Nilianza kupambana na maisha nikiwa bado mwanafunzi

Nilianza kupambana na maisha nikiwa bado mwanafunzi

Joined
Oct 5, 2026
Posts
31
Reaction score
51
Kuna watu ambao maisha yao huanza kuwa magumu baada ya kukua, lakini wapo ambao wanalazimika kukutana na uhalisia wa maisha wakiwa bado wadogo, wakati ambao walipaswa kuwa na jukumu moja tu: kusoma na kujenga msingi wa maisha yao ya baadaye.
Mimi ni mmoja wa watu hao.
Ninapoamua kuisimulia safari yangu, siandiki kwa sababu maisha yangu yamekuwa rahisi, wala siandiki kwa sababu kila kitu nilichokiota kimefanikiwa. Ninaandika kwa sababu kuna safari ambayo nimeipitia, kuna mambo ambayo nimeyaona, na kuna nyakati ambazo hata mimi mwenyewe nikizikumbuka, najiuliza nilipata wapi nguvu ya kuendelea.
Katika familia yetu nimezaliwa peke yangu. Sina kaka, dada wala mdogo wangu, na kwa sasa matumaini ya kupata ndugu wengine hayapo tena. Wazazi wangu wamezeeka sana, pia wana changamoto za kiafya

Tangu nikiwa shule, nilikuwa na uwezo wa kusoma na nilijituma sana. Nilifanya vizuri kiasi kwamba naamini jina langu lilianza kufahamika shuleni. Ndoto yangu kubwa ilikuwa kufanikiwa kupitia elimu ili siku moja niweze kuwasaidia wazazi wangu.

Nilipofaulu Form One, nilidhani safari yangu ya elimu ingeendelea vizuri. Lakini hali ya kifedha nyumbani haikuwa nzuri. Ada na maandalizi ya shule yakawa changamoto, nikachelewa kuripoti. Nilipokwenda, sikuwa hata na begi la madaftari, na nilikuwa na madaftari machache tu.
Wakati mwingine watu wanapomwona mwanafunzi amechelewa kuanza masomo, wanaweza kudhani hana nidhamu au hajali elimu yake. Lakini si kila kuchelewa kunatokana na uzembe. Wengine wanakuwa wanapambana na mambo ambayo hawawezi kuyaeleza mbele ya kila mtu.


Wakati huohuo, afya ya Mzee wangu ilizidi kudhoofika hadi akawa mtu wa kitandani. Uwezo wa familia kutafuta kipato ukapungua, huku mahitaji kama kodi, chakula na matibabu yakiendelea kuwepo.


Mama ndiye aliyebeba jukumu kubwa. Alikuwa anakwenda machinjioni, anakusanya nyama na utumbo, kisha anavitembeza majumbani ili kupata fedha za kuendesha familia.


Nilipoona hali hiyo, nilianza kujisikia kwamba nilipaswa kusaidia kwa namna yoyote niliyoweza. Nikaanza kufanya vibarua vya kufyatua tofali, kulima na saidia fundi pale fursa ilipopatikana.


Wakati mwingine nilipopata kazi, nilikosa kwenda shule. Si kwamba nilikuwa nimechoka kusoma, bali nilikuwa nimejikuta katikati ya majukumu ya nyumbani.


Nilikuwa na ndoto kubwa, lakini mazingira yalikuwa yakinilazimisha kupambana na maisha nikiwa bado mwanafunzi.


Sikujua kwamba hatua hizi ndizo zingekuwa mwanzo wa misukosuko ambayo baadaye ingeathiri zaidi safari yangu ya shule.


ITAENDELEA...
 
Katika familia yetu nimezaliwa peke yangu. Sina kaka, dada wala mdogo wangu, na kwa sasa matumaini ya kupata ndugu wengine hayapo tena. Wazazi wangu wamezeeka sana, pia wana changamoto za kiafya

Tangu nikiwa shule, nilikuwa na uwezo wa kusoma na nilijituma sana. Nilifanya vizuri kiasi kwamba naamini jina langu lilianza kufahamika shuleni. Ndoto yangu kubwa ilikuwa kufanikiwa kupitia elimu ili siku moja niweze kuwasaidia wazazi wangu.

Nilipofaulu Form One, nilidhani safari yangu ya elimu ingeendelea vizuri. Lakini hali ya kifedha nyumbani haikuwa nzuri. Ada na maandalizi ya shule yakawa changamoto, nikachelewa kuripoti. Nilipokwenda, sikuwa hata na begi la madaftari, na nilikuwa na madaftari machache tu.
Wakati mwingine watu wanapomwona mwanafunzi amechelewa kuanza masomo, wanaweza kudhani hana nidhamu au hajali elimu yake. Lakini si kila kuchelewa kunatokana na uzembe. Wengine wanakuwa wanapambana na mambo ambayo hawawezi kuyaeleza mbele ya kila mtu.


Wakati huohuo, afya ya Mzee wangu ilizidi kudhoofika hadi akawa mtu wa kitandani. Uwezo wa familia kutafuta kipato ukapungua, huku mahitaji kama kodi, chakula na matibabu yakiendelea kuwepo.


Mama ndiye aliyebeba jukumu kubwa. Alikuwa anakwenda machinjioni, anakusanya nyama na utumbo, kisha anavitembeza majumbani ili kupata fedha za kuendesha familia.


Nilipoona hali hiyo, nilianza kujisikia kwamba nilipaswa kusaidia kwa namna yoyote niliyoweza. Nikaanza kufanya vibarua vya kufyatua tofali, kulima na saidia fundi pale fursa ilipopatikana.


Wakati mwingine nilipopata kazi, nilikosa kwenda shule. Si kwamba nilikuwa nimechoka kusoma, bali nilikuwa nimejikuta katikati ya majukumu ya nyumbani.


Nilikuwa na ndoto kubwa, lakini mazingira yalikuwa yakinilazimisha kupambana na maisha nikiwa bado mwanafunzi.


Sikujua kwamba hatua hizi ndizo zingekuwa mwanzo wa misukosuko ambayo baadaye ingeathiri zaidi safari yangu ya shule.


ITAENDELEA...
Hizi stori zako fupi fupi kaandike kwenye channel za Whatsapp uanze kulipisha followers....utapata pesa.
 
IMG-20250405-WA0361.jpg
 
Hizi stori zako fupi fupi kaandike kwenye channel za Whatsapp uanze kulipisha followers....utapata pesa.
Mkuu, samahani, hivi ni sehemu gani nimeandika kwamba nina shida na pesa au natafuta pesa kupitia hii story?
 
Tuendelee Sehemu ya pili mtanisamehe kama mwandiko mbaya

SEHEMU YA PILI: Nilianza kupambana na maisha nikiwa bado mwanafunzi​


Wakuu, karibu tena kwenye mwendelezo wa simulizi yangu. Kama umepitwa na sehemu ya kwanza, tafuta uisome ili uelewe nilikotoka na namna safari yangu ilivyoanza.


Baada ya kujishughulisha na vibarua vya hapa na pale, nilianza kupata vijisenti. Haikuwa pesa nyingi, lakini kwa mtu aliyekuwa na ndoto kubwa kama mimi, kila shilingi ilikuwa na maana yake.


Nilikaa chini nikawaza sana. Nikajiuliza, hivi hii pesa nikiitumia tu kwenye matumizi ya kila siku, nitafika kweli kule ninapotaka kwenda?


Ndipo nikapata wazo la kuanzisha biashara.


Tatizo lilikuwa moja tu: nilikuwa mwanafunzi, na sheria za shule hazikuruhusu kufanya biashara.


Lakini mimi kichwani nilikuwa nimeshajiona kama mfanyabiashara mkubwa. Nilikuwa naona fursa mahali ambapo wengine hawakuona kitu.


Nikatenga kiasi kidogo cha pesa niliyokuwa nimepata, nikaanza kutengeneza bagia.


Siku ya kwanza nilikuwa na mkakati wangu wa kipekee. Nikasema lazima watu waijue biashara yangu, na njia pekee ya kuwafanya waijue ni kuwapa nafasi ya kuonja bidhaa yangu.


Basi wakuu, siku hiyo nikatoa ofa ya bure!


Nilianza kuwagawia baadhi ya wanafunzi wenzangu kuanzia Form One hadi Form Four. Sikuwa nagawa kwa kila mtu, lakini nilihakikisha watu kadhaa wanapata nafasi ya kuonja bagia zangu.


Nilichokuwa nakitafuta siku hiyo hakikuwa faida. Nilikuwa natafuta wateja.


Na kweli, mpango wangu ulianza kufanya kazi.


Wanafunzi wakaanza kupenda bidhaa yangu. Break time ikawa muda wangu wa kazi. Watu wakaanza kuniulizia bagia, wengine wakawa wanaweka oda mapema.


Lakini kitu kilichonishangaza zaidi ni kwamba wateja wangu wengi walikuwa wadada.


Wakuu, hapo ndipo nilipoanza kuelewa kwamba biashara inahitaji zaidi ya kuwa na bidhaa tu. Unahitaji kujua wateja wako wanataka nini, uwafikie kwa wakati, na uhakikishe hawakosi wanachokihitaji.


Polepole, jina langu likaanza kujulikana.


Faida ikaanza kuonekana. Siku nyingine nilikuwa napata shilingi 2,500, siku nyingine 3,000, na siku nzuri kabisa nilikuwa nafika shilingi 3,500.


Kwa mtu mzima, labda hizo pesa zilikuwa za kawaida. Lakini kwa mimi niliyokuwa bado mwanafunzi, zilikuwa pesa zilizonifanya nianze kuota ndoto kubwa zaidi.


Pesa ilianza kuwa tamu. Na ukweli ni kwamba, utamu wa pesa ukiingia kichwani mapema, unaweza kukufanya usahau hata mambo yaliyokuwa muhimu kuliko hiyo pesa yenyewe.

Kadiri siku zilivyokuwa zinakwenda, biashara yangu ilianza kukua. Mtaji ukaongezeka, nikaanza kufikiria namna ya kuongeza uzalishaji na kusambaza bidhaa sehemu nyingine.


Nikaanza kumpelekea mzigo dada mmoja aliyekuwa na duka. Nilifanikiwa kumshawishi aingize bagia zangu kwenye biashara yake, na mara kwa mara alikuwa anachukua mzigo wangu. Nilikuwa nikimpa posho kidogo ili kazi iende vizuri.


Wakuu, hapo sasa nilianza kujiona nimepiga hatua.


Nilikuwa na biashara shuleni, biashara mtaani, na mtu mwingine anayesaidia kuuza bidhaa zangu.


Kichwani mwangu nilikuwa na mipango mingi sana. Nilianza kufikiria nitapanua biashara kiasi gani, nitaongeza mtaji kiasi gani, na nitafika wapi nikizidi kuendelea hivi.


Lakini kuna jambo moja nilikuwa nalisahau.nilikuwa Bado mwanafunzi

Kadiri biashara ilivyokuwa inakua, ndivyo masomo yalivyoanza kupoteza nafasi yake kwenye maisha yangu.


Kuna siku nilikuwa naona bora niende mtaani kutembeza mzigo kuliko kwenda darasani. Siku nyingine nilikuwa nakosa shule kabisa kwa sababu nilikuwa naangalia biashara.


Mwanzoni nilijipa moyo kwamba nitakuja kurekebisha mambo. Nilijiambia biashara ikiimarika nitajikita kwenye masomo.


Lakini wakuu, mara nyingi mtu akishaanza kuonja mafanikio ya haraka, ni rahisi sana kujidanganya kwamba anaweza kuendesha kila kitu kwa wakati mmoja.


Bila kujua, nilianza kuitelekeza shule yangu mwenyewe.

Kitu kilichonifanya nijione nina akili ya biashara ni pale nilipoanza kufikiria namna ya kumsaidia mama.


Nilimshauri aanze kuuza mkaa nyumbani ili apunguze kutembea huku na kule kutafuta riziki.


Nilikuwa na kiasi fulani cha pesa, nikampa. Mama akaongeza na pesa zake, akaanza biashara ya mkaa.


Nilifurahi kuona kwamba mawazo yangu hayakuwa yananiendeleza mimi tu, bali yanaweza pia kuisaidia familia.


Lakini kuna kitu nilikuwa sijakiona.


Mama naye alianza kuona jinsi nilivyokuwa napenda biashara kuliko shule. Na kadiri nilivyoendelea kuipa biashara muda mwingi, ndivyo nilivyozidi kujitengenezea matatizo ambayo sikuwa nimeyapanga.


Siku moja, mambo yakabadilika kabisa.


Barua ikaletwa nyumbani kutoka shuleni.


Ilikuwa ni taarifa kwamba mzazi alitakiwa kufika shuleni pamoja na mimi ili kutoa maelezo kuhusu sababu za kutohudhuria masomo.


Wakuu, ile barua ilipofika nyumbani nilijua tu kwamba sikuwa na jinsi ya kuikwepa hali hiyo.


Nikajiandaa, tukaenda na mama shuleni.


Nilikuwa na matumaini kwamba mama angeeleza hali ilivyokuwa, labda mambo yangemalizika kwa mazungumzo.


Lakini nilichokutana nacho siku hiyo kiliniacha bila maneno.


Tulipofika shuleni, mama alianza kueleza mambo yake. Kadiri alivyokuwa akiongea, ndivyo nilivyozidi kushangaa.


Kwa namna nilivyoelewa, badala ya kueleza kwa utulivu sababu zilizokuwa nyuma ya tabia yangu, mama alionekana kunigeuka. Alisema siku hizi nilikuwa nimekuwa jeuri na sitaki kusoma.


Wakuu, nilihisi kama nimeachwa peke yangu mbele ya watu.


Sikuwa nasema kwamba nilikuwa sahihi kwa kutohudhuria shule. Nilijua nilikuwa nimekosea. Lakini ndani yangu nilikuwa na mambo mengi ambayo nilitamani yaeleweke.


Hata hivyo, sikuwa na nafasi ya kuyaeleza kwa namna niliyotaka.


Na hapo ndipo adhabu ilipokuja.

Wakuu, kuna walimu ambao hata ukisikia tu wanaitwa, moyo unabadilika.


Shuleni kwetu kulikuwa na mwalimu mmoja tuliyependa kumuita Mjeshi.


Jina hilo halikuwa la bahati mbaya. Siku hiyo nilijua kwa nini tulikuwa tunamuita hivyo.


Adhabu ilianza, na nikajikuta nikishikwa mikono na wanafunzi wawili huku wengine wakinishika miguu. Kwa hali niliyokuwa nayo, nilijikuta nimeinuliwa juu, kisha nikapokea kipigo ambacho mpaka leo nakikumbuka.


Wakuu, ile siku ilikuwa ngumu sana kwangu.


Maumivu ya mwili yalikuwa upande mmoja, lakini aibu na mawazo yaliyokuwa kichwani mwangu yalikuwa upande mwingine.


Nilijiuliza, hivi nimefika hapa kwa sababu gani? Nilianza biashara ili niboreshe maisha yangu, iweje sasa imekuwa sababu ya kunirudisha nyuma?


Siku hiyo nilisema moyoni mwangu kwamba nimechoka.


Nikaamua kuacha mambo ya biashara na kujikita kwenye masomo.


Nilirudi nyumbani, lakini mwili haukuwa sawa. Niliugua kwa wiki nzima.


Ilikuwa ni moja ya nyakati ambazo nilihisi nimefika mwisho wa nguvu zangu.


Nilikuwa nimeingia kwenye biashara nikiwa na matumaini ya kujikwamua, lakini sasa nilikuwa nimejikuta kwenye hali ambayo sikuwa nimeitarajia.


Baada ya kupona, nilianza tena kujikita kwenye masomo.


Nilijaribu kurudi kwenye mstari. Nikajiambia lazima nimalize shule vizuri, hata kama biashara italazimika kusubiri.


Lakini wakuu, kuna kitu nilikuwa sijakijua vizuri kuhusu pesa.


Ukiishazoea pesa ya biashara, kuiacha kabisa si jambo rahisi. Ni kama unakuwa umeingia nayo mkataba bila kusaini popote!


Nilivumilia kwa wiki tatu hivi.


Baada ya hapo, nikaanza tena kuikimbiza biashara wakati wa weekend. Siku za shule nilijaribu kuhudhuria masomo, lakini nilikuwa bado na mawazo mengi kuhusu biashara yangu.


Mtihani ulipofika, nikafanya mtihani na shule ikafungwa kwa likizo.


Nilipoona tumefunga, nilifurahi sana!


Sio kwamba nilikuwa nimefurahia matokeo yangu. Nilifurahi kwa sababu niliona nimepata nafasi ya kupumua na kuendelea na biashara bila bughudha ya kwenda shule kila siku.


Lakini nilipokuja kuona matokeo yangu, nilikutana na ukweli ambao haukuwa mtamu hata kidogo.


Nilikuwa nimeshuka kutoka nafasi ya tatu bora hadi nafasi ya ishirini.


Kutoka Top 3 mpaka Top 20!


Wakuu, kwa mtu aliyekuwa anasoma kwa bidii na kuzoea kufanya vizuri, hayo yalikuwa mabadiliko makubwa.


Lakini cha kushangaza ni kwamba sikuumia sana.


Nilijipa moyo kwamba tumefunga shule na sasa nitakuwa huru kuendelea na biashara.


Hapo ndipo nilipogundua kwamba nilikuwa nimeanza kuipa pesa nafasi kubwa kuliko elimu yangu.

Likizo ilipoanza, biashara yangu iliyumba kidogo. Mtaji haukuwa mkubwa kama nilivyotaka, na mambo hayakwenda vizuri kila wakati.


Hata yule dada mwenye duka, niliyokuwa nikimpelekea bagia, nilipunguza kumpelekea mzigo.


Lakini mimi sikuwa mtu wa kukaa chini nikisubiri bahati.


Nikatafuta kazi ya siku ya kubeba tofali.


Wakuu, nilifanya hiyo kazi kwa sababu nilikuwa na lengo. Nilihitaji kupata pesa ya kuongeza mtaji wangu.


Baada ya kupata pesa, nikaja na wazo lingine.


Nikaanza kurangua miwa bondeni nikaweka nyumbani mama akiendelea kuuza mkaa nyumbani huku anauza na miwa, na mimi nikiendelea na biashara yangu ya bagia.


Nilianza tena kumpelekea yule dada mzigo wa bagia, lakini wakati huohuo nilikuwa na mzigo mwingine ninaoutembeza mtaani.


Polepole, nikaanza kupata wateja wa kudumu.


Kila siku nilikuwa napitisha mzigo, na kadiri siku zilivyopita, faida ikaanza kuonekana.


Nilikuwa nafurahia kuona juhudi zangu zinaanza kuzaa matunda.


Nikaanza kutengeneza kisanduku changu cha siri, nilichokuwa nakificha na kuweka kiasi cha pesa kila nilipopata faida.


Nilikuwa na mpango maalumu.


Nilijiambia baada ya likizo kuisha, nitakivunja kile kisanduku, nijue nimekusanya kiasi gani na nianze kupanga hatua inayofuata.


Kila nilipoweka pesa ndani yake, nilihisi niko hatua moja karibu na ndoto zangu.


Sikuwa najua kwamba siku moja tu ingeweza kubadilisha kila kitu.

Wakuu, hapa ndipo nilipoanza kujua kwamba si kila mtu anayekuja nyumbani kwako anakuja na nia unayodhani.


Likizo ilikuwa inaelekea mwisho. Zilibaki kama siku tano hivi shule zifunguliwe.


Siku moja ndugu yetu mmoja alikuja kutusalimia nyumbani.


Siku hiyo sikuwa katika hali nzuri. Sikujisikia vizuri, na kwa hiyo sikuweza kuandaa mzigo wangu kama kawaida.


Pesa zangu zilikuwa bado zimehifadhiwa . Baadhi zilikuwa ndani ya kile kisanduku changu cha siri, na nyingine zilikuwa ndani ya begi.


Siku hiyo nilikuwa na mambo mengine ya kufikiria, bila kujua kwamba jambo kubwa zaidi lilikuwa linakuja.


Baadaye, nilipokuja kuangalia pesa zangu... Ili niandae hali ikiwa sawa nifate miwa bondeni niandae na mzigo wangu

Nilianza kutafuta huku na kule. Nikajiuliza labda nilikuwa nimekibadilishia sehemu, lakini kadiri nilivyoendelea kutafuta, ndivyo nilivyozidi kupata hofu.


Haikuishia hapo.


Pesa nyingine zilizokuwa ndani ya begi nazo zilikuwa zimepotea!


Wakuu, nilibaki nimesimama bila kujua nifanye nini.


Pesa niliyokuwa nimehangaika kuitafuta kwa kufanya vibarua, kutembeza bagia, kuuza miwa na kujinyima mambo mengi, ilikuwa imepotea ndani ya muda mfupi.


Na mtu niliyemhisi kuhusika na tukio hilo alikuwa ni yule ndugu aliyekuja kutusalimia.


Kwa nilivyoelewa, alikuwa amechukua kisanduku changu pamoja na pesa nyingine, kisha akaondoka.


Nililia sana, wakuu.


Sio kwa sababu tu nilikuwa nimepoteza pesa, bali kwa sababu nilikuwa nimepoteza jasho langu.


Nilikuwa nimeanza kuona mwanga mbele yangu. Nilikuwa na mipango mingi sana kwa pesa zile. Nilikuwa nimejinyima, nimefanya kazi ngumu, na nilikuwa najipa moyo kwamba siku moja juhudi zangu zingebadilisha maisha yangu.


Sasa kila kitu kilionekana kuwa kimefutika.

Na kilichoniumiza zaidi ni kwamba shule ilikuwa inafunguliwa baada ya siku tano tu.


Nilijiuliza nitafanyaje? Nitarudije shule wakati kichwani mwangu nilikuwa na mipango ya biashara, lakini sasa sikuwa na mtaji wa kuanzia?


Nilikuwa nimepambana na maisha, nikajenga kitu kidogo kwa mikono yangu mwenyewe, halafu kwa muda mfupi nikajikuta nimerudi pale nilipoanzia.


Wakuu, kama umewahi kufanya kazi kwa jasho lako halafu ukapoteza kila kitu ghafla, utajua maumivu niliyokuwa nayapitia siku hiyo.


Usiku ulipofika, mawazo hayakuniruhusu kupumzika vizuri.


Nilikuwa najiuliza maswali mengi bila kupata majibu.


Je, ningeweza kuanza tena kutoka sifuri?


Je, ningeweza kurudi shule na kuendelea na maisha kama kawaida?


Na zaidi ya yote, je, ningeweza tena kumwamini mtu baada ya jambo lile lililonitokea?


Nilikuwa sijui kwamba siku tano zilizokuwa zimebaki kabla ya shule kufunguliwa zingekuwa na maana kubwa sana katika maisha yangu.


Wakuu, hapa ndipo sehemu hii inaishia.

Tuonane sehemu ya tatu, tuendelee na safari hii ya maisha. 🙏🏽
 
Back
Top Bottom