Wewe umefanya utafiti kuhusu mikataba ya DP World, sawa. Lakini, DP World inaingizwa nchini na Bunge la JMT kupitia mgongo wa nchi yao ya Dubai, kwa makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii (IGA) kati ya nchi yao Dubai na Tanzania.
Makubaliano hayo, yaliyotiwa saini na Waziri, kwa niaba ya Serikali, na kubarikiwa na Bunge, sasa rasmi ni Mkataba wa Ushirikiano, ukiwa hauna muda wa ukomo wala nafasi ya Tanzania kujitoa, labda, labda kuurekebisha.
Mkataba huo (IGA) unaitambua DP World kama kampuni pekee itakayotekeleza miradi yote ya bandari zote na maeneo ya uwekezaji Tanzania Bara kwa muda ambao ushirikiano huo utadumu (Ibara ya 5 ya IGA). Hii ina maana gharama za miradi hiyo, pasipo ushindani dhidi ya DP World, zitabebwa na Tanzania Bara.
Yawezekana, mashauri dhidi ya DP World duniani kote, ndio yamepelekea kuingia Tanzania kwa mgongo wa nchi yao, Dubai. Nasema hivyo kwani tayari kulikuwa na maelewano (MoU) kati yao (DP World) na TPA, Shirika letu la Bandari, uliotiwa sahihi tarehe 22/2/2022. IGA imetiwa sahihi tarehe 3/10/22, ndani ya miezi 12, kama ilivyotakiwa.
Kwa mantiki hiyo, IGA ni mkataba wa kimangumashi na Tanzania tumeingizwa mkengeni.
WAJINGA NDIO WALIWAO