Anonymous77
JF-Expert Member
- May 29, 2022
- 589
- 1,515
Kwanza kabisa nianze Kwa salamu: Asalam alaykum na kwawale wasiopenda salamu hii basi habari za asubuhi ndugu zanguni wana JF.
Kwanza kabisa ningependa kwenda moja kwa moja kwenye pointi husika nayo ni kile nilichokiona usiku wa Leo.
Kwa kawaida yangu na ratiba zangu za kulala siku za hivi karibu zimekuwa kabla ya kulala lazima nichome ubani chumbani na pale ninapotaka kulala ni lazima nishike udhu na Baada ya hapo nasoma surat nas X3 surat faraq X3 surat ikhas X3 na ayatul qurs X3 Kisha huplay Quran na kuiacha ikisomwa kuanzia surat fatiha Kisha Baada ya hapo ndipo hulala zangu nikiongezea na maombi mengine ya kiswahili na udambwi dambwi kama kuomba maisha marefu afya njema na mengine mengine si mnajua life yetu hii "pangu pakavu tia mchuzi" bila maombi haiendi.
Basi bhana leo mida ya saa 10 kama sio Kumi basi 11 au 12 alfajir Giza lilikuwepo si haba kwani sikutoka nje na niliona ni Giza kupitia dilisha ambalo japokuwa lilikuwa na pazia ila I trust my eyes.. bila shaka palikuwa Bado hapajakucha.
Nilichokishuhudia ni kwamba wakati nimelala nimeona viumbe wawili wakiwa na mavazi meupe juu mpaka chini mmoja akiwa karibu na kona ya mlango na wapili akiwa kitandani nilipolala nahisi alikuwa akinikanda kanda mkono wangu wa kushoto yani ubavu wangu wa kushoto kwani nilikuwa nimelalia ubavu mmoja nao ni ule wa kulia na uwa kushoto ukiwa huru na ndio ulikuwa juu nae ndio alikuwa kama kanishika na kufanya kama vile anakanda lakini sielewi kitendo kile dhumuni lake au maana yake nini hasa my point ni hapo alikuwa katika ubavu wa kushoto akidili nao wakati huo huo mwingine akiwa katika Kona ya mlango Yani pembe iliyokaeibu na mlango kwa maana ukifungua mlango inakuwa kama Kona.
Huyu aliekuwa nyuma yangu sikufanikiwa kumuona sura na aliepo mbele yangu aliekuwa kasimama karibu na Kona ya mlango huyu pia sikumuona sura bali niliona tu jinsi alivyosimama sijui kama alikuwa kanipa mgongo au la ila nina walakini alikuwa akinitazama tu Kwa maana hiyo sura ilikuwa mbele ila sikuona zaidi ya vazi lake la rangi nyeupe alilovaa kuanzia chini mpaka juu kama kanzu tu ila Tofauti na yake ni kuwa lake lilifika mpaka kichwani.
Wakati nashuhudia ni kama nilikuwa ndotoni lakini ndoto ambayo ni kama nilikuwa naona kinachoendelea ila Sina la Kufanya zaidi ya kutulia tuli kama mtu aliemwagiwa Maji ya baridi sababu sikuweza kufanya chochote zaidi ya kushuhudia tu kitendo kile kwa sekunde zipatazo 30 hadi 40 Kisha nikashituka kutoka katika hali Ile ya kutoweza kufanya lolote nikiwa kama niko ndotoni.
Enyi wana JF naombeni ushauri na msaada wenu ni nini hiki..