Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Juzi nilikutana na mwanafunzi wangu ambaye kwa Sasa ni Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Tulijadili mambo tofauti Ila Moja ya kilichomfurahisha ni namna alivyoaminishwa ni vigumu kwake kuwa Jaji lakini Katika ugumu huo akajikuta jina lake lipo KWENYE vyombo vya habari ameteuliwa Katika nafasi hiyo.
Kwa eneo alilokuwa anafanyia kazi na kwa uzoefu wake kisheria kazi ya ujaji aliona ni ngumu na hata alipokabidhiwa anaamini ni moja ya kazi yenye hadhi tofauti na iliyofungamanishwa na ukosefu wa Uhuru wakufanya mambo mengi Ila inayohitaji uzoefu Katika kutenda haki.
Kwa maoni yake, mfumo wa upatikanaji Majaji nchini unaambatana na mambo mengi magumu akiyataja.
1. Ni mfumo usiojali siniority, kwamba leo wapo mahakimu wamesota na Wana uzoefu na sifa elimu lakini inapokuja uteuzi wa Jaji wanaweza wakaachwa wakachukuliwa watu nje kabisa ya mfumo wa Mahakama na ambao baadhi yao awajawahi kuamua kesi hata Moja. Hata ungekuwa competent namna gani Uhuru wako wakuwaongoza Hawa mahakimu na watendaji wa Mahakama unapokwa kutokana na wao kukuzidi experience, unafanya maamuzi lakini ushauri mpana unaupata kwa walio chini Yako.
2. Jaji anapoteuliwa nje ya mfumo wa Mahakama na akiwa hana jina huko alikotoka anaachwa bila kupewa ushirikiano, haya tunayaona yanatokea mahakamani ambapo majaji wanatoa maamuzi then KWENYE rufaa maamuzi yao yanachanwachanwa kama vile walio Mahakama ya rufaa walisoma vyuo tofauti. Hii sometimes inatokea Kwa kukosa ushirikiano au kujiona Mimi jaji najua Kila kitu.
3. Upo ushirikina KWENYE Utumishi wa umma, kuteuliwa kinyume kabisa cha utaratibu au kuteuliwa wakaachwa wenye uzoefu kumepelekea wenye imani za kishirikina kuzijaribu NAFSI za majaji na wapo majaji wamepofuka.
4. Mahakama Tanzania inakosa Uhuru Kwa sababu utaratibu wa kumpata Jaji unaweza fanywa gizani na wakumwondoa pia ukafanywa gizani. Siku mahakama ikiweka utaratibu nuruni tutapona.
Pamoja na surprise ya ujaji lakini mwanafunzi huyu anaeleza wazi kwamba hakuna mahakama inayoweza kushindana na serikali na ndio maana hata mAh ikitoa baadhi ya hukumu serikali upinga kuzitekeleza.
Mwisho aliomba nimweke kwenye maombi ikiwezekana astaafu bila kuamua kesi yoyote kuliko Kustaafu akiwa amehukumu kinyume kabisa na dhamira Yake