Ukipata huo ufafanuzi wa hiyo sheria na kanuni ulete hapa jukwaani tuelimike wote.Naendelea kusema, haya ni mapya kwangu na sikuyajua kabla, sikujua kama mchezaji kuubetua mpira kwa miguu na kisha kuurudisha kwa kipa wake kwa kutumia kichwa ni kosa, lakini mchezaji huyo huyo kuupiga mpira moja kwa moja kwa kipa wake kwa kutumia mguu sio kosa, bila kujali kipa amekamata au hajakamata mpira kwa mikono. Hakika elimu haina mwisho. Hata hivyo nasisitiza sitayapokea moja kwa moja, nitayachunguza kwanza
Zanzibar wanamarefa Bora sana,wangewepo huku bara Simba na Yanga wasingekuwa wanapata mteremko kirahisiView attachment 2080195
hicho kifungu unakielewaje mkuu
hapa hatujadili makosa ya refa tu,tunajifunza piaYagangwe yajayo...
Sawa ni muhimu wote tunaendelea kujifunza!Naendelea kusema, haya ni mapya kwangu na sikuyajua kabla, sikujua kama mchezaji kuubetua mpira kwa miguu na kisha kuurudisha kwa kipa wake kwa kutumia kichwa ni kosa, lakini mchezaji huyo huyo kuupiga mpira moja kwa moja kwa kipa wake kwa kutumia mguu sio kosa, bila kujali kipa amekamata au hajakamata mpira kwa mikono. Hakika elimu haina mwisho. Hata hivyo nasisitiza sitayapokea moja kwa moja, nitayachunguza kwanza
Hii hapaToeni reference basi na wengine tukasome hiyo sheria
Wanachomaanisha kosa ni la Inonga sio Manula na ndio maana faulo ilitengwa alipokuwa inongaHuyu Kipa aliuchukua Moira kwa mikono lkn kwenye mechi ya Simba : Manula aliuchukua kwa miguu
Nimeuliza swali lakini sijajibiwa bado. Mbona alipourudisha mpira nyuma, Manula hakuukamata kwa mikono ila refa akapiga filimbi ya kosa? Mimi nijuavyo kipa anachokatazwa ni kudaka/kushika mpira uliorudishwa nyuma kwa makusudi, lakini anaweza kuucheza kwa miguu