Nilichogundua shida maofisini kwenye utoaji wa huduma hazipo kwa Mabosi, zipo kwa wasaidizi

Nilichogundua shida maofisini kwenye utoaji wa huduma hazipo kwa Mabosi, zipo kwa wasaidizi

Kikwava

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2015
Posts
1,741
Reaction score
1,068
Husika na mada hapo juu tunawaomba MA-PS (Baadhi), huko MAOFISINI mtuhudumie kwa upendo na kwa haraka, nimefanya utafiti kidogo nimegundua kumbe mabosi wana moyo wa kutuhudumia Ila wanakwamishwa na masekretari wao.

Mfano;
1. Ps unamsalimia hakujibu kwa makusudi.
2. Ps anakataa usionane na boss umwambie shida yako.
2. Ps anakaa na file lako mpaka siku 3 bila kumpelekea Boss.
3. Ps anakununia bila sababu
4. Barua yakuandika dk20 anasema uende baada ya siku 3
IKUMBUKWE, KUHUDUMIA WATU KWA MOYO NA UPENDO NI IBADA, Badilikeni.
 
Jaribuni kuwapa vi-TIPS na motisha na hamasa pia; wengi wao wako hapo lakini kazi husika hawaipendi kutoka moyoni. Hakuna mtu anayeipenda kazi yake, then akaifanyia mzaha kiasi hicho.

Huduma mbovu ni ishara ya kukosa elimu ya kutosha, kutojitambua, na kutojiamini.
 
Jaribuni kuwapa vi-TIPS na motisha na hamasa pia; wengi wao wako hapo lakini kazi husika hawaipendi kutoka moyoni. Hakuna mtu anayeipenda kazi yake, then akaifanyia mzaha kiasi hicho.

Huduma mbovu ni ishara ya kukosa elimu ya kutosha, kutojitambua, na kutojiamini.
Yah! Upo sahihi mkuu, wengi wanafanya kazi Kama hawataki.
 
Kuna PS kalikuwepo pale UDOM ofisi ya Directorate of Undergraduate Studies

Yule Dada mse.ng....eeee sana sijui yuko wapi nowdays
Hawa watu baadhi ni shida kwakweli ukiingia kwenye 18 zao watakunyanya Sana, anaweza kukwambia boss hayupo huku unasikia anaongea na simu.
 
Sionagi umuhimu wa hao watu huko serikalini hizo nafasi kwanza zingefutwa tu mbona mashirika yasiyo ya kiserikali haya huo ujinga ujinga hivi, watu waandika report wenyewe
Bora kuwepo na foleni tu yakusikilizwa shida zetu kuliko kuwepo kwa Hawa ma-ps huwa wanatuondolea mood mpaka tunaichukia ofs kabsa
 
Wengi wao huwa wana upeo mdogo mno wa akili + hekima! Wewe ukitaka kuwapatia ukifika tuu anza na kumpongeza hata kama kavaa malunyalunya utaona anatoa ushirikiano! Wote wana tatizo moja michongo mingi ya mabosi wao wanaiona sasa wanapoambulia patupu hasiri huwa ni kwa kila mtu!
 
unaacha barua, kama ina ushindani kwake usahau hiyo barua kufika kwa bosi
wanamjua bosi kuliko ndugu wa bosi wanavyomjua bosi wake
hataki kuona mwanamke mwenzake kaja akiwa amependeza kumzidi (kwa wanawake)
wambea na wanoko kupita maelezo
huwa anajiona mke mkubwa kwa bosi na anaweza amua lolote bosi akitoka
 
Back
Top Bottom