Nilichogundua kutoka kwa mwamuzi Nassir Salim (Azam FC vs Simba SC) fainali ya Mapinduzi Cup

Mwamuzi Nassir Salim wa Zanzibar aliyechezesha fainali ya Kombe la Mapinduzi kati ya Azam FC na Simba SC hakuwa na ufahamu kuhusu sheria ya mchezaji kurudisha mpira kwa golikipa wake. Mwamuzi huyu alikuwa anajua kwamba mpira wowote uakaorudishwa na mchezaji kwa golikipa wake ni faulo. Alifanya hivyo katika matukio mawili:

1. Wakati golikipa Mathias Kigonya alipomchezea rafu mbaya Pape Sackho, mwamuzi alikuwa hajaliona tukio hili la rafu, ila alikuwa ameliona na kulitolea adhabu tukio lililofanyika kabla Kigonya hajacheza faulo. Alichokiona ni beki wa Azam akirudisha kwa golikipa wake akitumia kichwa. Mwamuzi akatafsiri ni kosa na ndio maana akatoa adhabu ya indirect kick ndani ya box la Azam. Tukio hili waliligundua wachache maana lilikuja kufunikwa na maamuzi mapya baada ya mwamuzi msaidizi na fourth official kumuita kwenye kibendera na kumueleza kuwa kuna faulo mbaya amefanyiwa Sackho, na ndipo ikawa penati, otherwise isingekuwa Sackho amfanyiwa faulo wengi mngeshangazwa na uamuzi wa indirect kick kwa sababu kipa amerudishiwa mpira, wakati sheria inaruhusu kurudishiwa kwa kichwa au kifua

2. Tukio la pili ni pale Onyango alipourudisha mpira nyuma, Henock Inonga akaubetua na kuuinua kisha akaupiga kichwa kumpa Manula. Cha kushangaza mwamuzi akakimbilia aliposimama Inonga na kuamuru ipigwe indirect kick, na hii ndio iliyakuwa dhahiri maana ilipigwa ingawa kila anayejua sheria za soka alishangaa

View attachment 2080189
Unajifanya unajua kumbe huna unalo lijua
 
Kwa nini refa alipiga filimbi kabla Manula hajaushika mpira? Sheria hii inazuia back pass pale ambapo golikipa ataukamata kwa miguu, lakini back pass huku kipa akiucheza kwa miguu inaruhusiwa. Ina maana Inonga angeurudisha kwa mguu halafu Manula angeendelea kuwa nao mguuni na kucheza tena pasi, nalo pia ni kosa?

View attachment 2080293
wote wanaojua Sheria za mpira Inonga aliporudisha mpira kwa Manula wote waliwaza aliunawa ,lakini si vinginevyo
 
Nimeuliza swali lakini sijajibiwa bado. Mbona alipourudisha mpira nyuma, Manula hakuukamata kwa mikono ila refa akapiga filimbi ya kosa? Mimi nijuavyo kipa anachokatazwa ni kudaka/kushika mpira uliorudishwa nyuma kwa makusudi, lakini anaweza kuucheza kwa miguu
Refa alitafsiri lengo na nia ya mchezaji!
 
Nimeuliza swali lakini sijajibiwa bado. Mbona alipourudisha mpira nyuma, Manula hakuukamata kwa mikono ila refa akapiga filimbi ya kosa? Mimi nijuavyo kipa anachokatazwa ni kudaka/kushika mpira uliorudishwa nyuma kwa makusudi, lakini anaweza kuucheza kwa miguu
Sio lazima audake soma vizuri sheria
 
Kwa Inonga referee alikua sahihi, Ila kwa Sacko mwamuzi hakuona tukio ndio maana hakumpa nyekundu, Ila ilipaswa apewe nyekundu na penati. Kwa sababu ile ilikua violence faul sio reckless.
Violent foul ndio ila hakumnyima opponent nafasi ya kufunga Mana mpira alikuwa ashaudaka ndipo faulo ikafuatia. Na haikuwa ndani ya eneo la golikipa. Hivyo ilipaswa kuwa red card na indirect kick
 
Mwamuzi Nassir Salim wa Zanzibar aliyechezesha fainali ya Kombe la Mapinduzi kati ya Azam FC na Simba SC hakuwa na ufahamu kuhusu sheria ya mchezaji kurudisha mpira kwa golikipa wake. Mwamuzi huyu alikuwa anajua kwamba mpira wowote uakaorudishwa na mchezaji kwa golikipa wake ni faulo. Alifanya hivyo katika matukio mawili:

1. Wakati golikipa Mathias Kigonya alipomchezea rafu mbaya Pape Sackho, mwamuzi alikuwa hajaliona tukio hili la rafu, ila alikuwa ameliona na kulitolea adhabu tukio lililofanyika kabla Kigonya hajacheza faulo. Alichokiona ni beki wa Azam akirudisha kwa golikipa wake akitumia kichwa. Mwamuzi akatafsiri ni kosa na ndio maana akatoa adhabu ya indirect kick ndani ya box la Azam. Tukio hili waliligundua wachache maana lilikuja kufunikwa na maamuzi mapya baada ya mwamuzi msaidizi na fourth official kumuita kwenye kibendera na kumueleza kuwa kuna faulo mbaya amefanyiwa Sackho, na ndipo ikawa penati, otherwise isingekuwa Sackho amfanyiwa faulo wengi mngeshangazwa na uamuzi wa indirect kick kwa sababu kipa amerudishiwa mpira, wakati sheria inaruhusu kurudishiwa kwa kichwa au kifua

2. Tukio la pili ni pale Onyango alipourudisha mpira nyuma, Henock Inonga akaubetua na kuuinua kisha akaupiga kichwa kumpa Manula. Cha kushangaza mwamuzi akakimbilia aliposimama Inonga na kuamuru ipigwe indirect kick, na hii ndio iliyakuwa dhahiri maana ilipigwa ingawa kila anayejua sheria za soka alishangaa

View attachment 2080189
Umendika kama unazijua sheria za soccer lakini acha nikwambie HUJUI KITU.
Refa alikuwa sahihi kabisa, ni kosa kumrudishia kipa wako mpira ambao haukua katika movement kwa kuubetua kutoka chini na kuupiga kwa kichwa kwenda kwa kipa hata kama kipa hataudaka bado litakuwa kosa. Tujifunze kupitia sheria na kanuni za mpira wa miguu pamoja na marekebisho yake madogo ya mara kwa mara.
 
Kwa nini refa alipiga filimbi kabla Manula hajaushika mpira? Sheria hii inazuia back pass pale ambapo golikipa ataukamata kwa miguu, lakini back pass huku kipa akiucheza kwa miguu inaruhusiwa. Ina maana Inonga angeurudisha kwa mguu halafu Manula angeendelea kuwa nao mguuni na kucheza tena pasi, nalo pia ni kosa?

View attachment 2080293
Haijalishi kipa ataudaka au hata daka lakini adhabu ipo palepale, unaadhibiwa kwa kusudio. Angeurudisha kwa mguu lisingekuwa kosa, kosa ni kuubetua kwa mguu na kuurudisha kwa kichwa wakati mpira haukuwa katika movement yoyote.
 
Huyo ni Ivan Perisic mchezaji Mkubwa tu alipewa kadi kwa kitendo kama cha Inonga, Lakini wana Simba hawatakiView attachment 2080383
Mkuu, naomba kwa utulivu kabisa usome swali langu. Baada ya kulisoma na kulielewa ndipo unijibu (unielimishe).

Tukio uliloliweka la Ivan Perisic, golikipa aliporudishiwa aliukamata mpira kwa mikono. Mimi ninachosema, refarii wa Zanzibar aliashiria kosa akapiga filimbi wakati Manula anao mpira miguuni, na hakuukamata kwa mikono. Sasa kuanzia hapo naomba uniambie (unielimishe), Je, adhabu ipo pale pale bila kujali golikipa aliyerudishiwa mpira ameucheza kwa miguu wala mikono?

1642146063547.png

1642146135730.png
 
View attachment 2080487

View attachment 2080490
Mkuu nshasema pale kilichofanyika refa alitafsiri tukio la henock ni upotezaji muda pasipo sababu za msingi. Mpira ulikuwa miguuni, hakuwa kwenye mazingira hatari Mana alikuwa na nafasi ya kuendelea kucheza kawaida ila yeye akaulazimisha mpira utoke kwenye kuchezwa kwa mguu kwenda kwenye motion ya mpira Wa kichwa.
 
Violent foul ndio ila hakumnyima opponent nafasi ya kufunga Mana mpira alikuwa ashaudaka ndipo faulo ikafuatia. Na haikuwa ndani ya eneo la golikipa. Hivyo ilipaswa kuwa red card na indirect kick
Kwanza unaonekana ukuangalia mpira, kwa kitendo Cha kusema ilikua nje ya penalty area. Pili, Violent foul yoyote ina red card. Na kwa vile ni ndani ya penalty area ilikua viendane na adhabu ya penalty. Mfano ingekua ni reckless foul kwamba alikua anafanya tackling mpira Sasa kaukosa hapo ndo ilitakiwa apewe yellow card na penalty. Violent foul hata iwe katikati ya uwanja ni direct red card
 
Kwa Inonga ilikuwa sahihi Mana pale inaangaliwa dhamira yake kwamba ni kupoteza muda Kwa wazi kabisa pasipo sababu za msingi. Henock alikuwa peke yake angeweza kuendeleza tu mchezo hivyo hakukuwa na sababu za kufanya vile. Kwa tukio la sacko refa alichemka kutoa penati. Ilipaswa kuwa faulo ndani ya 18 na red card kwa kipa!
Uko serious ile ni freekick!!!!!!!?Ukiondoa mahaba ile ni penalti halali tu
 
Back
Top Bottom