Uchaguzi 2020 Nilichoshuhudia kwenye kampeni za Tundu Lissu Sumbawanga, CHADEMA inafeli kwenye mikakati

Wazingatie Ushauri ili wafanikiwe, Wakiendelea na Kampeni za kuipigia kampeni NEC na Majibizano kwa wagombea wengine, wataishia kunawa tu. Wao wawaambie wananchi wa kila ukanda watawafanyia nini, wakipewa ridhaa
 
Mleta mada!!!
Mambo mengi uliyoyasema ndugu Tundu Antiphas Lissu ameyaelezea Vizuri kwenye kampeni zake. Alipokuwa njombe mjini na hata makambako na mufindi, nilifanikiwa kuangalia live kampeni zake , aliongelea vizuri tozo za zao la mbao na alisema wao watafanyaje

Alipokuwa mbeya na Songwe amesema vizuri sana juu ya Kuip a kipaumbele mikoa ya Nyanda za juu kusini, aliongelea Uhuru wa watu kuuza mazao yao sehemu wanazoona zinabei nzuri, alisema kuhusu kuifanya kanda ile kuwa sehemu kuu ya biashara kwa nchi yetu na nchi za sadc.

Inabidi ufahamu kuwa mgombea kwa siku anafanya mikutano rasmi 4 maeneo tofauti na pia anafanya mikutano mingine isiyo rasmi mingi akiwa njiani. Kwa sababu muda ni mchache ni ngumu sana kwa yeye kuelezea kila kitu in detail kwa sababu ya muda.

Hii ndo mana mgombea wa Chadema anahamasisha sana kuwe na midahalo kwa sababu kwenye mdahalo ndo mgombea anaeleza in detail Sera zake
 
Ushauri ni kitu kizuri, na wahusika wataamua kama wachukue kipi, waache kipi! Nafikiri wagombea wa ubunge na udiwani, wafanye research ya eneo analokwenda mgombea Urais , kabla TAL hajasimama, wao waeleze kero za jimbo, afu TAL azijibu kwenye hotuba yake!
 
Nimezisikia kampeni za Lissu za Leo Kirando Nkasi, Majimoto Kavuu na Mpanda, zimefuata ushauri wa mleta mada 100%. Wagombea wa majimbo husika wamesimama wakatoa kero za majimbo yao kisha zikafafanuliwa na mgombea Urais. Nkasi wamejibiwa CHADEMA watakavyofanya ili wavuvi wasichomewe nyavu, wakulima wapewe soko huria la mazao yao, Kavuu wameambiwa hakuna ng'ombe wa mfugaji atakayetaofishwa na serikali kwa kuingia kwenye hifadhi kwa bahati Mbaya, Mpanda wamehakikishiwa soko huria la Tumbaku na Asali.
 
Mleta mada nafikiri wewe ni neutral, hupelekwi na uvyama - Kwa nini nasema hivyo: umemrekebisha Mgombea wa CHADEMA at the same time umewapa point za kuegemea CCM watakapoenda kukampaini mikoa hiyo.
Very good
 
Na kaifafanua vizuri sera ya Majimbo akiwa Mpanda Mjini simply kabisa
 
Lissu anajitahidi sana hasa ukizingatia mazingira magumu ya upinzani chini ya serekali ya awamu ya tano.
 
Lissu anajitahidi sana hasa ukizingatia mazingira magumu ya upinzani chini ya serekali ya awamu ya tano.
Kibaya zaidi hawa mbuzi jike wa kijani wamewabana wapinzani kwenye kutafuta vyanzo vya pesa ili kuendesha kampeni wakati wao wanafursa ya kutumia hata pesa za umma kimagumashi maana tunawaona wanakuja maofisi wanapewa mafuta nk maana hawa wakuu wa taasisi ni wanachama wao.
 
Ni punguani tu ndie atakae shindwa kumwelewa Lissu narudia ni punguani

Sent from my BLL-L22 using JamiiForums mobile app

Mkuu yawezekana tuko mapungwani wengi mnoo, kwa kuwa Chadema ni chana kina jiita ni cha wasomi, uchambuzi wa kinachofanywa na Chadema ni vizuri utumie HYPOTHESIS ANALYSIS/ SYNTHESIS ANALYSIS kwa kila hatua.

Kila wakifanyacho kina kataa katika analysis hii, yeyote mwenye uwezo wa kutumia analysis hii ajaribu halafu atufahamishe.

Mwanasiasa mzuri ni sawasawa na Mwl yeyote mzuri :
- - jee unaweza ku connect na ama wafuasi wako?
- - jee unaweza ku connect na wanafunzi wako?

Unapotuma ujumbe kwa watu wako jee unashuhudia mzuka ?

Sio lazima uwe na elimu kubwa sana kuweza kufikisha ujumbe na ukawapa mzuka iwe wanafunzi au washabiki wako.

Na baada ya kutoa ujumbe , ukawapandisha mzuka, wataenda kulala huku wakiendelea kuamini ujumbe uliotamka kwa muda mrefu ?.

Kwa hiyo Kufanya au kutofanya vizuri kwa Tundu Lissu kutathibitishwa tarehe 29/10/2020.
 
Sera ya majimbo imewagusa sana watu mikoani
 
Sera ya majimbo imewagusa sana watu mikoani
Hii ni kiboko ya wapuuzi wanotumia pesa hovyo kwa kujipendelea kwao au kutumia pesa vibaya kama kufanya biashara za kununua wapinzani,kuhonga ,kugawakkawa pesa za umma hovyo au kuwanyima wengine maendeleo kwa kisingizio cha sijui hawajamchagua nani kutoka mboga mboga huu ni upuuzi mkubwa maana kodi tutoe wote na rasilimali za maeneo yetu zivunwe lakini eti tunyimwe kisa pesa zoote ziko mfuko mkuu.
Sera hii itakomesha mambo ya sijui rais alete stend mara rais katua bilioni kadhaa stupid
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…