ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Habarini wapiga kura wenzangu.
Jana nilipata fursa ya kuhudhuria mkutano wa Kampeni wa mgombea wa CHADEMA ndugu Tundu Lissu, kiukweli watu walijitokeza wengi sana kumlaki na walionesha ushirikiano kwa kumsindikiza kwa maandamano hadi hotelini kwake hiyo ni mida ya saa mbili usiku, polisi walijaribu kuwazuia bila mafanikio.
Wakati anaanza kujinadi alianza vizuri kwa utangulizi lakini kadiri mda ulivyoenda sikuona akinadi na kuwakumbusha sera yake kuu ya bima ya afya kwa wote na kui-connect na hali za maisha ya watu halikadharika jinsi hiyo sera ya bima ya afya ilivyomsaidia hata yeye kupona huko Ulaya, maana kiukweli ukiwatazama watu wengi walikuwa na nyuso za huruma na machozi kwamba hawaamini huyu bwana alipona kutokana na shambulio lake.
Sera ya bima ya afya, uhuru na maendeleo ya watu anatakiwa atembee nazo kila anapokwenda na ainadi tena kwa kutumia mfano wake mwenyewe maana inahusu hadi kuboresha sekta ya afya na Lishe moja kwa moja. Lakini pia niliwahi msikia kwamba ataitumia gesi na madini mengine kuwa dhamana ya kupata pesa za kugharamia bima ya afya kwa wote. Ilitakiwa aifafanue kwa utaratibu huu.
Alizungumzia hoja ya kuweka ukanda huru wa biashara hasa kwa mikoa hii ya mpakani lakini, hii hoja hakuweza kuifafanua kwa lugha nyepesi ili watu wa kawaida waelewe,mathalani wanavyoweza kunufaika na biashara huria ya mipakani,angetolea mfano wa Tunduma ambako kilo moja ya sukari kutoka Zambia na Malawi ni sh.2000 wakati hiyi hiyo sukari hairuhusiwi kuuzwa huku Sumbwanga,kwa nini pale iuzwe na hapa ikatazwe wakati mkoa huu pia unashea mipaka na Zambia?
Watu wangeelewa hoja ya ukanda huru wa biashara kwa mfano huo mwepesi ilhali sukari ya Tzn ni sh. 3000-3200/= kwa mkoa huu, nk nk. Lakini pia alitakiwa atumie fursa hii kuinadi sera yake ya kuondoa utitiri wa kodi na kuwa na makisio makubwa ya kodi ili kuwapa fursa wananchi kujiajiri na kufurahia kulipa kodi .
Tatu kwa Mikoa hii ya Nyanda za Juu Kusini kuanzia Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe na Rukwa shughuli kuu ni kilimo na biashara za kuvuka mipaka lakini hakuweka ufafanuzi wa namna atakavyowainua wakulima ambapo kwa ukanda huu ilifaa azungumzie pembejeo na mambo ya masoko na shughuli za ugani, sasa alizungumzia kidogo akiwa Chitete Momba tena akiwalenga zaidi watu wa Momba wakati ilitakiwa iwe hoja kuu ukanda wote huu.
Hapa ndipo angweza kueleza jinsi vikwazo na mageti yanayowekwa na serikali kuwanyonya wakulima, kupangiwa wanunuzi,kuzuiwa kuuza popote utakapopata soko na kusaidiwa pembejeo na kuwekewa bima za mazao bila kusahau pembejeo.
Kwa Iringa na Njombe angweza kuelezea jinsi ambavyo wafanyabiashara wa misitu na mazao yake wanavyolialia kwa tozo zaidi ya 20 maana waliwahi Mwambia rais alipokuwa ziarani Njombe sasa yeye ange-capitalize hizi kero na kuahidi kuzifuta na pia angeeleza jinsi mahusiano mabaya kati ya Tzn na Kenya yalivyowaathiri wakulima wa miti na horticulture maana soko lao kubwa ni Kenya.
Nne watu wa CHADEMA hawako makini au hawana taarifa sahihi za mabo ya kiuchumi maana huwezi kuwa unasema miradi ya reli haina tija kwa sasa(maendleo ya vitu) at the sama time unaahidi kujenga reli kati ya Mpanda-Sumbawanga-Tunduma. Huku ukisema CCM wameua reli ya Tabora-Kaliua-Mpanda wakati iko hai na inafanya kazi, huku ni kujichanganya na kukosa umakini na taarifa sahihi.
Kwanza sina hakika kama reli hii anayoahidi TL ni economically viable maana ukanda huu hauna mzigo mkubw kihivyo kiasi cha kuhitaji reli, pili ukanda huu una mipaka mingi na nchi jirani trade liberalization tu ndio inafaa na kuwawezesha watu kuzifikia nchi hizo jirani.
Mwisho Watu wa CDM hawana watu makini wanaoweza kuchambua takwimu za serikali, sera nk nk kama walivyo akina Zito, Lipumba, Bashe nk ,ni rai yangu watafute au wa-recruit watu wenye talent za uchambuzi watawasaidia sana kuweza kuchambua sera na takwimu za serikali na kuzihusianisha na maisha ya watu, akina ZZK wa ACT WAZALENDO waliweza kuonesha kwa kuichambua ilani ya CCM na utekelezaji wake na kuhitimisha kwamba CCM imetekeleza 31% tu ya ilani yake. Pili inatakiwa kabla ya mgombea wao kuhutubia wahakikishe wanatafuta kero stahiki za watu wa eneo husika ili zitumike kukoleza kwenye sera zao mama.
All in all kampeni ya jana kwa Mkoa wa Rukwa naona ilifanikiwa maana sio jambo la kawaida kwa watu wa mkoa huu kugeukia upinzani ghafla pengine ni kutokana na kupata wahamiaji wengi wa mikoa ya jirani kama Iringa, Mbeya na Songwe ambao wamewaambukiza tabia za kutoburuzwa na kudanganywa na CCM.
Karibuni kwa michango.