Nilidanganya umri ukweni sasa penzi limekolea nachomokaje?

Mdukuzii

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
2,552
Reaction score
6,422
Nilikutana na huyu binti mwaka jana akiwa mmbichi kabisa, kutokana na muonekano wangu hakuwahi kuniuliza umri. ila nimempita miaka 15.

Kuna siku akanipa simu niongee na mama yake, mama mtu akaanza kuniuliza maswali mengi sana nikayapangua, alivyouliza umri nikapunguza miaka kumi.

Sasa naona penzi limenoga kwa bintiye nataka kuweka ndani mzigo na najua kila kitu kitajulikana. Uongo wangu utakuwa bayana.

Mama mkwe atanichukuliaje sijui akigundua nakaribiana nae umri.

Tofauti ya umri inaweza isiwe big issue tatizo ni kumdanganya mama mkwe,siku akijua ukweli imani juu yangu itapungua
 
Kwenye eneo la posa na mahari hakunaga mambonya kuulizana umri.

Jipange tukachukue mwali wetu sheikh
 
Hiyo ishu ndogo tu. Kama kichwa kiko kama cha Lowasa kimwagie piko uchanganye na masizi.

Kama sura Ina mikunjo kama bumps za barabarani nenda saloon kabandikwe foundation kisha upigwe rangi.

Ikigoma nenda kwa painter wa rangi za nyumba.

Siku ukifika utaonekana underaged
 
Na hutokubaliwa labda uwe na mkwanja watakuvumilia
 
Wadanganye tena
 
Kwani kuna takiwaga kupeleka cheti cha kuzaliwa ili kuonyesha miaka yako wakati wa taratibu za kufunga ndoa??

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
kikubwa binti anakupenda
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…