PostGE2025 Nilichokishuhudia kwenye maandamano: Serikali ya Tanzania imeshindwa vita

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections


Malcolm Mimi naipenda sana Tanzania, ila uongozi huu umekuwa ukihatarisha sana usalama wa Taifa hata kupelekea watu kuwaza na kupanga mambo mazito sana sana.

Moja wapo ni kuanza kupanga mkakati wa kulipua gati muhimu bandarini.

Tusipokuwa waangalifu Nchi inaenda kuwa failed a failed state completely
 
Ila bongo nyoso tunaishi kwa neema ya Mungu tu. Machafuko ya siku tatu tu tayari njaa mtaani imeshatamalaki, je yangeendelea wiki mbili tu vita ingeisha maana hadi makachero wangekufa njaa
 
Hili mbona ni dogo sana ndugu yangu.

Kuna silaha zimepita mpaka fulani hivi zimefika Dar Es Salaam nyingi mnoo.

Kiukweli mpaka kufika 2027 dunia nzima haitaamini kwamba hawa ni watanganyika.
​
 
"Kila nikifiria siku za mbeleni moyo wangu hugubikwa na majonzi na woga mkubwa. Siku hizi nashindwa hadi kulala vizuri, nalala saa kumi usiku nakuwa kwenye mawazo mengi sana. The Tanzania we grew up in, is gone and it will never come back."
😭😭😭😭😭😭😭😭😭
 
Duh Mzee Mwanakijiji njoo ndugu yangu
 
Father una akili sana. Naomba kama una binti kijana wangu aje aoe kwako tafadhali
 
Kwa sababu vyombo vya ulinzi vilitegemea silaha na kuua, ikitokea siku wananchi wakiandamana tena ni dhahiri watakuwa makini na hatari zaidi...

Haya ni mambo ambayo yanaweza kutokea endapo kutatokea tena maandamano basi:

1. Lock down itakuwa ndefu zaidi.

2. Wananchi watafunga barabara ili kuzuia movements za askari na wajeda.

3. Tutarajie uharibifu mkubwa zaidi wa mali za umma maana wananvhi wangali na hasira.

4. Tutarajie vifo zaidi vya askari kwa sababu hivi sasa askari wamejiwekea label kuwa wao ni maadui na "wauaji" - Hili ndio linaoloogofya sana maana ni chimbuko la vita na mapinduzi.
 
Hili mbona ni dogo sana ndugu yangu.

Kuna silaha zimepita mpaka fulani hivi zimefika Dar Es Salaam nyingi mnoo.

Kiukweli mpaka kufika 2027 dunia nzima haitaamini kwamba hawa ni watanganyika.
​
Vyombo vya ulinzi vilikuwa wapi?
 
Kila mahala kwenye mjadala unahusiana na hali iliyopo na kilichotokea 29 October 2025 haya ndio nayoyasema

1. Ni kwamba jeshi letu na vyombo vyetu vimejiweka uchiiiii wa mnyama ikitokea hata kama imepigwa mechi ya kirafiki tu ya wiki moja na ka Rwanda tutapasuliwa mchana kweupe Vikosi vya adui vitakua vinapiga chai Dar na Dodoma sio tu kwasababu ya uchache wa silaha na na hayo ma logistics yani watakaochangia ushindi wa adui ni wabongo wenyewe watawataja walipo watataja kila kilochofichwa kwasababu ya chuki ambayo ipo

2. Tofauti na ile ya Iddi Amini ambapo Raia wali support nchi yao hii ya sasa raia wata support adui, Jw walipewa vyakula na kila kitu kutoka kwa wananchi safari hii watapokea usaliti ambao hawajawahi kukutana nao.

3. Vyombo si vinalala nakusema raia wakigeni wanaingia kuleta vurugu basi dua ziishie kwa hao hao raia pasitokee GenZ wakapokea raia na silaha wallah familia za askari na vyombo vingine na CCM watakiona cha mtema kuni.
 
Hili mbona ni dogo sana ndugu yangu.

Kuna silaha zimepita mpaka fulani hivi zimefika Dar Es Salaam nyingi mnoo.

Kiukweli mpaka kufika 2027 dunia nzima haitaamini kwamba hawa ni watanganyika.
​
Mkuu Malcom,

Unazungumziaje uhusika wa Abdul kwenye huu uharibifu unaondelea Tanganyika? Japo naelewa kuwa kwa mujibu wa historia ,Tanganyika imeanza kupoteza mwelekeo miaka ya 95 kadili ya maandiko yako.

Lakini pia umezungumzia silaha.

Upo sahihi 100% ila nakuhakikishia kuwa 2027 ni mbali sana. Sisiem wameharakisha haraka sana mchakato wa vijana kumiliki silaha na magenge ya uasi kwa kasi ya 5G kwa hiki kilichotokea juzi.
 
Kitu pekee nachoweza kusema mda hauko upande wao watawala mabadiliko ya nakuja na Uoga ndani yake na watu wanaogopa mabadiliko ni wale walioshiba Mafisadi , wezi wanyonyaji. Ndo waoga wa mabadiliko. Maskini hawezi kuogopa mabadiliko Maneno ya Jk Nyerere. Hao wote uliowataja walikua na uwezo wa kuweza kulinda walichonacho mapema sana kuliko kupelekea kupoteza hata kidogo ambacho wangeweza kuklinda. Sijui uoga ulitoka wapi wa kushindwa kutoa Tume huru hapo nyuma wangeweza kujinasua kwenye shimo kubwa ambalo wanaenda kundumbukia. Kuishi kwa mazoea na bila kujali nyakati na Kukosa uwajibikaji ndo kunaenda kuangamiza hili taifa Mwigulu juzi anasema ye ametokeo kwenye familia maskini sasa unajiuliza ungekua umetokea familia maskini ungekubali Ubunge na Uwaziri mkuu ambao unatokana na umwagaji damu wa watoto maskini Kisa tu kudai haki zao ambalo sio kosa kisheria? Maandamano ni kosa gani kisheria katiba imeruhusu maandamano hata kama ni kosa kisheria adhabu yake ni kupigwa risasi? Mmeua ndoto za watoto wangapi Mungu atusandie
 
Mleta maada unatisha sana

Nakumbuka siku moja ulipinga katiba ya majimbo nchini, ukisema hatuwezi kufanya jambo kwa kuwaiga marekani maana ni nchi mbili tofaut na watu wake ni tofaut

Na ulisema si kila jambo ambalo limefanyika nchi flan likafanikiwa basi usitegemee ukilipeleka nchi nyingine likafanyikiwa

Lakini pia ushawahi kusema kwamba marekani wana rais sababu wana bunge imara sisi huo mfumo tuliiga bila kutizama mbele
 
Nakushukuru sana Kaka Malcom kwa maelezo yako mazuri umenijibu swali langu nililokuuliza kwenye Thread ile.

Hata hivyo naamini andiko lako linatoa mwanga kwa vyombo vya usalama na makachero wenzako ili waone namna ya kufanya ili Tanzania Yetu itamalaki tena

BIla hatua madhubuti hakuna aliyesalama, niliona ile oktoba wote tulijificha kwenye mahandaki hakukuwa na kada wa chadema wala wa ccm, katibu mkuu wala mbunge. Sote tulipigika kwa mda mfupi tukijawa na hofu. Ndio nikajua thamani ya amani ktk Taifa.
 
Ndio vijana aliosema Nyerere. Kule Ulaya maendeleo yalianza miaka ya 1700s baada ya vijana kama hawa. Sisi tumechelewa wamezaliwa 1990
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…