi, ile naianza mbuga ya mikumi usingizi kama woote! (Kama mnavyojua mbuga za wanyama huruhusiwi kusimama! ni sehemu ambayo ni hatari kusimama, au kuegesha gari sijui upige usingizi kidogo). Basi nilipata shida saana ukizingatia ni usiku na nilikuwa peke yangu! Sijui huo usingizi ulitoka wapi maana si kwa kuyumba huko wakati spidi ilikuwa haizidi 40km/h. Mikumi ina urefu kama kilometer 50 - 60 kuivuka na ukiongeza kama kilometer 20 (buffer zone) inafika kama 70km hivi I guess! Nakwambia nilitumia kama masaa 2 kumaliza mbuga na kufika sehemu ya mahoteri. Kipindi hicho ilikuwa mwaka 2014. Basi nikaendesha na kufunguliwa Gate ya hoteli na kuingiza gari ndani ili angalau nikalale pia kwa usalama wa gari. Eeebwaanah wee! Kufika reception naambiwa for a night 🌙 ni 80,000/=. Nilichoka! Kuondoka siwezi! Nikaingiwa na akili ya kujifanya kuna kitu nimesahahu kwenye gari nilivyoingia kwenye gari nikashusha vioo vya nyuma kidogo na kupiga mbonji mpaka asubuhi saa 2. Nashukuru Mungu hakuna aliyenibughudhi na nadhani sijui walinistahi au vipi maana sikuona nikifwatwa au kuuliza nilivyawasha gari asubuhi na kuondoka! Mlinzi alinifungulia Gate kwa tabasamu na kunitakia safari njema na kusema "Karibu tena". Kwakweli bei za uduma sehemu za washua tuwaachie wenyewe!
Karibu tena VAMOS HOTEL MIKUMI
tuu wakarimu kwa wateja wa aina yote
 
Karibu tena VAMOS HOTEL MIKUMI
tuu wakarimu kwa wateja wa aina yote
Hahhahah! Nimeishasahau jina la hiyo hoteli! Lakini hiko mkono wa kulia ukitokea mbuga ya wanyama! Ni hoteri ya ghorofa moja imepakwa rangi nyeupe! Siku moja nitaenda kuwashukuru kwa ukarimu! BVR 2015
 
hii hatari sana, mimi niingiaga saluni namaliza kunyoa sikutaka mambo mengi nikaosha. kutoka hapo naambiwa 5000. toka ile siku sigusi kitu bila ya kujua bei. taja bei ndo nifanye maamuzi
mkuu,umekosea kuandika…nadhani ulikusudia 50,000/= ila umeandika 5000/=
 
Je, ikizidi?
Hiyo tena sio starehe yakuanza kuuliza bei....wee kama unataka kwenda enjoy unajipima na eneonu alotaka kwenda.
Wee ukifika una oda tuu unajuanhapa kuku hawezi zidi 50k.

Leo ukinda zako pale rotana sii unakuwa na million mfukoni unajua kabosa ata nile nini haiwezi zidi million
 
Kabla sijampeleka Mtu sehemu naenda mwenyewe hiyo sehemu kuangalia na kuuliza bei, sitakagi hekeheka Mimi.... tangu niuziwe Ugali 30000 wakati Mfukoni nina 5000 nimejifunza
Hakika wewe ni MWAMBA haswa. Nimependa stratergy yako. Sijui kwa nini wengi wa Waafrika hatupendagi kitu kinahitwa; window+shopping?
 
Hiyo tena sio starehe yakuanza kuuliza bei....wee kama unataka kwenda enjoy unajipima na eneonu alotaka kwenda.
Wee ukifika una oda tuu unajuanhapa kuku hawezi zidi 50k.

Leo ukinda zako pale rotana sii unakuwa na million mfukoni unajua kabosa ata nile nini haiwezi zidi million
Hapa kuna mawili; either wewe ni mwanamke usiejielewa au bado mtoto unayeishi kwa shemeji
 
Nimecheka sana, eti kamoja kiherehere, mie nakumbuka nikiwa kikazi Dom mida ya saa 4 usiku nikaingia saloon nikwangue nywele, ile kumaliza bei kaniambia buku 5 na kunyoa kwenyewe ovyo, iliniuma hiyo buku 5
Kuna mmoja alimaliza kunyoa akaambiwa buku 5 jamaa akakata akasema usione hiki kitambi mimi sina kitu buku 2 hii hapa kama hautaki piga mwano waje waniue
 
Hapa kuna mawili; either wewe ni mwanamke usiejielewa au bado mtoto unayeishi kwa shemeji
Naishe kwa shemeji....tena naona shemeji hamgegedi dada yangu vizuri. Itabidi nimsaidie shemeji kumgegeda dada vizuri haiwezekani kila leo dada ana makasiriko
 
Nilienda kutembea Dar es Salaam kwa dada yangu wakati wa sherehe hizi za christimass.

Basi tarehe 25/12 kama kawaida tulikwenda ibadani na kurudi nyumbani,kilichofuata ni maongezi tu ya kifamilia huku tukichoma nyama jioni na kunywa pombe pamoja na shemeji na marafiki zake.

Tarehe 26/12 nikataka na mimi onyesha msuli wangu kwa shemeji ili asinichukulie poa…Basi bwana nikawaambia leo niachieni hawa vijana nitoke nao out nao waone raha ya kuwa na mjomba,wako watoto wanne na dada wa kazi. jumla watano.

Basi wao wenyewe wakataja mahala wanataka kwenda…ni beach fulani hivi wamejenga vizuri sana na kuna michezo mingi sana ya watoto,vyakula na vinywaji.

Basi tukaondoka tukafika…kiukweli mimi nilidhani ni mahala naweza afford kulipia kila kitu na nilitenga 100,000/= nzima kwa ajili ya kutumbua.

Sasa kufika nikaambia kwanza vijana wapate chakula.Wakaagiza kila mmoja chipsi kavu pamoja na kuku nusu.Pia waliagiza juice freshi na kuna kamoja kiherehere kakaagiza pizza moja ya kushare wote…yule dada wa kazi kwa aibu za kikubwa aliagiza chipsi na mshkaki mmoja tu na juice.

Mahesabu yangu yalikua pale itakata kama 50,000/= hivi pamoja na michezo yao ile…wakamaliza kula,mimi mwenyewe nikaagiza bia zangu 5 pamoja na nyama choma ya mbuzi.

…..sasa game ikaanza karibia wanamaliza kula yule dada ndio akaniletea ile “menu”,lahaulaaaa

chipsi kavu-inasoma 6000/= mara 5
kuku nusu-inasoma 21,000/= mara 4
fresh juice-inasoma glass moja 6000/= mara 5
pizza moja-inasoma 35,000/=
mshkaki mmoja(niligundua wameandika fillet)-3500/=
nyama choma mbuzi—inasoma 25,000/= per portion
bia moja local ni 4000/= mara 5

kwa haraka haraka ilisoma kama 227,500/= kinyume kabisa na matarajio yangu.

Kwanza nilihisi baridi sana imenichapa sababu vitu vyote vishaagizwa na vingine vishaanza kutumika,watoto wanaenjoy sana na huwezi waambia kitu wakakuelewa.

Hapo wanasubiri washibe nikawalipe kila mmoja 5000/= ya kwenda kwenye michezo yao ya watoto…

Mimi bhana nikajitetea nataka kulipa kwa kadi…walete mashine,lengo langu hapa kubahatisha sababu ndio zilikua tarehe bosi anaingiza chochote kwenye account.

Ile kugusa tu pyaaaaa….nakuta sms inaingia umefanikiwa kulipia 227,500/= kwenda Utulivu beach resort,ikaja na sms ya muamala wa makato ya muamala kama 4000/= hivi.

Kwa kweli mood yote ilikata…kwa mshahara wangu hiko kiwango kilikua ni zaidi ya nusu yake mimi nimetumia kulipia watoto kula sehemu ambayo siyo level zangu….ila nikakaza kiume,ile kulipia kwa kadi nikaonekana doni sana pale.

basi na ile laki mkononi nayo nikaibunya mjini…..sahivi niko zangu kwenye katarama narudi zangu mkoani na somo.

Umewahi kutana na dhahama kama hii?!😂
Hiyo ndiyo ile maana ya jogoo washamba hawiki mjini.Wasalimie wapanda Katarama popote walipo waambie mjini shule ,shamba Darasani
 
H
Nilienda kutembea Dar es Salaam kwa dada yangu wakati wa sherehe hizi za christimass.

Basi tarehe 25/12 kama kawaida tulikwenda ibadani na kurudi nyumbani,kilichofuata ni maongezi tu ya kifamilia huku tukichoma nyama jioni na kunywa pombe pamoja na shemeji na marafiki zake.

Tarehe 26/12 nikataka na mimi onyesha msuli wangu kwa shemeji ili asinichukulie poa…Basi bwana nikawaambia leo niachieni hawa vijana nitoke nao out nao waone raha ya kuwa na mjomba,wako watoto wanne na dada wa kazi. jumla watano.

Basi wao wenyewe wakataja mahala wanataka kwenda…ni beach fulani hivi wamejenga vizuri sana na kuna michezo mingi sana ya watoto,vyakula na kupokea.

Basi tukaondoka tukafika…kiukweli mimi nilidhani ni mahala naweza kumudu kulipia kila kitu na nilitenga 100,000/= nzima kwa ajili ya kutumbua.

Sasa kufika nikaambia kwanza vijana wapate chakula.Wakaagiza kila mmoja chipsi kavu pamoja na nusu.Pia waliagiza juice freshi na kuna kamoja kiherehere kakaagiza pizza moja ya kuwashirikisha wote…yule dada wa kazi kwa aibu kubwa aliagiza chipsi na mshkaki mmoja tu na juice.

Mahesabu yangu yalikua pale itakata kama 50,000/= hivi pamoja na michezo yao ile…wakamaliza kula,mimi mwenyewe nikaagiza bia zangu 5 pamoja na nyama choma ya mbuzi.

.....sasa mchezo ikaanza karibia wanamaliza kula yule dada ndio akaniletea ile “menu”,lahaulaaaa

chipsi kavu-inasoma 6000/= mara 5
kuku nusu-inasoma 21,000/= mara 4
fresh juice-inasoma glass moja 6000/= mara 5
pizza moja-inasoma 35,000/=
mshkaki mmoja(niligundua wameandika minofu)-3500/=
nyama choma mbuzi—inasoma 25,000/= kwa sehemu
bia moja local ni 4000/= mara 5

kwa haraka haraka ilisoma kama 227,500/= kinyume kabisa na matarajio yangu.

Kwanza nilihisi baridi sana imenichapa sababu vitu vyote vishaagizwa na vingine vishaanza,watoto wanaenjoy sana na huwezi waambia kitu wakakuelewa.

Hapo wanasubiri washibe nikawalipe kila mmoja 5000/= ya kwenda kwenye michezo yao ya watoto…

Mimi bhana nikajitetea nataka kulipa kwa kadi…walete mashine,lengo langu hapa kubahatisha sababu ndio zilikua tarehe bosi anaingiza chochote kwenye akaunti.

Ile kugusa tu pyaaaaa….nakuta sms inaingia umefanikiwa kulipia 227,500/= kwenda Utulivu beach resort,ikaja na sms ya muamala wa makato ya muamala kama 4000/= hivi.

Kwa kweli mood yote ilikata…kwa mshahara wangu hiko kiwango kilikua zaidi ya nusu yake mimi kutumia sehemu ya kulipia watoto ambayo siyo level zangu….ila nikakaza kiume,ile kulipia kwa kadi nikaonekana doni sana pale.

basi na ile laki mkononi nayo nikaibunya mjini…..sahivi niko zangu kwenye katarama narudi zangu mkoani na somo.

Umewahi kutana na dhahama kama hii?!😂
 
mkuu,umekosea kuandika…nadhani ulikusudia 50,000/= ila umeandika 5000/=
5000 mkuu, hapo nilikua mwanafunzi mkuu nishazoea buku buku, kws pale niliona wakienda mbali buku 2, ila wakapita na buku 5 yangu. Ni hatari sana mkuu
 
Back
Top Bottom