Lax
JF-Expert Member
- Feb 10, 2022
- 4,740
- 7,179
Hatari sanatutafute hela mwananguššš
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hatari sanatutafute hela mwananguššš
š¤£Kabla sijampeleka Mtu sehemu naenda mwenyewe hiyo sehemu kuangalia na kuuliza bei, sitakagi hekeheka Mimi.... tangu niuziwe Ugali 30000 wakati Mfukoni nina 5000 nimejifunza
Mkuu buku 5 mbona ndogo hiyošNimecheka sana, eti kamoja kiherehere, mie nakumbuka nikiwa kikazi Dom mida ya saa 4 usiku nikaingia saloon nikwangue nywele, ile kumaliza bei kaniambia buku 5 na kunyoa kwenyewe ovyo, iliniuma hiyo buku 5
Mkuu pole Sana Hii Story yako imenichekesha Sanaaš¤£š¤£watoto ndio walinichuuzaā¦kumbe hapo wanaendaga kwenye zile class party na walimu waoā¦pana bei vibaya mno.
mimi mgeni mjini
šššArusha kuna hotel moja ya kihuni nilifikia hapo nikaona viloba vya konyagi kipindi vipo, nikakata vitatu fasta nikaweka na maji natoa ten naambiwa hela haitoshi kiloba kimoja 5000 iliniuma acha tu
š¤£š¤£š¤£š¤£ yaani umenichekesha mpaka watu hapa Target wamenishangaa sana!! š¤£š¤£ kweli wewe rudi tu huko mikoani maisha ya Dar huyawezi!! š¤£š¤£š¤£Nilienda kutembea Dar es Salaam kwa dada yangu wakati wa sherehe hizi za christimass.
Basi tarehe 25/12 kama kawaida tulikwenda ibadani na kurudi nyumbani,kilichofuata ni maongezi tu ya kifamilia huku tukichoma nyama jioni na kunywa pombe pamoja na shemeji na marafiki zake.
Tarehe 26/12 nikataka na mimi onyesha msuli wangu kwa shemeji ili asinichukulie poaā¦Basi bwana nikawaambia leo niachieni hawa vijana nitoke nao out nao waone raha ya kuwa na mjomba,wako watoto wanne na dada wa kazi. jumla watano.
Basi wao wenyewe wakataja mahala wanataka kwendaā¦ni beach fulani hivi wamejenga vizuri sana na kuna michezo mingi sana ya watoto,vyakula na vinywaji.
Basi tukaondoka tukafikaā¦kiukweli mimi nilidhani ni mahala naweza afford kulipia kila kitu na nilitenga 100,000/= nzima kwa ajili ya kutumbua.
Sasa kufika nikaambia kwanza vijana wapate chakula.Wakaagiza kila mmoja chipsi kavu pamoja na kuku nusu.Pia waliagiza juice freshi na kuna kamoja kiherehere kakaagiza pizza moja ya kushare woteā¦yule dada wa kazi kwa aibu za kikubwa aliagiza chipsi na mshkaki mmoja tu na juice.
Mahesabu yangu yalikua pale itakata kama 50,000/= hivi pamoja na michezo yao ileā¦wakamaliza kula,mimi mwenyewe nikaagiza bia zangu 5 pamoja na nyama choma ya mbuzi.
ā¦..sasa game ikaanza karibia wanamaliza kula yule dada ndio akaniletea ile āmenuā,lahaulaaaa
chipsi kavu-inasoma 6000/= mara 5
kuku nusu-inasoma 21,000/= mara 4
fresh juice-inasoma glass moja 6000/= mara 5
pizza moja-inasoma 35,000/=
mshkaki mmoja(niligundua wameandika fillet)-3500/=
nyama choma mbuziāinasoma 25,000/= per portion
bia moja local ni 4000/= mara 5
kwa haraka haraka ilisoma kama 227,500/= kinyume kabisa na matarajio yangu.
Kwanza nilihisi baridi sana imenichapa sababu vitu vyote vishaagizwa na vingine vishaanza kutumika,watoto wanaenjoy sana na huwezi waambia kitu wakakuelewa.
Hapo wanasubiri washibe nikawalipe kila mmoja 5000/= ya kwenda kwenye michezo yao ya watotoā¦
Mimi bhana nikajitetea nataka kulipa kwa kadiā¦walete mashine,lengo langu hapa kubahatisha sababu ndio zilikua tarehe bosi anaingiza chochote kwenye account.
Ile kugusa tu pyaaaaaā¦.nakuta sms inaingia umefanikiwa kulipia 227,500/= kwenda Utulivu beach resort,ikaja na sms ya muamala wa makato ya muamala kama 4000/= hivi.
Kwa kweli mood yote ilikataā¦kwa mshahara wangu hiko kiwango kilikua ni zaidi ya nusu yake mimi nimetumia kulipia watoto kula sehemu ambayo siyo level zanguā¦.ila nikakaza kiume,ile kulipia kwa kadi nikaonekana doni sana pale.
basi na ile laki mkononi nayo nikaibunya mjiniā¦..sahivi niko zangu kwenye katarama narudi zangu mkoani na somo.
Umewahi kutana na dhahama kama hii?!š