Nilichoshuhudia leo wakati natuma fomu ya bodi ya mikopo

Nilichoshuhudia leo wakati natuma fomu ya bodi ya mikopo

alunashadya

Member
Joined
Aug 15, 2014
Posts
57
Reaction score
10
Habarini wanaJF wenzangu!

Nnatoa dukuduku ya niliyoshuhudia leo, leo nililazimika kwenda kuituma fomu ya bodi kinachoshangaza hawa jamaa wanataka tutume kwa EMS.

Nilifika posta nikakuta foleni kiasi ya watu wakingojea kupata huduma hiyo, nikaenda upande flani nikamkuta mlinzi anakagua form na kuzibana na kutoa maelekezo kilichonishangaza alikuwa anachaji mia tano kwa kila atakayempatia form kupitia pitia, hivi kwani ndio utaratibu?

Naona jamaa yule alikuwa anajipatia kiujanja ujanja isitoshe EMS wanatoza tsh 5500 per parcel!
 
hao wa 500 wameliwa,coz body wanataka receipt
 
Mm sijaelewa hapo,.....Ina maana huyo mlinzi alikuwa anatoa receipt ya ems au alikuwa ana charge watu wanaohitaji maelezo jinsi ya kutuma hzo form?
 
sijui kwanini nchi hii ni masikini wakati watu wanajua kutumia fursa hivyo mlinzi akikagua form 100 kwa siku ana 50000/= BRN Oyeee.
 
Mkuu ebu nisaidie hili,hizi fomu ukimaliza kujaza online ukaprint Nani na Nani wanasehemu yao ya kusaini kabla ya fomu kutumwa?kuna nafasi za serikali ya mtaa na ya kamishina wa viapo au hizi za online hazina?
 
Mm sijaelewa hapo,.....Ina maana huyo mlinzi alikuwa anatoa receipt ya ems au alikuwa ana charge watu wanaohitaji maelezo jinsi ya kutuma hzo form?

Yule mlinzi nilimgundua kama mjanja mjanja,hivi mimi nilimkwepa,risiti unapewa ukishakamilisha toka kwa watoa huduma wa EMS!
 
Mkuu ebu nisaidie hili,hizi fomu ukimaliza kujaza online ukaprint Nani na Nani wanasehemu yao ya kusaini kabla ya fomu kutumwa?kuna nafasi za serikali ya mtaa na ya kamishina wa viapo au hizi za online hazina?

Ktk online unajaza tu ukiprint unapaswa upeleke kwa kamishna wa viapo na serikali ya mtaa ndipo uitume
 
Mkuu, huo ni wivu. Mlinzi analipwa buku 80 kwa mwezi, hiyo fursa ya kuwapurusa jero jero zenu imekuja mara moja kama leo kwanini asiitumie.

Mbona mitandao inakuibia vifurushi kila siku hulalamiki, TBL wanapandisha bei ya bia na bado munanunua? Tuwe realistic kidogo, fikiria huyo mlinzi ndio mzee wako halafu atokee mtu kama wewe amharibie fursa yake adimu.

Umesikia wabunge watalipwa kiinua mgongo cha milioni mia ngapi?
 
Acha kushabikia ujinga wewe........huyo mlinzi babako nini???
 
Back
Top Bottom