Nilichokikuta kwenye simu ya mpenzi wangu nimebaki njia panda, niendelee naye au nimuache?

Nilichokikuta kwenye simu ya mpenzi wangu nimebaki njia panda, niendelee naye au nimuache?

Idrisa1510

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2018
Posts
254
Reaction score
351
Kama heading hapo juu inavojieleza, nina mpenzi wangu na nimwaka watatu sasa tangu tulipoanzisha mahusiano.

Yeye anasoma chuo cha Kati Mbeya diploma ya ualimu mwaka wa pili na Mimi Niko hapa UDOM mwaka wapili bachelor of science with Education.

Walikua na rikizo ya mwezi hivi mmoja ambayo iliitumia Kwa kwenda kwao kama slivonieleza Mimi.

Kufuatia kwamba ni siku nyingi tulikua hatujaonana, nilimuomba atakapotoka kwao Tanga kurejea chuoni Mbeya baada ya kua rikizo imeisha apite Dodoma walau tuonane.

Jumamosi hii ilopita ndio alikua anarejea chuoni akawa amepita hapa Dodoma na tuka spend siku tatu pamoja mpaka jumatatu.

Lakin wakati tukiwa pamoja, nili download hacking app ya spycheckup Nika install na kukamilisha settings zote Kwa ajili ya kuanza kpekua texts zake za kwenye SMS, WhatsApp na call history zake.

Wakati Niko nae hakukua na dalili mbaya kwenye simu yake kiasi kwamba nikamuona ni innocent.
Lakin baada ya Tu kuachana na yeye kuelekea chuoni kwao ndio niaanza kushuhudia madudu.

Huyu msichana kumbe kabla ya kuja kwangu alikua Kwa njemba moja huko morogoro na alikaa yapata wiki nzima Kwa jamaa Hilo.

Hili nimelijua baada ya kubaki nampekua kupitia ile hacking app niloitega kwenye simu yake.

Yani nilikua nasoma chatting zake za WhatsApp na SMS, jamaa linamsifia kwamba anaweza kazi na linasema wiki moja alokaa nalo ilikua ndogo Kwa jinc alivokipa mambo adimu.

Kinachoniuma ni jinsi mavompenda huyu binti na tuliko toka ukijumlisha na malengo tulowekeana. Pia nime spend some amounts of money katika kipind chote za mahusiano kwa kujua ndio mke mtarajiwa kitu ambacho kinaniuma Sana mpaka sasa.

Sijamwambia chochote mpaka sasa maana inashauriwa kutofanya maaumuzi wakati WA hasira, but nazid kuumia kila naposoma chatting zake hiku maana ukiachana na Hilo njema la morogoro kuna jamaa mwingne nazani niwa hapohapo chuoni kwao ananilia tunda langu.

Guyz, actually nimekosa cha kuamua. Either nimpige chini nisonge mbele au nimkosoe Kwa anayoyafanya then niendelee nae coz ningali nampenda Sana.

In addition,. Nataka after three weeks nikapime HIV/AIDs maana nilienda peku Kwa binti huyu nilipokua sijui kama katoka Kwa mshkaji mwingine isije ikawa kaniachia na matadhi.
 
Mkuu kwanza sio lazima wew uanze kumwambia, sababu ukimwambia inaweza kuwa ndo tiketi yake kukuacha.....cha kufanya kama kweli unampenda na unamalengo nae, jitahidi iongezewe uoendo, jitahidi umjari zaidi ya sasa, jitahidi umheshimu, jitahidi uwe perfect gentleman kwake, badilika kuwa positive jitahidi hata kuwa unamwambia malengo yako kwake na malengo ya biashara na career yako unavyotaka iwe...... pia jitahidi usali Mungu atafanya kitu..... After all ulifanya haya yeye mwenyewe kama ni mtu wa kujielewa basi atabadilika ila uoneshe you are the top gentleman kimawazo kaka.....unaweza kumuacha pia lakini kama unampenda kwa kiasi kikubwa utateseka tu utakaposhindwa kumsahau.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwanza sio lazima wew uanze kumwambia, sababu ukimwambia inaweza kuwa ndo tiketi yake kukuacha.....cha kufanya kama kweli unampenda na unamalengo nae, jitahidi iongezewe uoendo, jitahidi umjari zaidi ya sasa, jitahidi umheshimu, jitahidi uwe perfect gentleman kwake, badilika kuwa positive jitahidi hata kuwa unamwambia malengo yako kwake na malengo ya biashara na career yako unavyotaka iwe...... pia jitahidi usali Mungu atafanya kitu..... After all ulifanya haya yeye mwenyewe kama ni mtu wa kujielewa basi atabadilika ila uoneshe you are the top gentleman kimawazo kaka.....unaweza kumuacha pia lakini kama unampenda kwa kiasi kikubwa utateseka tu utakaposhindwa kumsahau.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Nitajaribu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanamke akiamua kutoa uchi yake hakuna wa kuzuia ,kikubwa we endelea kuonesha upendo kama wote (ata kwa kufake) ...anza mchakato wa kutafuta backup mambo ikikaa sawa usubiri kutoa hukumu nzitoo

Ila pia ungesamehe tuu maana na wewe si unapita na k z vibinti vya watu chuoni (win win situation)
 
Kwa huu uandishi wako, nachelea kusema wewe ni kilaza wa kutupwa, Kiswahili lugha yako ya taifa unashindwa kuimudu halafu unajiita mwanachuo?

Inaumiza sana kuona Taifa linalotambulika kama chimbuko la lugha ya kiswahili wasomi wake hawajui hata uandishi sahihi wa maneno na sentensi zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
It's better Ku skip post kuliko kutolea mapovu yasio na maana kwangu. Ndio nina uandishi mbovu, now what? Njoo usome wewe badala yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika mistake wengi wetu tunayofanya katika mahusiano tuliyonayo ni kumchunguza tulie naye

Binafsi sijawahi kuwa mtu wa kumfatilia niliye naye kwasababu najua moyo wangu ulivyo na ukweli mchungu wa kujitakia sitoweza kuu-handle

Mi naamini mwanamke anayekupenda kwa dhati hawezi kukusaliti..hadi inatokea mwanamke anaenda kulala week nzima kwa jamaa mwingine ni ishara kubwa sana kwamba sio sahihi kwako

Fanya maamuzi
 
Back
Top Bottom