Mkuu umenigusa penyewe wala sina la kuongezea.
Kuhusiana na mada hii mwandishi kanivuta pale aliponipa hadithi ya Mama muuza ndizi na kitu kimoja tu kimeniacha hoi...
Katika imani yangu ya Watu na Mazingira, mkuu wangu alipokula ndizi nne alimuuliza yule mama kama anajua amekula ndizi ngapi yeye akifikiria kwamba mama hakuona kumbe huko kwetu mashambani wakulima huhesabu maganda ya ndizi baada ya wewe kula hawana haja wala sababu ya kulinda au kukutazama unafanya nini..
Hali hiii ipo hata katika maamuzi mengi ya kimaisha. Watu wa vijijini sii wajinga kama JK anavyofikiria. wao wamemwachia akifanya anayofanya wanasubiri tu kuhesabu maganda. Na siku ya kura CCM na JK watashangaa kupewa gharama ya madudu waliyoyafanya kwa sababu walifikiria wananchi wa vijijini hawaoni...
Naomba MUNGU amwezeshe na na Dr. Benson Bana wa REDET asome maelezo yako makini ili ajue hisia halisi za mtanzania wa leo hii.
Nimeisoma hii makala kuhusu utulivu, kwa utulivu wa asilimia 100
Hongera sana, Maggid .... read that 'piece' so you build your capacity...
mwandishi amejithidi kuwasilisha ujumbe wake kwa ustadi mkubwa.
tatizo bado ni lile lile je chadema wamejenga msingi kwa wananchi toka kwenye roots? rejea post ya maggid.
Kuna mambo ya msingi sana ambayo wapinzani wanapaswa kuyafanya zaidi ya kusema ccm mafisadi wamefanya hivi na vile.
Hivi wapinzani wanajua kweli nguvu ya ccm ipo wapi?
Ndugu yangu,
Ahsante sana,
Makala hiyo imeandikwa na rafiki yangu Godfrey Dilunga ( Raia Mwema)
Pamoja na kuwa ni kazi nzuri, lakini mimi nimekiona pia ambacho labda wengi wenu hamjakiona.
Maana, mtu mzima unaweza hata kujifunza kwa mtoto wa miaka sita. Unachotakiwa ni kuwa na utayari wa kujifunza. Kuna siku mtoto wangu wa miaka sita alinifundisha hili; " Niliandaa uji wa ulezi wa asubuhi . Akawa wa kwanza kuamka kabla ya wenzake. Nikamwambia; " Nenda mezani, chai tayari!".
Akaenda, baada ya sekunde chache akaniita; " Baba njoo!"
Nikaenda, akaniangalia usoni na kuniambia; " Baba hii sio chai, huu ni uji!"
Nikakiri mapungufu. Na mapungufu yale kwangu ni ya kimalezi, wengi tunayo. Tukiwa kuruta JKT enzi zile nakumbuka na usomi wetu wa form six, pale kambini Itende JKT, baada ya mchakamchaka wa alfajiri na usafi tuliambiwa na Afande Paul; " Kuruta nendeni mkanywe chai!".
Wote tuliokuwa pale Kambini Itende, wengine tumo nao humu JF ni mashahidi, kuwa pale Itende tulikunywa maji ya moto yaliyochemshwa pamoja na vumbi la kahawa na sukari. Haikuwa chai. Lakini ni nani kati yetu alithubutu kumwambia afande Paul; " Hii sio chai, ni kahawa, ingawa si kahawa hasa!"
Tatizo hilo la kimalezi linatusumbua wengi wetu mpaka hii leo. Unaona kwa macho kuwa bwana mkubwa anakupa chungwa, halafu anakwambia; "pokea embe hili!" Wewe unakubali!
Mtoto wangu wa miaka sita anatupeleka kwenye kutafakari alichoandika ; Godfrey Dilunga; " Nimeona waschotaka kukiona" ( Raia Mwema)
Dilunga anaandika;
"Nguvu ya utulivu na usikivu ya mkusanyiko wa watu zaidi ya 40,000 niliyoshuhudia Ifakara ndiyo iliyojitokeza Lupiro-Mahenge, Njombe, Songea na Iringa."
Anaendelea kuandika; "Kama leo mkusanyiko wa walalahoi zaidi ya 40,000 katika kila mkutano wanakua watulivu, ipo siku utulivu na usikivu ule utafanyiwa kazi na walalahoi hao hao. Siku hiyo itafika kama watawala watazidi kujenga wananchi wa mfano wa mama muuza ndizi." ( Dilunga, Raia Mwema)
Sasa hapa sijamwona aliyehoji na kudadisi uhakika wa anachokiandika Dilunga. Hivi ni kweli pale Ifakara Dilunga aliwaona watu 40, 000? Ifakara sikuwapo, lakini pale Mwembetogwa Iringa nilikuwapo. Watu waliofika pale hawakuzidi 5000. Ukubwa wa uwanja wa Mwembetogwa na maeneo ya jirani hauwezi ukajaa watu zaidi ya 5000 na wakaweza kumsikia anayezungumza achilia mbali kumwona kwa sura.
Ndio tatizo letu, tunapenda kusikia tunavyotaka kusikia, na kuona tunavyotaka kuona. Shilingi ina pande mbili, tuwe na ujasiri wa kuangalia upande wa pili wa shilingi. Ujasiri wa kuangalia tusivyotaka kuangalia, kusikiliza tusivyotaka kusikia. Sina cha kuhofia katika kuandika fikra zangu, maana ni fikra zangu. Fikra huru. Na najua kuwa mimi si malaika, nina mapungufu yangu. Ndio maana tukaitwa wanadamu. Najifunza kila siku, hata ninapokutana na mchoma mahindi pale Kitonga. Kijana aliyeishia darasa la saba, naamini nina nitakachojifunza kutoka kwake. Na kwa mwanadamu, katika yote unayayotakiwa kuyakubali. Usisahau kuukubali ushamba. Nimezaliwa mjini na kukulia mjini, tena Ilala, Dar. Lakini siku zote natanguliza ‘ushamba ' wangu. Ndivyo nilivyo.
......................... Nguvu ya utulivu na usikivu ya mkusanyiko wa watu zaidi ya 40,000 niliyoshuhudia Ifakara ndiyo iliyojitokeza Lupiro-Mahenge, Njombe, Songea na Iringa.
Kwa heshima zote, nawasilisha ujumbe kwa watawala kwamba; utulivu na usikivu ule wa hoja ni shinikizo kwenu kubadilika; kinyume chake siku zetu zitaanza kuhesabika. ..............................................
Kasheshe,
..call me crazy, but I have been dreaming of the day when our President would come frm a party that does not have a majority in the parliament.
..mwanzo nilikuwa naomba CCM wa-lose majority of the seats, lakini inavyoelekea ni rahisi zaidi, in the near future, kwa vyama vya upinzani kupata Raisi, kuliko majority ya bunge la muungano.
..naamini mfumo wetu wa utawala na bunge utafanya kazi vizuri zaidi ikiwa Raisi atatoka kwenye chama kisicho na majority bungeni, au tukiwa na situation ambapo the majority is very slim in the parliament.
..uchaguzi huu kura yangu ya Uraisi ni kwa Dr.Wilbroad Slaa.
A+; A+; A+; Katika maudhui yote matatu nakupa A+ mimi ni mwalimu tena wahesabu unastahili A+. Nawaomba wana JF tuanzishe promotions ya members wanaocontribute serious articles kama hizi. Kwa kuanzia napendekeza mubezi atambuliwe na level ya seniority. Be blessed for nourishing our hungry minds.
Unajua kuna vyakula vingine huwa tunakula kwa mazoea tu; halafu mtu anakupikia chakula ambacho ulifikiri unakijua na kinapugusa ulimi wako unajikuta mate yanakupalia; unapomaliza unaona aibu kuuliza "kuna kingine?". Nimependa makala!!! Kama ni kachumbari basi hii ni ile original..
Mkuu tatizo watu wanadhani kuandika upande wa pili wa shilingi wa chadema na slaa ni uhaini, watu wanataka kusikia yale tu wanayotaka kuyasikia wao, ni mabungufu makubwa ya fikra