Harakati za maisha zilinifikisha kijiji kinachoitwa Chiuta huko mkoani Lindi. Kijiji kipo eneo fulani ndani na uwanda wa juu (Makonde plateau) kama unaelekea Tandahimba ukitokea mji wa Mtama (kwa watoto 😆😆😆).
Miaka yangu michache niliyoishi kule nikifanikisha jambo fulani hivi, aisee nilichezewa na wanga haswa, hilo lazima nikiri.
- Niliamshwa mara nyingi tu nikiwa nimevuliwa nguo, hapa nilikuwa nahisi kabisa abdala kichwa-wazi wangu amechezewa kwa kuvutwa vutwa hovyo hovyo. Nilikuwa nayahisi kabisa maumivu ya mvuto.
- Nimeshaitwa jina langu na 'kuitika' nikiwa natokea usingizini mara kadhaa.
- Vitu vyangu vimetoweka kimazingara mara nyingi tu.
- Mtu kuliita jina langu kisha kutoweka.
- Mbweha kuniamkia.
- Bundi kuniletea mzigo wa kuni kichwani n.k.
Kiufupi nilichezewa na nikachezeka, walinizoea hadi kufikia hatua ya kunidharau kwa kunicheka kabisa vijiweni. Yaani unapigwa dongo fulani unajua tu kuwa ninayeambiwa ni mimi. Mfano, 'kuna watu ikifika usiku ni malofa tu'.
Katika yote, lile la kwanza linaniuma mpaka leo. Vimaombi vyangu havikusaidia kitu katika kunifikia. Natamani kufurahi ninaposikia mmoja ya wazee ambaye, kwa utemi wake wa kichawi, alijiweka wazi kabisa kwangu kama mmoja ya waliokuwa wananichezea amefariki, anapambana na hali yake huko sasa!
Yote kwa yote, nashukuru nilitoka salama eneo lile aisee!