Mimi kupitia roho mbaya ya Yule mama nilipewa zawadi ya shamba heka moja ndani ya Mkoa mmoja wapo wa kanda ya ziwa.
Yule mama ni mtumishi mwenzangu, Kilichotokea nilikuwa napita kwenye korido la ofisi nikakutana na Bibi age imeenda ana documents zote zinazohitajika mkononi.
Mimi: Mama Shikamoo!!
Mama: Marhaba mwanangu, naomba unisaidie.
Mimi: Nini Shida mama.
Mama: Mwanangu nimekuja kumdhamini mtoto wangu ana kesi apa, nimeambiwa nimuone mama Fulani ndo atanisaidia Ila amenisimamisha hapa masaa mawili, Nisaidie mwanangu nimekuja na Mzee yupo nje nae miguu inamsumbua Sana.
Mimi: Naomba nione Documents mama (Ananipa nasoma soma zote zimekamilika)
Mama naomba nifate.
Namfata muhusika mama Fulani (Mtumishi mwenzangu) Namuhoji huyu mama mbona ameambiwa akuone ww ndo utaweza kumsaidia amekaa Hapo kwenye korido zaidi ya masaaa mawili naomba umsaidie basi. (Yupo busy anachezea simu uku ananijibu uyo Bibi msumbufu nilimwambia alete pamoja barua za utambulisho kutoka serikali za mitaa ziligongwa muhuri kwenye passport size na nakala ya kitambulisho cha NIDA)
Mimi: Mbona kila kitu kipo sawa barua za mwenyekiti zipo, nakala ya kitambulisho cha NIDA kipo na Documents nyingine za muhimu hizi hapa. Naomba msaidie ana mgonjwa uko nje anamsubiri na wametoka kijiji cha mbali.
Mama Flani( Mtumishi Mwenzangu): Sawa, Ila muda umeisha waambie waje kesho
Mimi: ( Naangalia saa Bado Dk 30 muda wa KAZI uishe.) Nachukua maamuzi ya haraka naingia ofisini Kwa Boss wangu moja kwa moja nikiwa na Documents za Yule Bibi namuelezea Kwa upana anaelewa. Anazipitia Documents anaridhia, zinagongwa muhuri na saini. Kibali cha dhamana kinatoka. Naambiwa mwambie Bibi Angie ndani.
Naenda kumuita anasikilizwa Mimi nipo pembeni. Boss anatoa order ya dhamana Kwa mtuhumiwa.
Haraka Sana ndani ya Dk 20 kijana anaachiwa Kwa dhamana. Bibi anamchukua kijana wake wanaondoka baada ya kuagana.
Narudi ofisini kwangu ili nijiandae kutoka sababu muda wa kazi umeisha. Mara nasikia mlango wa ofisi unagongwa namwambia apite kumbe ni Yule kijana wa Yule mama aliyeachiwa Kwa dhamana.
Kijana: Kaka samahani Mzee na mama wamenituma nije nikuombe namba ya simu na wanashukuru Sana Kwa msaada uliowapa.
(Nampatia kijana namba. Tunaagana wanaondoka.)
Zinapita wiki mbili naenda likizo. Baada ya likizo ya Mwezi mzima narudi Job.
Siku hiyo nipo nyumbani napigiwa simu namba ngeni. Nauliza Nani mwenzangu!!
Najibiwa Mimi Mama Fulani ulitusaidia siku zile kesi ya kijana wetu. Hata hivyo kesi iliisha salama na kijana alishaachiwa. Tulikutafuta tukaambiwa upo likizo. Vipi umesharudi Baba angu?
Mimi: Asante mama, nilisharudi kazini.
Mama Fulani: Baba, Mzee anaomba jumamosi upatapo nafasi uje kijiji Fulani ukifika ulizia Kwa boda boda wakulete Kwa Mzee Fulani, Usiniangushe Baba angu Mzee atafurahi mno kukuona.
Mimi: Sawa mama nitajitahidi kufika. (Tunaagana)
Siku ya tukio napanda gari kutoka mjini Hadi uko kijijini (mwendo wa saa NNE) nafika naulizia Kwa Mzee Fulani ni wapi? Boda ananipeleka.
Nafika, baada ya salamu na maongezi mafupi. Chakula kinaletwa Lahaula!! nimechinjiwa jogoo na wali Safi. ( Nakula nashiba)
Nawashukuru pale, Mzee anajadiliana na mkewe mara kijana anatumwa akamuite mtendaji wa kijiji, na mjumbe WA nyumba kumi sijakaa Sawa na majilani wameitwa.
Naambiwa Kuna kikao pale nisiwe na hofu, natambulishwa naambiwa wao Kama familia wameamua kunikatia sehemu ya shamba lao heka moja Kwa ajili ya shukrani na utu wangu kwao.
Mkataba unaandikwa pale , naoneshwa majirani zangu tuliopakana mipaka ya shamba, mashahidi wanasaini. Nakabidhiwa nalala zangu nao wanabaki na zao. Tunaagana naondoka kurudi Nyumbani.
Ukweli ni kwamba: Taasisi nyingi za serikali kupata huduma bila kusumbuliwa au kuhangaishwa ni ndoto. Wengi hupata huduma nzuri kutegemea kujuana na mtu Flani au laah iwe Tu imetokea mtoa huduma ana moyo wa kipekee.
Kitu kibaya zaidi usiombee uhudumiwe na hawa mama zetu au dada zetu, ni zaidi ya mateso. Dharau, kujishaua, Mateso, Kiburi yaani sijui hata kwann inakuwaga hivyo.
Customer Care Kwa Bongo Bado Sana.
Ni Mungu Tu.