Nilidanganya umri ukweni sasa penzi limekolea nachomokaje?

Nilidanganya umri ukweni sasa penzi limekolea nachomokaje?

Dah mkuu ila kwa ushauri wangu kama wewe una 35 ina maana binti ana 20. Kumuoa binti wa umri huo ni sawa na kujivika mabomu na kuishi kwa matumaini kwamba hayatalipuka. Unless awe ni binti anaejielewa sana.
Anajieleea sana,hata mama yangu aliolewa na umri huo ba leo ana wajukuu na hakuwahi kuachika
 
Wanawake huwa tuna maumbo mabaya mwanamke wa miaka 30 huwezi fananisha na mwanaume wa miaka 30.

Zamani walikuwa wazee wanapishana na wake zao zaid ya miaka 10 na ndoa zinadumu kama uko kwenye 30' tafuta bint wa miaka 20 aliyetulia oa utanishukuru mkuu.
Ndio sio miaka 10 Sasa I'm talking with experience Ambayo nimejiona

Last year Kuna Mzee 1 na mkewe for now ni marehemu , huyu Mzee alikuwa na miaka 68 mkewe alikuwa na miaka 50 baada ya Mzee kustahafu kazi Yeye alikuwa mtu wa kupumzika home muda mwingi ila mkewe kutwa kucha alikuwa ni kiguu na njia hiyo Tabia ilikuwa Ina mkwaza sana yule Mzee lakini afanyaje Sasa wakati Yeye tayari ameshachoka na mkewe Bado ana nguvu mwili Bado una hitaji kushughulikiwa
 
Unaweza kuwe mkwe wake hata kama umemzidi mtoto wake miaka 20. Babu yangu wake zake wengine walikuwa ni wadogo kuliko mtoto wake wa kwanza
Acha woga mimi nimezaa nae watoto wawili na kwao hata sijafika na mama mkwe na baba mkwe tunaongea fresh, na binti yao naishi naye hadi leo. Tulikutana Dar na wazazi wapo Kilimanjaro
 
Mama mkwe ni kijana au ni mzee? Naona ni kama mmeanza mapema
 
Acha woga mimi nimezaa nae watoto wawili na kwao hata sijafuka na mama mkwe na baba mkwe tunaingea fresh, na binti yao naishi naye hadi leo. Tulikutana Dar na wazazi wapo Kilimanjaro
Dunia imebadilika sana
 
Wakuu mwanaume inabidi umzidi miaka mingapi mke wako ? Mwenye uelewa atuelekeze !!
Hakuna guarantee bwana mim mzee wangu kiheshima yupo mkoa mwaka juz koa mwanmke kamzidi miaka 35 na wamezaa watoto mzee ana miaka karibu 75 Kifupi vijana wa Sasa tupo na mashida mengi sana asee siku moja nilimulza mzee vip huogopi kupolwa Mali na vijana jibu alilo nipa labda wanibie wazee wezangu sababu wao wanambinu nyingi sana vijana kama nyiny hamuwez kabsa akaongeza ukitaka kuoa wake wengi na wasikupe shida njoo nikufundishe baba zako tulikua tunafanyeje maana mzee hadi alipo fika ana wake karibu sita na wote wanamogopa balaaa na kumueshimu
 
Dah huyo ndio legendary
 
Back
Top Bottom