PostGE2025 Nilichokishuhudia kwenye maandamano: Serikali ya Tanzania imeshindwa vita

PostGE2025 Nilichokishuhudia kwenye maandamano: Serikali ya Tanzania imeshindwa vita

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Kinachoendelea kwasasa nchini Tanzania ni jambo watawala hawakuwahi litegemea kama litakuja kutokea Tanzania, na wanaliogopa mno: KUTENGENEZA MAGENGE YA WANANCHI SUGU.

Watanzania waliletengenezwa na Mzee Nyerere kuwa kama kondoo, yaani Serikali iwapige kofi halafu wanageuza shavu jingine wapigwe kofi jingine. Mtanzania anaweza kuwa amemzidi nguvu za mwilini polisi, lakini hata kama polisi atamshambulia alikuwa haweza kurudisha. Ni mara nadra mno kukuta watanzania wanagombana na mamlaka.

Tokea 2017-2025 watanzania walishuhudia wenzao wengi wakitekwa hadharani bila huruma na hawakuweza kufanya lolote lile. Bahati mbaya watawala walitegemea kwamba wakiwaua kikatili wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi mkuu basi wataweza kunyamaza. Kuna siku Raisi Samia Suluhu akajitapa kabisa kwamba "Waulize Gen-Z kama kuna mtu ana ujasiri wowote wa kufanya vurugu" akiamini kabisa kwamba amewakomesha kabisa watanzania wa bara.

Hili linafanana sana na mapinduzi ya mwaka 1905-1906 nchini Urusi ambayo hayakufanikiwa. Mfalme wa Urusi badala ya kuwasikiliza watu akawa mbabe, na baada ya watu kuogopa ndiyo wakawa majasiri zaidi na makatili. Miaka tisa baadaye yani mwaka 1917 zamu ya Mfalme wa Urusi kuuwawa ikafika. Urusi walikuwa na shirika kubwa la kijasusi (The Okhrana) ambalo lilikuwa na uwezo wa kipekee kabisa lakini lilishindwa kumlinda Mfalme Nicholas Ramanov.

The Okhrana walishawashinda kabisa wana mapinduzi wa Urusi kina Lenin. Tatizo lilianza pale ambapo Urusi ilianza kushambuliwa na maadui kutoka nje kama Ujerumani, Uturuki, Marekani na Japan. Wakati wa vita ya kwanza ya dunia, wanamapinduzi wa Urusi waliamua kuungana na maadui wa Urusi ili kuipindua serikali ya Ramanov. Jambo hili halikuwa jema lakini ukatili wa serikali ya Ramanov uliwapelekea wanamapinduzi kuungana na maadui wa taifa lao, jambo ambalo liliigawa Urusi vipande-vipande.

===============================================================================
TISS + JWTZ + CCM wasipojifunza kwa kinachoendelea, siku siyo nyingi damu itamwagika sana huku bara. Ubaya zamu hii hawataumia raia peke yao, bali na watawala pia. Vitendo vilivyotokea jana na juzi vinafikirisha mno: Mosi, Watanzania wa kawaida kuamua kufukuzia gari ili kuokoa uhai wa mtu na kufanikiwa, tena dhidi ya watu wenye silaha za moto hadi mhanga akatoroka ni jambo ambalo limejenga taswira mbaya ya uasi kwa watanzania.

Pili, kitendo cha afisa mkubwa wa serikali kuwekewa vikwazo na taifa kubwa duniani na watanzania wengi kuoneshwa kufurahishwa ni jambo la kuogopesha. Marekani anawawekea vikwazo watu wengi mno, hata maafisa wa Ujasusi wa Kagame waliwahi kushikiliwa nchini Uingereza, lakini wanyarwanda wengi walikarahishwa na hicho kitendo. Tanzania imekuwa tofauti sana, maana wengi wamefurahi, hata mimi binafsi nimefurahi sana.

===============================================================
Mnawaua watanzania, mnawatesa hadharani, huku mkiwanyanyasa na kufanya maisha yao kuzidi kuwa ya kimasikini, siku wakiamua kuusi na kuungana na maadui wa nje mtalalamika na kusema wamekosa uzalendo ??? Unaweza ukahisi hili haliwezekani, lakini mifano hai imewazunguka:

1. Musseveni aliungana na Tanzania dhidi ya serikali yake ya Uganda.
2. Kagame aliungana na Tanzania na Uganda dhidi ya serikali yake ya Rwanda.
3. Kabila aliungana na Tanzania, Uganda na Rwanda dhidi ya serikali yake ya Zaire.
4. Chiume aliungana na Tanzania dhidi ya serikali yake ya Malawi.

Wahenga husema, MUOSHA HUOSHWA. Siku siyo nyingi hawa watanganyika mnaowapuuza watafanya mambo ya hatari na ajabu halafu wote tutapoteza nchi na kushuhudia mauaji makubwa mno. Ubaya zaidi, Tanzania ikiingia kwenye machafuko makubwa ya kisiasa lazima mataifa mengi ya hapa Afrika, Ulaya, Amerika na Asia yataingia kupora mali huku yakiunga mkono pande zote.

Ninyi maafisa TISS + JWTZ mnaoua na kutesa watanzania, siku inakuja mtaamka tu na kujikuta hamna chenu, serikali imeanguka na mishahara hailipwi, mkaishia kuwa masikini kama walivyokuwa KGB na Red Army baada ya kuanguka USSR. Majumba yenu ya Mbweni, Masaki na Bunju yakawa hayana faida tena kwasababu hamna MDHAMINI.

================================================
ENIWEI, shupazeni shingo lakini siku inakuja.

Tena itakuja kama MWIVI, wakati ule hamtegemei.

Ninyi watawala wa Tanzania hamko tofauti na mataifa mengine hata kidogo.

Ni suala la muda tu, sisi tuko hapa tunakunywa KAHAWA, na panapo majaliwa tutakuja kuwakumbusha.
​
Kikwete hana akili, mabavu aliyotumia kumpitisha Samia pale Dodoma 2025, angetumia kumpitisha Emmanuel Nchimbi yaliyotokea 29 Oct 2025 yangetokea?
 
Asante mkuu, sichoki kukusoma kila mara nakusearch kupata update yoyote mpya.
Mungu akulinde sana.
Usisumbuke kumtafuta (search) ameandika nini.
Fungua profile yake bofya 'Follow'.
Kila akiandika utapata taarifa.
 
Back
Top Bottom