SoC02 Nilichojifunza kuhusu U-Simba na U-Yanga ndani ya ligi yetu

SoC02 Nilichojifunza kuhusu U-Simba na U-Yanga ndani ya ligi yetu

Stories of Change - 2022 Competition

Crosby

Member
Joined
Aug 25, 2022
Posts
5
Reaction score
3
Yanga (Young Africans Sport Club), ni klabu moja wapo ya mpira wa Tanzania iliyoanzishwa 1935 ambapo makao makuu yakiwa Jangwani Kariakoo, Dar es Salaam. Ikiongonzwa na Rais Engineer Hersi Ally Said .Wakiwa mabingwa wa kihistoria mara ishirini na nane 28.

Simba (Simba Sports Club), ni klabu moja wapo mpira wa Tanzania iliyoanzishwa 1936 ambayo makao makuu yakiwa Msimbazi “B” Kariakoo, Dar Es Salaam. Imeundwa baada ya Yanga kuvunjika.Simba kwa sasa ikiwa chini ya mtendaji mkuu mwanadada mpiga kazi Barbara Gonzalez. Wakiwa na Ubigwa wa Ligi Kuu mara 22 wakiwa nyuma ya yanga mara 6.

Simba na Yanga zimetengeneza derby iitwayo kariakoo derby, ni ani moja wapo ya derby bora na yenye mvuto mkubwa sio tu Afrika Mashariki hata Afrika kwa ujumla. Hizi ni timu zenye uhasama mkubwa sana na zenye mashabiki wengi sana hapa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Sasa hii derby ya kariakoo, ndo sasa ikatengeneza uSimba na uYaga. Yaani watu wanamapenzi kweli kweli au kindakindaki na timu hizi za kariakoo yaani uwaambii kitu kuhusu Simba Au Yanga. Em tuziangalie faida na hasara za uSimba na uYanga kama ifuatavyo;

FAIDA ZA USIMBA NA UYANGA KATIKA LIGI YETU YA TANZANIA “LIGI KUU”;
  • Hukuza Ligi Yetu, kwani simba na yanga zimejenga mashabiki wengi, sasa hichi kitendo kinafanya watu wengi wafatilie mpira wa Tanzania lakini sio watanzania tu hadi watu wa mataifa ya nje wanafatilia hizi timu zetu. Hichi kitendo kinafanya ligi yetu kuaangaliwa Zaidi.
  • Kufanya usajili wa kibabe; ushindani wa ligi umeongezeka kutokana na Usimba na Uyanga. Kwa msimu huu wa 2022/2023 tumeona usajili umefanyika wa gharama kubwa sana na waaina yake jinsi wachezaji wanavyotambulishwa mfano hii imeonekana kwa Azizi Ki, ulikua ni usajili mkubwa kufanyika Tanzania uliotumia gharama kubwa na aina yake ya utambulisho wa saa sita usiku na dakika moja. Hivo hivo usajili kwa mzungu Dejan na Nassoro Kapama hapo msimbazi.
  • Umefanya kuvutia wachezaji wa kigeni kuja kwenye ligi yetu, hii imeonekana moja kwa moja kwa mchezaji Cesar Manzoki mchezaji wa Vipers SC ya Uganda kuwa na ndoto ya kuja kucheza na Simba Mnyama ( hii imeonekana kwenye klipu ya video akiwa akiongea). Hii yote imetokana na ushindani wa kariakoo derby, sasa hii hukuza ligi yetu.
  • Simba kuwatia machungu Yanga kuweza kufanya vzuri klabu bingwa, unajua simba na yanga ni kama mapacha, huyu akifanya vzuri na mwingine itampa hamasa na yeye kuweza kufanya vzuri. Hii imetokea pale Simba Sports Club mnyama mkali kufika hatua ya robo fainali klabu bingwa Afrika. Sasa hii imekua kama motisha na yanga nayo iweze kufanya vzuri huko klabu bingwa Afrika.
  • Kuongeza ladha ya mpira nje ya uwanja au nje ya dakika tisini, hapa tunazungumzia mjadala wa mpira baada ya mpira kumalizika. Kwani mpira nje ya uwanja ndo huwa mkubwa sana kwa jinsi wanavyotupiana vijembe. Mfano hii imeonekana kwa usajiri huu wa 2022/2023 kwa yule mzungu Dejan kwa ule msemo “LETE MZUNGU” na pia ule utamu wa kutetema kwa Fiston Kalala Mayele. Sasa hivi vitendo vinaongeza sana ladha ya ligi yetu pendwa LIGI KUU.
  • Kuongeza mapato ya ligi yetu; kwani kuwa na utajiri wa mashabiki wengi maana yake mapato makubwa kwani watu wengi ni rasiliamali tosha. Mapato watayapata kwa njia ya tiketi za uwanjani na mauzo ya jezi sasa hichi kitu kinaongeza mapato ya ligi kuu.
  • Kuongezeka kwa mauzo ya jezi, sasa mashabiki wa kariakoo derby kulingana na tambo zao zinafanya mauzo ya jezi kuwa makubwa sana. Pia hii imeonekana kwa Simba Sports Club msimu wa 2022/2023 kuuza jezi zao zote “SOLD OUT” ndani ya masaa machache.Huu upinzani kariakoo derby unafanya mtu kuwa na mapenzi kindaki ndaki na simba au yanga.
HASARA ZA USIMBA NA UYANGA KATIKA LIGI YETU;

  • Kuzisahau timu zingine, kulingana na vyombo vya Habari vingi kuongela simba ya yanga tu hii inapelekea kuzisahau tumi zingine zinzo shiriki ligi kuu.Unakuta masaa yote wanazungumza simba na yanga , sio tu vyombo vya Habari ya wachambuzi wa mitandao ya kijamii wanazungumzia simba na yanga tu. Hichi kitendo cha usimba na uyanga kinadhoofisha ligi yetu.
  • Uchambuzi wa kimchongo kwa waandishi, hii utokea pale mchambuzi ni mwanasimba hata kama yanga ifanye vzuri aje lazima ataipinga tu kwa kasoro kadhaa wala usishangae asiipongeze.Sasa hichi kitendo kinadhoofisha ligi kuu yetu.
  • Kutokupewa kipaumbele wachezaji wa ndani, hii imeanza kuonekana huu msimu mpya unakuta FIRST ELEVEN ya yanga au simba wamejaa wachezaji wa kigeni. Kwani hawa watani wajadi wenyewe wametokea kuamini wachezaji wa nje ndo wazuri wataleta upinzani kushinda wazawa. Hichi kitendo kinadhoofisha timu yetu ya taifa stars kwani itakua dhaifu.
  • Utani uliopitiliza, hivi karibuni kupitia huu upinzani wa simba na yanga unakuta mashabiki wanatukanana kabisa matusi makubwa, kupigana na kuchaniana jezi. Sasa hichi kitendo akileti picha nzuri katika ligi yetu, kwani inabidi ilete upinzani wa kujenga kuliko kubomoa.
Hitimisho
Kwa kumalizia kusema mbali kwa kujitokeza kwa hizi changamoto za uSimba na uYanga, mimi ndo zimenifanya nianze kufatilia ligi yetu pendwa. Sema kweli Utani huu wa jadi wa kariakoo derby ni mtamu sana zaidi ya bia tamu. Kwasasa ni heli niache kula nikaangalia endapo timu moja wapo ikiwa inacheza.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom