PostGE2025 Nilichokishuhudia kwenye maandamano: Serikali ya Tanzania imeshindwa vita

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Wamekuwa wakionywa kila mara kuwa ujeuri wakenge kutosikia,kutokubali,kutokuelewa wala kutokubali kueleweshwa hadi ubongo wake ashuhudie ukichungulia nje ya fuvu lakichwa chake ndiyo chanza cha kulifikisha taifa hapa tulipo na na matokeo ya siku na baada ya uchafuzi/chaguzi
 

Nikiwaangaliaga wale Wazee wa ccm huwa nasikitika sana!
 
Nilichojifunza kwenye yale maandamano ni Samia amshukuru sana Magu kupeleka ikulu Dodoma vinginevyo muda huu angekuwa Oman. Kwa kifupi siku ya tarehe 29 Dar yote ilikuwa mikononi mwa waandamanaji. Walitamalaki watakavyo na walifanya lolote waliloona linapendeza kwao.

Kosa kubwa la waandamanaji ni ilipofika jioni wakarudi makwao na kuachia ibilisi nafasi ya kujiunda upya! Lilikuwa kosa kubwa sana la kimkakati kwa mpiganaji ambaye ameshaachiwa uwanja na adui.
 
Uchambuzi mz
Uchambuzi bora wa mwezi kabisa huu.
 
By the way, this is one of the very best article ambalo sijalisoma kwa Miaka mingi Sana, sikufaham ila una uwezo mzuri sana wa Hoja, mpangilio na uandishi, hongera sana!
Siyo tuu anauwezo mkubwa bali ndugu yetu huyu ni 'a walking encyclopedia'.

Akianza kushusha nondo za international politics na kuleta nukuu za kihistoria ya lini tukio kama hilo lilitokea wapi na mwaka gani, siyo tuu kukujengea hoja bali unajikuta umepata elimu tosha.
 
Ni jana tuu niliwaza kuhusu Ikulu ya Dodoma kumuokoa. Cha kushangaza, wakati Magu anaamua kujenga Ikulu kama ile ya Dar, Dodoma; Kikwete alibeza kimzaha, akisema, "sisi watu wa pwani tulipenda ibaki Dar"
 
.. kinachofuata hakitapendeza kabisa.
Inasikitisha Sana. Kuna uzi nilikukatalia jambo. Nadhani, I was naive at that particular time.

Kinachonishangaza ni namna gani rouge apparatus ili outsmart the Wazalendo wa kweli wa Taifa ili.

Naomba kinachofuata kisiwe cha kututia majonzi Tena, bali cha kutuleta pamoja sisi Watanzania kwa misingi ya haki. Hata hivyo, haiwezi kupita hivi hivi kama upepo. Haki lazima itendeke kwa uhalisia

Asante kwa uzi huu
 
Nawaza tu,hawa vijana waliowapeleka jkt kisha wakawanyima ajira,tuko nao mitaani..siku akatokea adui akawapatia siraha,sijui kama Tanzania itabaki salama.
Viongozi wawajibike kwa wananchi na sio kwa mafisadi.
 
Uko sahihi kabisa kuhusu watoto wa kuanzia 95 kwenda mbele.

Iko hivi, kisayansi kizazi kimoja hutengenezwa kwa miaka 15 na baada ya hapo huwa kinaanza kuishi misingi ambayo kilijengewa. KGB wanasema ukitaka kuvuruga nchi basi anza na watoto mashuleni. Badilisha mitaala na mbinu za kielimu ambazo kizazi kinakua nayo.

Watanzania wengi ambao walisoma shule ya msingi kuanzia mwaka 1975 na kumaliza 2005 wanaendana sana kifikra na kimawazo. Elimu ilikuwa ni suala la kitaifa na siyo huria kama leo hii. Mitaala yetu ilikuwa imelalia kwenye elimu ya kijamaa (Marxist Leaning Education). Tunanyweshwa hadi sumu kwamba UBEPARI ni mfumo dhalimu wa kiuchumi, tunaimba nyimbo za kumsifu Nyerere na tunahudhuria Chipukizi-CCM.

Vizazi vyetu vilijengewa nidhamu ya woga, lakini tulifundishwa kufikiri kabla ya kutenda. Kizazi chetu sisi watu wana uelewa mkubwa wa siasa za nchi, dunia na historia, ila elimu yetu ilitunyima ujasiri na ililenga kutuzalisha kuwa wafanyakazi maofisini. Hata mtu akiishia darasa la saba alikuwa ana ufahamu mkubwa ya Uraia, Nidhamu, Stadi za Kazi na Maarifa ya Jamii.

Tofauti na wengi tunavyofikiri, Gen-Z siyo kizazi cha kwanza kufanya fujo hapa Tanganyika. Kizazi cha Millennials waliaozaliwa mwaka 1981 hadi 1986, kiliwahi kufanya vurugu kubwa za namna hii, utofauti ni kwamba hazikuwa vurugu za kisiasa. Kama utakumbuka kuanzia mwaka 1994 mashule ya bweni kulikuwa na vurugu sana na wanafunzi walishindikana kabisa. Tambaza, Mkwawa, Tosamaganga, Umbwe, Lyamungo, Lupata, Iyunga nk zilikuwa na watu wakorofi haswaaa.

Wanafunzi walikuwa wanachoma shule, wanaua makondakta na kufanya vurugu nyingine kama kutengeneza mabomu maabara (Hili lilitokea Tosamaganga, Ifunda na Mkwawa) na kukamatwa. Serikali ya Mkapa na vyombo vya usalama katika kuhakikisha hiki kizazi ambacho kinaanza kuonesha kuchukia CCM hasahasa kwenye uchaguzi wa 1995 kwa kuwaunga mkono NCCR-Mageuzi, walikuja na mkakati madhubuti kabisa wa kuvuruga elimu ya nchi.

Shule zikaanza kufungwa na kufutwa, ufaulu wa wanafunzi ukapungua kabisa wasomi wasiwe wengi, mitaala ikabadilishwa kwa kiwango cha ajabu na elimu huria ikapanuliwa jambo lililopelekea kuanguka kabisa kwa elimu nchini. Baada ya 2006 wakaja na utaratibu wa shule za kata ambao ulichangia wanafunzi wengi kukosa waalimu wa kutosha kufundisha baadhi ya masomo kwasababu walimu wazuri wote walienda shule binafsi ambazo vigogo ndiyo walipeleka watoto wao.

TATIZO LINAKUJA HAPA: Kizazi ambacho hujakiandaa kwa miaka 15, huwezi kukitawala kirahisi kwasababu hamuwezi kuwa nacho ukurasa mmoja kimawazo. Millenials walizimwa vizuri na kurudishwa kwenye mstari, serikali ikisaidiwa na wazazi ambao waliamini kabisa elimu ndiyo ufunguo wa maisha na CCM ndiyo chama kitakachowafikisha nchi ya ahadi.

Gen-Z ni tofauati kabisa. Mtoto anaweza akamaliza shule bila kujua kusoma na kuandika vizuri, hafahamu kabisa historia na nchi, hamjui Nyerere wala falsafa zake hivyo hawezi kuheshimu chochote kuhusu serikali au chama. Tofauti na Millennials, Gen-Z hawajanyweshwa ile sumu wa woga ambayo ilitolea kupitia elimu ya kijamaa.

Gen-Z wamezaliwa kipindi ambacho fursa ndogo-ndogo za kiuchumi zinapatikana kiurahisi hivyo na uchumi wa masoko umekomaa. Millennials tulitegemea ajira za maofisini, kwamba soma, faulu, omba kazi ufanukiwe maisha. Gen-Z bila woga hawachagui kabisa kazi. Tena ukizingatia wengi hawafaulu vizuri, basi huanza kutafuta hela pindi wamemaliza kidato cha nne. Bodaboda na Bajaji wengi ni Gen-Z. Wadada wa Soloon wengi ni Gen-Z. Mawinga wengi wa Kariakoo ni Gen-Z. Mafundi simu na Laptops wengi ni Gen-Z.

Kiufupi, Gen-Z kwa idadi yao wao ndiyo waendesha uchumi wa nchi. CCM ilivyovuruga elimu kwa maksudi ili kuendelea kuwatawala watanganyika kiurahisi imelata matokeo yasiyotabirika (The Plan Has Backfired). Kungekuwa hakuna mtandao basi mkakati wa CCM ungefanikiwa ila tatizo ni kwamba Gen-Z wengi wamelelewa na INTERNET, huku wazazi wao wengi wakiwa wametingwa na ugumu wa maisha na nyumbani hawapo.

=====================================================================
Watoto kama hawa ambao hawafikiri mara mbili ukishawakwaza haina kurudi tena. Gen-Z wengi hata wazazi tumewashindwa kabisa. Ukimkoromea anakujibu na kuvimba, hivyo tunaongea nao kwa kuwabembeleza siyo mabavu tu kila siku. Hawa watoto wako hivi siyo kwasababu kuna kitu wanacho la hasha. Gen-Z wa mataifa kama Uchina, Ujerumani na Urusi ambako elimu bado ni suala la kitaifa hawako hivi, wana uzalendo mkubwa mno wa kushangaza.

Ila sehemu ambako elimu ni huria kama Uingereza, Ufaransa, Marekani chamoto wanakipata kutoka kwa Gen-Z. Ndiyo maana mbali na udikteta wa Paul Kagame kutumia jeshi kutawala, ametumia elimu kuwazubaisha wanyarwanda wengi ambao ukiwasikiliza huwa hawaamini kuna dunia nyingine nje ya Rwanda, jambo ambalo siyo kweli.

Gen-Z wengi wana ujasiri mkubwa (Exceptionally Bold) ila They Lack Deep Thinking, Deep Analytical Skills, Common Sense na wanakitu wanasaikolojia tunakiita Diminished Danger/Diminished Responsibility ambapo ubongo unashindwa kuchakata hatari na kuona ni jambo la kawaida tu au kitu cha kawaida.

===============================================================
CCM haina PLAY-BOOK ya kupambana na Gen-Z. Kule Marekani magenge ya kizayuni kama AIPAC yamewashindwa kabisa Gen-Z hasa linapokuja suala la Palestina, mpaka sasa Marekani hafahamu afanyaje, mbali na kutumia teknolojia kuwadhibiti. Hapa Tanzania ambako vyombo vya usalama vilibweteka na kujiamini kupita kiasi, bila kufahamu kwamba mchwa washaanza kuvitafuna kwa ndani kimya-kimya, hawamaliza salama hata 2027.

Matatizo yote haya yalianza 1995 na kama watu wangekuwa makini na kuona mbali, basi Tanzania ingejiepusha na matatizo mengi sana. Lakini ndiyo hivyo washachelewa na meli imeanza kuzama, hapa kila mtu anahangaika kujilinda kivyake. Mle ndani CCM + TISS + TPDF, watageukana na kuchinjana kupita kiasi mambo yakakavyozidi kuwa mabaya kila mtu akitaka kukwepa lawama.

Zanzibari wanaweza kujitoa kwenye MUUNGANO, lakini mapema kabisa tutashuhudia ule Uzanziberi na Uzanzibara kwasababu adui yao wa kumrushia lawama Tanganyika a.k.a Machogo hawatakuwepo. Mwaka 1964, watu wa nje walihusika na mapinduzi lakini ukatili wote dhidi ya waarabu ulisaidiwa kuratibiwa na Wazanzibara. Hata mwaka 2001, watanganyika waliuwa wazanzibari kikatili, wakisaidiwa na Wanzanzibara.

Umeona Sudan ilivyo leo ? Wote ni waislamu lakini kuna Muislamu Muarabu na Muislamu Muafrika. Mwanzoni ilikuwa ni Waislamu dhidi ya Wakristo Weusi. Walipotengana tu, ikafahamika kwamba kumbe kuna utofauti pia baina ya Waislamu weusi na Waislamu Waarabu.

====================================================================
NOBODY is SAFE
​
 
Dodoma kiliwaka tarehe 30th Oktoba 2025, lengo lilikuwa kwenda CHAMWINO ila ilitumika nguvu kubwa ya kutisha kuzuia lisifanyike. Ndiyo maana tuliapishana kwenye kambi za kijeshi. Pia sidhani kama anaweza kurudi Dar Es Salaam tena huyu mama maana hali itakuwa mbaya mno kwake kiusalama, endapo atakanyaga hapa.

Kuhusu kurudi majumbani, ni kwamba kuanzia majira ya saa tisa jioni baada ya mtandao kuzimwa vijana bado walikuwa wanaendelea kukinukisha vibaya mno. Ndipo wanajeshi wakatolewa wengine kambini na mauaji yakaanza, ilhali watanzania wakiamini kwamba jeshi lote liko upande wao. Hapa watanganyika tuligeukwa vibaya mno.

Walipofungia MTANDAO na VITUO VYA MAFUTA waliweza kudhibiti maandamano kwa kiwango kikubwa sana kwa kupunguza kasi. Ukweli ni kwamba watu hawakurudi ndani ila walikuwa wanafuatwa na zile IST, Landcruiser na Noah.
​
 
Malcom za sku nyingi? You were missed bro.

Mie nailaumu ccm iliyotekwa na kigenge
 
Nikiwaangaliaga wale Wazee wa ccm huwa nasikitika sana!
Miaka zaidi michache nyuma niliwahi kuandika hapa kwamba ile Mizee ya Cold-War inaharibu nchi na bila kuifukuza na kuiburuta kibabe nchi hii itaharibika. Nakumbuka watanganyika wengi walinishambulia sana.

Kuna Mzee ni Mshauri wa Samia, alishawahi kuniambia kwenye kikao fulani hivi mimi sina cha kumfundisha. Elimu yangu pamoja na wenzangu ni ya kukariri, Copy and Paste. Nakumbuka nilimwambia kuhusu mgogoro fulani nje ya mipaka ye Tanzania.

Kama kawaida akaanza na historia ya ujamaa na jinsi ambavyo wanasheria wa tanzania tunapenda kuwaigiza wazungu. Niliaondoka kwenye kikao nikisema Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii (Ile ya Kisukuma), kama hawa ndiyo wazee ambao tunawategemea kusaidia nchi basi tumeliwa.
​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…