Nilichokiona Usiku ule

Gautten Potten

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
1,642
Reaction score
3,426
Hi ni kwa wale wanao amini busara nyeusi zipo. Soma Kama stori ila usipuuze.

Kama una tabia ya kula vinavyosalia kuamkia siku nyingine iwe kwako au kokote kule "ACHA".
Hasa ukiwa huna nguvu ya ziada kaushaga tu.

Nilichokiona usiku kwa siku tofauti ndio kinanisukuma kukuambia haya.

TUKIO NILOSHUHUDIA

Mida ya Saa tisa kasoro kiu iliniamsha nikashindwa kujizuia nitoke niende kunywa maji ndio nawakuta watu wa wanne jikoni.

Mzee Mmoja ( Babu la kwenda ) na visichana vitatu wanakula na kutapikia kwenye Hotpot la chakula ila asubuhi maneda check sikuona kasoro.

Ule msosi nilikuja mpa dogo Mmoja jirani hapa akaukataa katakata na kusema Bro huoni umechezewa huo.

Nimewaza sana kuwa tunakula uchafu kiasi gani.

Nimewaza Sana dogo anaona me sioni,Nilichokiona usiku ilikuwa ni bahati au ?
 
...Hueleweki ! Mmemulewa ?....
 
Baada ya kuwakuta hao watu jikoni ukafanyaje
 
Kabla ya kulala izunguke nyumba yako uifunike kwa damu ya Yesu (kwa imani). Au nenda makanisani ukachukue chupa ya maji ya baraka. Kisha nyunyiza nje na ndani ya nyumba.
 
Kabla ya kulala izunguke nyumba yako uifunike kwa damu ya Yesu (kwa imani). Au nenda makanisani ukachukue chupa ya maji ya baraka. Kisha nyunyiza nje na ndani ya nyumba.
Shida zote hizo za nini!!?? Inatosha kumuamini Mungu aliyekuleta Duniani na kukupa pumzi yake,na yeye ndiyo anajua mwisho wako ni lini hapa Duniani!!
 
Shida zote hizo za nini!!?? Inatosha kumuamini Mungu aliyekuleta Duniani na kukupa pumzi yake,na yeye ndiyo anajua mwisho wako ni lini hapa Duniani!!
Maisha ya hapa duniani ni mapambano mithili ya askari aliye vitani. Zivae silaha zote ili uweze kuzishinda hila na mashambulizi ya upande wa pili.
 
Hata sjasoma nikamaliza ulichoandika boss, ila kwetu sisi Muslims imekuja dalili chakula chochote au kinywaji utakachokianza pasi na bisimillah Basi jua kishea na wakulungwa wale invisible ni jambo la kawaida sana na pia chakula chochote au kinywaji kilichoachwa wazi pasi na kufunikwa Basi tambua wale wakulungwa kupita nacho pia ni kitu possible afu hizo zote ni adabu tu chakula ukizingatia Basi kwisha!
 
Hii story haijakamilika, baada ya kuwaona ikawaje?
 
Usiku umeviona vibabu vinakula na kutapikia chakula halafu asubuhi unampa mtoto wa jirani anakwambia huoni kama chakula kimechezewa unashangaa dogo ameona halafu wewe huoni[emoji3]

Ngoja nipige zangu kiporo changu cha wali na maharage nkimaliza niende nkalijenge taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…