Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,705
- 30,041
Binafsi hapo awali sikuwa interested sana kufuatilia interview ya Milardi Ayo na Jesca Magufuli,lakini jana katika kupitia hapa na pale,nikasema ebu ngoja nichek hii interview
Kiukweli sikujutia kabisa kuangalia yale mahojiano,tena sana sana nilijilaumu kwanini hapo awali sikufuatilia mahojiano hayo
Kuna mambo mengi ambayo Jesca alizungumza na ambayo yametuwezesha kujua Jembe alikuwa ni mtu wa kariba ipi
Kwa ujumla wake Mwamba alikuwa mtu makini sana na mwenye kujua anachofanya
Kuna nukta chache ambazo nilizipenda,kunifurahisha na kunichukiza au kama sio kunikera pia
Twende pamoja.....
Nilipenda sana msimamo wa Magufuli kuwaambia wanawe kwamba Uraisi ni wake yeye na sio wao,kwa maana waishi na watu vizuri,waheshimu kila mtu mkubwa au mdogo,mwenye hadhi na asiye na hadhi
Jesca akaeleza kwamba,alipoanza kazi aliiambiwa amuheshima mdogo na mkubwa,hata kama huyo mkubwa atakuwa mfanya usafi hapo ofisini kwao
Hakika hayo ni maneno ya dhahabu kwa baba yoyote yule kwa mwanae,kumuelimisha mwanae umuhimu wa kuwaheshimu watu wote ambao anao kutana nao,kila mzazi anatakiwa afanye hivyo
Hapa nakumbuka ile miaka ambayo mwanamziki mmoja wa bongo fleva ndio alikuwa katika chat sana,naye si mwingine bali ni TID wakati anazindua album yake ya kwanza kabisa pale Diamond Jubilee nilikuwepo,nyimbo kama Zeze zilihit sana
Basi bwana mhenga huyu nikakutana nae kwenye kona za ukumbi ule,nikiwa kama mshabiki wake,nikamsalimia kwa bashasha lakini alichonijibu nilichoka! Akaniambia kwani unanijua mimi?
Dah ikabidi niwe mpole,hayo ndio matokeo ya kutofunzwa kuwaheshimu watu unao wajua na usio wajua
Kilichonifurahisha kama sio kunichekesha ni namna alivyokuwa anawatoa watoto wake out, nyie si mmezoeshwa kutolewa out kwenda beach au mbuga za wanyama au zoo
Wao walikuwa wanaambiwa wanatoka out,maskini wanajikwatua na viwalo safi lakini mwisho wa siku wanajikuta outing yao inaishia kwenye kukagua madaraja na barabara hahah
Kumbuka hapo wanafanyiwa surprize,Jesca anasema tumekagua sana madaraja na barabara na mzee wetu
Hizo ndio zilikuwa out zao na jiwe,mara chache chache sana walienda viwanja vya burudani na mbuga za wanyama,hakika yeye alikuwa mtu wa hapa kazi tu!
Na mwisho kilichonikera ni kwamba,unaambiwa jiwe anapenda sana magari ya benz,lakini ilikuwa radhi magari hayo yaoze lakini hakuna wa kuyagusa isipokuwa yeye tu
Anyway marehemu hatakiwi kusemwa sana
Hizo ndio nukta chache zilizo nifanya nichukue kalamu na kuandika haya
Ni hayo tu!