Nilichojifunza kuhusu ziara ya rais Magufuli gerezani Butimba

Jamani nimesoma vyote kwenye hii tread,nasema hivi kwa utawala huu wa Magufuli taasi zote lazima zishike Adabu na nidhamu,wakiendelea kupewa jambajamba za hapa na pale Kama Jana Raisi akiwaita wahusika direct kujibu hoja za Wafungwa oh oh nimeipenda Sana.
Nyinyi wenyewe mmeona sio wapelelezi au magereza wamechanganyikiwa kwenye kujibu hoja,nasema hivi wale wawili sijajua Kama Jana walilala usingizi mzuri na iwe funzo kwa wengine.

Mwisho:Kuna baadhi ya Wafungwa wamefanya makosa mabaya hapa DUNIANI kiasi wameacha familia za watu kwenye majonzi makubwa.
 
Yote yako OPEN ila namba 5 mkuu tunaoyajua acha tukae kimya mzee Hali nibaya Sana Kama umemsikiliza vizuri Yule Staff sergent akitoa malalamiko ya Askari ndio aliongea kila kitu...
Ndio maana hao jamaa wqnakua na hasira sana. Inasemekana askari magereza wanakua makatili mno kwa wafungwa, wanasikolojia wanahusisha hali hiyo na mazingira magumu wanayoishi na kufanya kazi

Ni vyema Amirijeshi Mkuu aliangalie hili kwa jicho la kipekee na angalau aanze kurekebisha hali
 
Yaani hao wapelelezi ni washenzi sana..... wao kakesi kadogo tu kakutaka maelezo madogo tu .. tayari rushwa anataka .... wapuuzi sana wale
 
Kila mfungwa aliyeongea amesema amehukumiwa miaka 30 jela......huko Mwanza uhalifu wao siyo wa kitoto

Kuna yule kiwete aliyehukumiwa kwa ubakaji.....Rais akamuuliza sasa wewe hii miguu miwili haifanyi kazi ila huo wa tatu ndio unaleta mabalaa?!!!
Mguu watatu simchezo.
 
KUMBUKA PIA TUMESIKIA UPANDE MMOJA TU. NA BAHATI MBAYA POLISI HAWANA JUKWAA LA KUJIBU HOJA.
Usiwatetee police wanajulikana sana ndio maana wakistaafu wanakufa mapema kwa madhambi walionayo
 
Itakuwa ameenda kuandaa mazingira ya kumuweka mstaafu mmoja jela
 
Wewe constable acha ujinga wa kuandika kwa herufi kubwa
 
Kuna mmoja file lake limepotea tangu 1979 hadi leo linatafutwa ili kesi iendelee, hapo hukumu bado.
 
Amna askari wanao ishi maisha ya kimaskini kama aksari magereza.. Nyumba zao zime choka sana pale butimba
 
Sio zote.....nenda pale ukachukue mfungwa wa kifungo cha maisha umuue ndio utajua...maiti yenyewe ina haki sembuse mfungwa
Uandishi wako mbovu sana, japo umeandika mambo ya msingi. Tanzania hii mfungwa anapoteza haki zote za kibinadamu.
 
Yote yako OPEN ila namba 5 mkuu tunaoyajua acha tukae kimya mzee Hali nibaya Sana Kama umemsikiliza vizuri Yule Staff sergent akitoa malalamiko ya Askari ndio aliongea kila kitu...


Huyo askari kwa mtazamo wangu Yuko very smart.

Ninaamin atafuatiliwa na kuelewa madaraka/ uongozi/ nafasi ili akatende yale aliyoyasema ambayo kimsingi ni mazuri.

Akipata support anaonekana ni madini.

Hivi askari magereza huwa hawapewi uDC/ uRC na mavyeo mengine kama askari police na askari jeshi?
 
Ukiondoa wafungwa wa kisiasa...wafungwa wengine wote waliobaki ni masikini


Pamoja na hayo watz tuache mahuruma huruma ya ******* na kuamin watu haraka.

Kila aliyeongea Jana anasema na kuonekana kama kaonewa. Na sisi tumeamin na kusonekana nao vilivyo bila kujiuliza.


Nigependa kujua ukweli kuhusu kesi ya kila mmoja aliyesema kabambikiwa ( ie upande mwingine wa story).


Waandishi tusaidieni kuzichimba na kutuhabarisha.
 
MTOA MADA NIKUULIZE SWALI KUHUSU KIPENGELE CHA PILI: KWA NINI POLISI WANABAMBIKIZA KESI?? KAMA N KWELI. NI KWA FAIDA GANI NA KWA NINI??
Njia ambayo ingekuwa bora ni kwa polisi akidhibitika amebanbika kesi basi ile adhabu imgeukie yeye maana lengo lake ilikuwa taabu kwa mwingine.
Tukifanya hivyo hakuna ataruhusu moyo wake kumsingizia mabaya mwingine
 
Njia ambayo ingekuwa bora ni kwa polisi akidhibitika amebanbika kesi basi ile adhabu imgeukie yeye maana lengo lake ilikuwa taabu kwa mwingine.
Tukifanya hivyo hakuna ataruhusu moyo wake kumsingizia mabaya mwingine
unaonaje rais akitoa msamaha kwa wafungwa wote,maana ni kama wamebambikiwa kesi wakati wote hawana hatia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…