Elections 2010 Nilichokiona kwenye mikutano ya Dr. Slaa

Elections 2010 Nilichokiona kwenye mikutano ya Dr. Slaa

mwandishi amejithidi kuwasilisha ujumbe wake kwa ustadi mkubwa.
tatizo bado ni lile lile je chadema wamejenga msingi kwa wananchi toka kwenye roots? rejea post ya maggid.
Kuna mambo ya msingi sana ambayo wapinzani wanapaswa kuyafanya zaidi ya kusema ccm mafisadi wamefanya hivi na vile.
Hivi wapinzani wanajua kweli nguvu ya ccm ipo wapi?
 
mubezi kama wewe sio muandishi, basi una kipaji, use your talent please. nimekupa thanx hapo juu.
 
Mkuu umenigusa penyewe wala sina la kuongezea.

Kuhusiana na mada hii mwandishi kanivuta pale aliponipa hadithi ya Mama muuza ndizi na kitu kimoja tu kimeniacha hoi...
Katika imani yangu ya Watu na Mazingira, mkuu wangu alipokula ndizi nne alimuuliza yule mama kama anajua amekula ndizi ngapi yeye akifikiria kwamba mama hakuona kumbe huko kwetu mashambani wakulima huhesabu maganda ya ndizi baada ya wewe kula hawana haja wala sababu ya kulinda au kukutazama unafanya nini..

Hali hiii ipo hata katika maamuzi mengi ya kimaisha. Watu wa vijijini sii wajinga kama JK anavyofikiria. wao wamemwachia akifanya anayofanya wanasubiri tu kuhesabu maganda. Na siku ya kura CCM na JK watashangaa kupewa gharama ya madudu waliyoyafanya kwa sababu walifikiria wananchi wa vijijini hawaoni...

umeongeza jambo, limekaa ki'concept zaidi. thanx. Mungu awabariki kwa vipaji mlivyopewa. tuzidi kumuomba pia atubadilishie utawala na atupatie uongozi. TUMECHOKA NA UTAWALA TUNATAKA UONGOZI.
 
Naomba MUNGU amwezeshe na na Dr. Benson Bana wa REDET asome maelezo yako makini ili ajue hisia halisi za mtanzania wa leo hii.

Mimi kwanza sina hata muda wa kuisoma hiyo report ya REDET coz wanaoiendesha hiyo timu ni wanamtandao na ni maswahiba wakubwa wa yule bwana mkwele.
Kaka sitaki kukuvimbisha kichwa ili tembo ukaitia maji but kwa mwendo huu tunahitaji sana waandishi makini kama nyie, yaani nimekuwa nikisoma huu ujumbe mpaka nywele zanisisimka na machozi kunilenga pia sikuwa napenda kabisa ufike mwisho, kazana kaka songa mbele twahitaji waandishi kama nyie ili kuikomboa nchi.
 
A+; A+; A+; Katika maudhui yote matatu nakupa A+ mimi ni mwalimu tena wahesabu unastahili A+. Nawaomba wana JF tuanzishe promotions ya members wanaocontribute serious articles kama hizi. Kwa kuanzia napendekeza mubezi atambuliwe na level ya seniority. Be blessed for nourishing our hungry minds.
 
nachangia tena....eeh mada nzuri lakini mmhh we kaka kulikoni??hata kama hukuwa na nia ya ndizi ila kula ndizi tano mmhh...nadhani ulikuwa na njaa sana!!!na huenda ilikuwa intention yako kupunguzza njaa huku ukicheki hali ya utulivu mkutanoni
 
Nimeisoma hii makala kuhusu utulivu, kwa utulivu wa asilimia 100

Hongera sana, Maggid .... read that 'piece' so you build your capacity...

Ndugu yangu,

Ahsante sana,

Makala hiyo imeandikwa na rafiki yangu Godfrey Dilunga ( Raia Mwema)

Pamoja na kuwa ni kazi nzuri, lakini mimi nimekiona pia ambacho labda wengi wenu hamjakiona.

Maana, mtu mzima unaweza hata kujifunza kwa mtoto wa miaka sita. Unachotakiwa ni kuwa na utayari wa kujifunza. Kuna siku mtoto wangu wa miaka sita alinifundisha hili; “ Niliandaa uji wa ulezi wa asubuhi . Akawa wa kwanza kuamka kabla ya wenzake. Nikamwambia; “ Nenda mezani, chai tayari!”.
Akaenda, baada ya sekunde chache akaniita; “ Baba njoo!”
Nikaenda, akaniangalia usoni na kuniambia; “ Baba hii sio chai, huu ni uji!”
Nikakiri mapungufu. Na mapungufu yale kwangu ni ya kimalezi, wengi tunayo. Tukiwa kuruta JKT enzi zile nakumbuka na usomi wetu wa form six, pale kambini Itende JKT, baada ya mchakamchaka wa alfajiri na usafi tuliambiwa na Afande Paul; “ Kuruta nendeni mkanywe chai!”.
Wote tuliokuwa pale Kambini Itende, wengine tumo nao humu JF ni mashahidi, kuwa pale Itende tulikunywa maji ya moto yaliyochemshwa pamoja na vumbi la kahawa na sukari. Haikuwa chai. Lakini ni nani kati yetu alithubutu kumwambia afande Paul; “ Hii sio chai, ni kahawa, ingawa si kahawa hasa!”
Tatizo hilo la kimalezi linatusumbua wengi wetu mpaka hii leo. Unaona kwa macho kuwa bwana mkubwa anakupa chungwa, halafu anakwambia; "pokea embe hili!" Wewe unakubali!

Mtoto wangu wa miaka sita anatupeleka kwenye kutafakari alichoandika ; Godfrey Dilunga; “ Nimeona waschotaka kukiona” ( Raia Mwema)
Dilunga anaandika;

“Nguvu ya utulivu na usikivu ya mkusanyiko wa watu zaidi ya 40,000 niliyoshuhudia Ifakara ndiyo iliyojitokeza Lupiro-Mahenge, Njombe, Songea na Iringa.”

Anaendelea kuandika; “Kama leo mkusanyiko wa walalahoi zaidi ya 40,000 katika kila mkutano wanakua watulivu, ipo siku utulivu na usikivu ule utafanyiwa kazi na walalahoi hao hao. Siku hiyo itafika kama watawala watazidi kujenga wananchi wa mfano wa mama muuza ndizi.” ( Dilunga, Raia Mwema)

Sasa hapa sijamwona aliyehoji na kudadisi uhakika wa anachokiandika Dilunga. Hivi ni kweli pale Ifakara Dilunga aliwaona watu 40, 000? Ifakara sikuwapo, lakini pale Mwembetogwa Iringa nilikuwapo. Watu waliofika pale hawakuzidi 5000. Ukubwa wa uwanja wa Mwembetogwa na maeneo ya jirani hauwezi ukajaa watu zaidi ya 5000 na wakaweza kumsikia anayezungumza achilia mbali kumwona kwa sura.
Ndio tatizo letu, tunapenda kusikia tunavyotaka kusikia, na kuona tunavyotaka kuona. Shilingi ina pande mbili, tuwe na ujasiri wa kuangalia upande wa pili wa shilingi. Ujasiri wa kuangalia tusivyotaka kuangalia, kusikiliza tusivyotaka kusikia. Sina cha kuhofia katika kuandika fikra zangu, maana ni fikra zangu. Fikra huru. Na najua kuwa mimi si malaika, nina mapungufu yangu. Ndio maana tukaitwa wanadamu. Najifunza kila siku, hata ninapokutana na mchoma mahindi pale Kitonga. Kijana aliyeishia darasa la saba, naamini nina nitakachojifunza kutoka kwake. Na kwa mwanadamu, katika yote unayayotakiwa kuyakubali. Usisahau kuukubali ushamba. Nimezaliwa mjini na kukulia mjini, tena Ilala, Dar. Lakini siku zote natanguliza ‘ushamba ‘ wangu. Ndivyo nilivyo.
 
mwandishi amejithidi kuwasilisha ujumbe wake kwa ustadi mkubwa.
tatizo bado ni lile lile je chadema wamejenga msingi kwa wananchi toka kwenye roots? rejea post ya maggid.
Kuna mambo ya msingi sana ambayo wapinzani wanapaswa kuyafanya zaidi ya kusema ccm mafisadi wamefanya hivi na vile.
Hivi wapinzani wanajua kweli nguvu ya ccm ipo wapi?

Una hoja ya msingi sana. Hicho ndicho ninachokiona mimi. Hata leo nikiwa pale kijijini Doma, niliwakuta akina mama wanane wanauza nyanya. Niliwauliza kuhusu uchaguzi. Mama mmoja akanijibu; "Hapa ni Amos na Kikwete" Ni Amos Makala. Kisha akasema; " Tumesikia amekuja mgombea Rais mpya, lakini tumeona picha yake tu, hatujamwona wala mtu wa kutwambia habari zake". Haya ni mambo ya msingi ya kuyafanyia kazi.
 
Ndugu yangu,

Ahsante sana,

Makala hiyo imeandikwa na rafiki yangu Godfrey Dilunga ( Raia Mwema)

Pamoja na kuwa ni kazi nzuri, lakini mimi nimekiona pia ambacho labda wengi wenu hamjakiona.

Maana, mtu mzima unaweza hata kujifunza kwa mtoto wa miaka sita. Unachotakiwa ni kuwa na utayari wa kujifunza. Kuna siku mtoto wangu wa miaka sita alinifundisha hili; " Niliandaa uji wa ulezi wa asubuhi . Akawa wa kwanza kuamka kabla ya wenzake. Nikamwambia; " Nenda mezani, chai tayari!".
Akaenda, baada ya sekunde chache akaniita; " Baba njoo!"
Nikaenda, akaniangalia usoni na kuniambia; " Baba hii sio chai, huu ni uji!"
Nikakiri mapungufu. Na mapungufu yale kwangu ni ya kimalezi, wengi tunayo. Tukiwa kuruta JKT enzi zile nakumbuka na usomi wetu wa form six, pale kambini Itende JKT, baada ya mchakamchaka wa alfajiri na usafi tuliambiwa na Afande Paul; " Kuruta nendeni mkanywe chai!".
Wote tuliokuwa pale Kambini Itende, wengine tumo nao humu JF ni mashahidi, kuwa pale Itende tulikunywa maji ya moto yaliyochemshwa pamoja na vumbi la kahawa na sukari. Haikuwa chai. Lakini ni nani kati yetu alithubutu kumwambia afande Paul; " Hii sio chai, ni kahawa, ingawa si kahawa hasa!"
Tatizo hilo la kimalezi linatusumbua wengi wetu mpaka hii leo. Unaona kwa macho kuwa bwana mkubwa anakupa chungwa, halafu anakwambia; "pokea embe hili!" Wewe unakubali!

Mtoto wangu wa miaka sita anatupeleka kwenye kutafakari alichoandika ; Godfrey Dilunga; " Nimeona waschotaka kukiona" ( Raia Mwema)
Dilunga anaandika;

"Nguvu ya utulivu na usikivu ya mkusanyiko wa watu zaidi ya 40,000 niliyoshuhudia Ifakara ndiyo iliyojitokeza Lupiro-Mahenge, Njombe, Songea na Iringa."

Anaendelea kuandika; "Kama leo mkusanyiko wa walalahoi zaidi ya 40,000 katika kila mkutano wanakua watulivu, ipo siku utulivu na usikivu ule utafanyiwa kazi na walalahoi hao hao. Siku hiyo itafika kama watawala watazidi kujenga wananchi wa mfano wa mama muuza ndizi." ( Dilunga, Raia Mwema)

Sasa hapa sijamwona aliyehoji na kudadisi uhakika wa anachokiandika Dilunga. Hivi ni kweli pale Ifakara Dilunga aliwaona watu 40, 000? Ifakara sikuwapo, lakini pale Mwembetogwa Iringa nilikuwapo. Watu waliofika pale hawakuzidi 5000. Ukubwa wa uwanja wa Mwembetogwa na maeneo ya jirani hauwezi ukajaa watu zaidi ya 5000 na wakaweza kumsikia anayezungumza achilia mbali kumwona kwa sura.
Ndio tatizo letu, tunapenda kusikia tunavyotaka kusikia, na kuona tunavyotaka kuona. Shilingi ina pande mbili, tuwe na ujasiri wa kuangalia upande wa pili wa shilingi. Ujasiri wa kuangalia tusivyotaka kuangalia, kusikiliza tusivyotaka kusikia. Sina cha kuhofia katika kuandika fikra zangu, maana ni fikra zangu. Fikra huru. Na najua kuwa mimi si malaika, nina mapungufu yangu. Ndio maana tukaitwa wanadamu. Najifunza kila siku, hata ninapokutana na mchoma mahindi pale Kitonga. Kijana aliyeishia darasa la saba, naamini nina nitakachojifunza kutoka kwake. Na kwa mwanadamu, katika yote unayayotakiwa kuyakubali. Usisahau kuukubali ushamba. Nimezaliwa mjini na kukulia mjini, tena Ilala, Dar. Lakini siku zote natanguliza ‘ushamba ' wangu. Ndivyo nilivyo.

ndugu zangu hawa wana mapenzi ya mtu pofu asieona upande wowote zaidi ya kipendacho. hawana uwezo wa kureason and analyzing facts in diffrent dimension na si kuwa wamekosa tools bali upofu

asante sana na hata ww ukismama kwenye mawazo yako utakuwa mtu mzuri na mwandishi mzuri wa articles zako

hawa ndio watu ambao ati tuwape dola, watu wanaonyweshwa uongo bila ya kuutafakari na kuupima

jana kulitoke habari mbili zenye mazingira sawa

moja kuna mwenzetu hapa katuandikia tetesi kuwa sheikh yahya hussein kafa tena tetesi tu, basi michango ya watu hawa huwezi kuamini bila ya kutaka kujua ukweli wa habari yenyewe walishabikia wakafurahi na kujipongeza na kutoa vifungu vya vitabu vitakatifu kuwa anastahiki kufa

nikasema na mm wacha niwapime kwa habari ya pili yenye muundo ule ule isipokuwa sasa baada ya sheikh hussein tumuweke kipenzi chao Dr slaa oh hii ilianzishwa mwisho kule ile na ile ilidumu hakuna aliepiga kelele wala kusema ifutwe, ila hii ilikua moto walijazana na bila ya kuhoji na kutafakari wakawa wakali. hawa ni watu wa aina gani ambao daima hawapimi kama greater thinkers ambao tuliwategemea na badala yake hutamani kusikia wanacho penda kukisikia na wasichopenda hata kiwe ukweli huchukia kukisikia
 
......................... Nguvu ya utulivu na usikivu ya mkusanyiko wa watu zaidi ya 40,000 niliyoshuhudia Ifakara ndiyo iliyojitokeza Lupiro-Mahenge, Njombe, Songea na Iringa.

Kwa heshima zote, nawasilisha ujumbe kwa watawala kwamba; utulivu na usikivu ule wa hoja ni shinikizo kwenu kubadilika; kinyume chake siku zetu zitaanza kuhesabika. ..............................................

pamoja na picha za uandishi kuwa zinavutia.............na kwa kuwa unajua wengi wetu hapa tunapenda nini............umechukua fursa hiyo tukusome kwa makini...........ili tusahau "ndizi" i.e. kura zetu..............well done Dilunga.............

Bandugu mimi bado naona yote hii ni changamoto ya kuongeza nguvu zaidi ya kushawishi wananchi wachague mabadiliko............
 
Asante sana Mubezi kwa uandishi wako murua uliotulia. Una kipaji kikubwa sana cha kuandika, hapa jukwaani naweza nikakulinganisha na Mwanakijiji. Kama hauko katika fani ya uandishi basi si vibaya angalau mara moja moja uwe unaandika katika baadhi ya magazeti yetu na wasomaji wengi watavutiwa sana na style ya uandishi wako. BIG UP Mubezi!
 
majjid umefilisika kiuandishi hadi nakuonea huruma ndugu yangu. naona umekaa mkao wa kusubiri hisani ya CCM upewe hata ukatibu tarafa!! pole sana ndugu yangu. jitahidi labda JK kama ataweza kuchakachuwa kura atakukumbuka na kukupa hata utendaji kata ya KIHESA iringa. maana majjid yule wa enzi zile siyo huyu!! huyu ni majjid alikaa ki HIZA TAMBWE zaidi. pole sna ndiyo maisha, kuishiwa hoja ni ugonjwa mbaya sana.

kwa wewe mtu wa pwani wala sikushangai, si umezaliwa msoga wewe!!
 
Majjid,

Nawe sasa mbona unakwenda kule ambako siko? Hata watu wa5 tu, ujumbe ndo una matter sasa hio ya 40,000 inakuuma nini hata kama nii 80,000?
 
Kasheshe,

..call me crazy, but I have been dreaming of the day when our President would come frm a party that does not have a majority in the parliament.

..mwanzo nilikuwa naomba CCM wa-lose majority of the seats, lakini inavyoelekea ni rahisi zaidi, in the near future, kwa vyama vya upinzani kupata Raisi, kuliko majority ya bunge la muungano.

..naamini mfumo wetu wa utawala na bunge utafanya kazi vizuri zaidi ikiwa Raisi atatoka kwenye chama kisicho na majority bungeni, au tukiwa na situation ambapo the majority is very slim in the parliament.

..uchaguzi huu kura yangu ya Uraisi ni kwa Dr.Wilbroad Slaa.

Suppose Dr. Slaa akikuahidi kuwa atamteua kuwa mbunge na kumchagua Prof. Lipumba kuwa Waziri wake Mkuu bado utakataa kumpigia kura? nakuhimiza umchague DK. Slaa kwa sababu aliisha ahidi kuunda serikali ndogo makini ya kuitoa Tanzania katika hili dimbwi la umaskini!
 
Mubezi,
Hongera sana kwa makala yako makini.Mimi si mwandishi wa habari lakini napenda kazi za waandishi wa aina yako.Naomba kama utaweza uipeleke kwenye magazeti ya kila siku ili isomwe na watu wengi zaidi.
Asante sana.
 
Unajua kuna vyakula vingine huwa tunakula kwa mazoea tu; halafu mtu anakupikia chakula ambacho ulifikiri unakijua na kinapugusa ulimi wako unajikuta mate yanakupalia; unapomaliza unaona aibu kuuliza "kuna kingine?". Nimependa makala!!! Kama ni kachumbari basi hii ni ile original..
 
A+; A+; A+; Katika maudhui yote matatu nakupa A+ mimi ni mwalimu tena wahesabu unastahili A+. Nawaomba wana JF tuanzishe promotions ya members wanaocontribute serious articles kama hizi. Kwa kuanzia napendekeza mubezi atambuliwe na level ya seniority. Be blessed for nourishing our hungry minds.

Hata mimi nampa CREDIT mwandishi wa habari hii. Now what if huyu bwana angekuwa amejenga hoja yake hiyo kumhusu mgombea mwingine say Lipimba wa CUF au JK wa CCM tungempa CREDIT lukuki kama hizo? If NO then we should rethink about our credibility as JF virtual community. Huyu bwana ameeleza suala la mmsingi sana kama jamii yetu ya kitanzania na ndilo linalo reflect TRUE values of a Tanzanian citizen.
 
Unajua kuna vyakula vingine huwa tunakula kwa mazoea tu; halafu mtu anakupikia chakula ambacho ulifikiri unakijua na kinapugusa ulimi wako unajikuta mate yanakupalia; unapomaliza unaona aibu kuuliza "kuna kingine?". Nimependa makala!!! Kama ni kachumbari basi hii ni ile original..

mkuu nakubaliana na wewe asilimia 100, kwamaana ya uandishi basi mwandishi ametumia ubunifu wa hali ya juu kuwasilisha ujumbe wake
upande wapili ni mkuu mubezi, amebeba sifa nyingi sana utadhani makala kaandika yeye wakati imeandikwa na dilunga, na ndio maana mods wanasisitiza kuandika chanzo cha habari kama ume copy na kupest
 
Ndugu yangu,

Ahsante sana,

Makala hiyo imeandikwa na rafiki yangu Godfrey Dilunga ( Raia Mwema)

Pamoja na kuwa ni kazi nzuri, lakini mimi nimekiona pia ambacho labda wengi wenu hamjakiona.

Maana, mtu mzima unaweza hata kujifunza kwa mtoto wa miaka sita. Unachotakiwa ni kuwa na utayari wa kujifunza. Kuna siku mtoto wangu wa miaka sita alinifundisha hili; " Niliandaa uji wa ulezi wa asubuhi . Akawa wa kwanza kuamka kabla ya wenzake. Nikamwambia; " Nenda mezani, chai tayari!".
Akaenda, baada ya sekunde chache akaniita; " Baba njoo!"
Nikaenda, akaniangalia usoni na kuniambia; " Baba hii sio chai, huu ni uji!"
Nikakiri mapungufu. Na mapungufu yale kwangu ni ya kimalezi, wengi tunayo. Tukiwa kuruta JKT enzi zile nakumbuka na usomi wetu wa form six, pale kambini Itende JKT, baada ya mchakamchaka wa alfajiri na usafi tuliambiwa na Afande Paul; " Kuruta nendeni mkanywe chai!".
Wote tuliokuwa pale Kambini Itende, wengine tumo nao humu JF ni mashahidi, kuwa pale Itende tulikunywa maji ya moto yaliyochemshwa pamoja na vumbi la kahawa na sukari. Haikuwa chai. Lakini ni nani kati yetu alithubutu kumwambia afande Paul; " Hii sio chai, ni kahawa, ingawa si kahawa hasa!"
Tatizo hilo la kimalezi linatusumbua wengi wetu mpaka hii leo. Unaona kwa macho kuwa bwana mkubwa anakupa chungwa, halafu anakwambia; "pokea embe hili!" Wewe unakubali!

Mtoto wangu wa miaka sita anatupeleka kwenye kutafakari alichoandika ; Godfrey Dilunga; " Nimeona waschotaka kukiona" ( Raia Mwema)
Dilunga anaandika;

"Nguvu ya utulivu na usikivu ya mkusanyiko wa watu zaidi ya 40,000 niliyoshuhudia Ifakara ndiyo iliyojitokeza Lupiro-Mahenge, Njombe, Songea na Iringa."

Anaendelea kuandika; "Kama leo mkusanyiko wa walalahoi zaidi ya 40,000 katika kila mkutano wanakua watulivu, ipo siku utulivu na usikivu ule utafanyiwa kazi na walalahoi hao hao. Siku hiyo itafika kama watawala watazidi kujenga wananchi wa mfano wa mama muuza ndizi." ( Dilunga, Raia Mwema)

Sasa hapa sijamwona aliyehoji na kudadisi uhakika wa anachokiandika Dilunga. Hivi ni kweli pale Ifakara Dilunga aliwaona watu 40, 000? Ifakara sikuwapo, lakini pale Mwembetogwa Iringa nilikuwapo. Watu waliofika pale hawakuzidi 5000. Ukubwa wa uwanja wa Mwembetogwa na maeneo ya jirani hauwezi ukajaa watu zaidi ya 5000 na wakaweza kumsikia anayezungumza achilia mbali kumwona kwa sura.
Ndio tatizo letu, tunapenda kusikia tunavyotaka kusikia, na kuona tunavyotaka kuona. Shilingi ina pande mbili, tuwe na ujasiri wa kuangalia upande wa pili wa shilingi. Ujasiri wa kuangalia tusivyotaka kuangalia, kusikiliza tusivyotaka kusikia. Sina cha kuhofia katika kuandika fikra zangu, maana ni fikra zangu. Fikra huru. Na najua kuwa mimi si malaika, nina mapungufu yangu. Ndio maana tukaitwa wanadamu. Najifunza kila siku, hata ninapokutana na mchoma mahindi pale Kitonga. Kijana aliyeishia darasa la saba, naamini nina nitakachojifunza kutoka kwake. Na kwa mwanadamu, katika yote unayayotakiwa kuyakubali. Usisahau kuukubali ushamba. Nimezaliwa mjini na kukulia mjini, tena Ilala, Dar. Lakini siku zote natanguliza ‘ushamba ' wangu. Ndivyo nilivyo.
Mkuu tatizo watu wanadhani kuandika upande wa pili wa shilingi wa chadema na slaa ni uhaini, watu wanataka kusikia yale tu wanayotaka kuyasikia wao, ni mabungufu makubwa ya fikra
By the way mkuu upo juu kwa makala zako
 
Kwa hakika hii ni article imetulia. Nafahamu JK anazisoma hizi, naomba aisome hii na kisha ampongeze huyu kijana na la mwisho naye amuunge mkono Slaa, akubali tu kuwa Dr kamzidi, na ni bora zaidi kwa maendeleo ya watanzania including JK himself. Ningekuwa mimi JK ningeandika historia ya kukubali kushindwa kabla ya kura na kumuunga mkono DR. Kwani nafahamu angeleta maendeleo kwa watanzania wote na kwa jinsi tunavyo yahitaji.
 
Back
Top Bottom