Nilichojifunza jukwaa hili... ni udanganyifu wa members

Nilichojifunza jukwaa hili... ni udanganyifu wa members

kwa kweli umenena, udanganyifu wa watu kujiita wakulima wa kitu fulani wapo, hata mimi niliwahi kutana nao, wanajiita wakulima wa vitunguu, nika-pm kwa msaada wa kupata maeneo huko walipo, nikiwa nimejieleza vya kutosha, unashangaa kimya, ukimpigia anakwambia samahani nimesafiri.
lakini hilo halifanyi jukwaa zima kuonekana la udanganyifu. wapo waaminifu kabisa na wengine binafsi nimefanya nao kazi na hata kupata ushauri wa kitaalam.
 
Wahenga wanasemaa JF kila mtu mjuaji, JF kila mtu mambo safi,, kumbe kuna makapuku huku yanakaa kwa shemeji zao, yanatumia simu na pc za dada zao kujitapa na kutoa ushuhuda feki,
 
Kufanya majadiliano ya kibiashara humu ndani...ni sawa na kutembea kariakoo huku ukiwa umefunika uso na kitambaa.....
 
sina hamu kabisa nilituma hela kwa mtu ya kuleta kuku wa kienyeji mpaka leo afadhali angeniletea hata manyai aniambie kachukue sehemu fulani nusu ya pesa niliompa weee...

kingine nikaingia chaka nikaletewa kuku toka mkoani uwi nikampa chanjo yote siku ya tisa wamelala wote
Bwana ametoa bwana ametwaa

Jina la bwana lihimidiwe
 
Kuna dada mmoja huko whatsapp...kazoazoa watu humu yaani ni anajua kila kitu, samaki yey uyoga yeye, pilipili yeye, mbuzi yeye ila kuja kuchunguza kumbe ni chenga tupu!!
 
Sifa moja ya ujasiriamali ni udadisi wa kina, sasa kama udadisi unafanyia humu tena PM mkiwa wawili hiyo ni dalili ya kuwa mishe za ujasi zitakushinda!!!
 
Mjuaji na muongo kama Pascal hakuna, kwa hili mimi nampa nambari ONE.
 
Kweli kabisa, utapeli pekee uliotokea ni wa Kitomari2 na toka hapo hatujasikia mtu kalalamika. Kama mmetapeliwa semeni na nani ili watu wajue. Pia majadiliano yanakuwa wazi hapa ili watu wakusaidie, kama mauziano mmeshauriwa mkono kwa mkono kama mtu humwamini. Tunaomba msiharibu sifa za jukwaa kuna wadau watu wamenunua bidhaa kwao ni waaminifu mf Malila, Chasha, Poultry Sayuni, Second Lieutenant na wengineo. Ukisikia member sio uamini wote tunajuana na hata ndugu wanaibiana jithibitishie mwenyewe ndio ulipe. Hayo whatsapp nayo ni hapa jukwaani? Mngemalizana uko uko.
Sifa moja ya ujasiriamali ni udadisi wa kina, sasa kama udadisi unafanyia humu tena PM mkiwa wawili hiyo ni dalili ya kuwa mishe za ujasi zitakushinda!!!
 
Kweli kabisa, utapeli pekee uliotokea ni wa Kitomari2 na toka hapo hatujasikia mtu kalalamika. Kama mmetapeliwa semeni na nani ili watu wajue. Pia majadiliano yanakuwa wazi hapa ili watu wakusaidie, kama mauziano mmeshauriwa mkono kwa mkono kama mtu humwamini. Tunaomba msiharibu sifa za jukwaa kuna wadau watu wamenunua bidhaa kwao ni waaminifu mf Malila, Chasha, Poultry Sayuni, Singo, Second Lieutenant na wengineo. Ukisikia member sio uamini wote tunajuana na hata ndugu wanaibiana jithibitishie mwenyewe ndio ulipe. Hayo whatsapp nayo ni hapa jukwaani? Mngemalizana uko uko.
Sifa moja ya ujasiriamali ni udadisi wa kina, sasa kama udadisi unafanyia humu tena PM mkiwa wawili hiyo ni dalili ya kuwa mishe za ujasi zitakushinda!!!
 
Mkuu heri ya xmass na mwaka mpya,
Ktk zama hizi, majanga hayakosekani, mojawapo ya majanga hayo ni kupungua kwa ukweli na kuongezeka kwa tabia ya kutaka vya haraka. Binafsi nimekutana na uhuni mara moja toka kwa wadau fulani,tulikutana hapa jf,walisema wana kitu fulani, ilhali hawakuwa nacho. Kwa upande wangu siwezi kushuhudia mabaya,na zaidi sana nimefaidika zaidi na jukwaa hili tangu nilipojiunga. Inauma sana kuona chombo chetu kinaharibika kienyeji hivi.

Kukosa kazi kwa vijana wengi, kumezalisha kundi la ma-middle men kwenye kila sector duniani,sio Tz pekee. Hili nalo ni somo kwa wajasiriamali wanaomaanisha.
 
Kweli kabisa, utapeli pekee uliotokea ni wa Kitomari2 na toka hapo hatujasikia mtu kalalamika. Kama mmetapeliwa semeni na nani ili watu wajue. Pia majadiliano yanakuwa wazi hapa ili watu wakusaidie, kama mauziano mmeshauriwa mkono kwa mkono kama mtu humwamini. Tunaomba msiharibu sifa za jukwaa kuna wadau watu wamenunua bidhaa kwao ni waaminifu mf Malila, Chasha, Poultry Sayuni, Singo, Second Lieutenant na wengineo. Ukisikia member sio uamini wote tunajuana na hata ndugu wanaibiana jithibitishie mwenyewe ndio ulipe. Hayo whatsapp nayo ni hapa jukwaani? Mngemalizana uko uko.

Ni Sawa Kabisa. Kuna haja ya kufanya majadikiano kwa kina kabla ya kupeanda tenda za msingi.

Mimi nimefaidika sana na hili jukwaa na bado linaendelea kunijenga.
 
Back
Top Bottom