Hakuna cha bure mjini zaidi ya salamu.
Demu; Mambo Mkaka
Jamaa: Poa mrembo.
Demu; Sorry! Eti Yombo4 ni IPI?(Kwa upole)
Jamaa: (akiwa kachangamka tofauti na awali). Ahaaa! mbona umefika, Ni lile jengo ukivuka kile kidaraja.
Demu;: Ahsante Mwaya,
Jamaa: Usijali
Demu anaanza kuondoka kule alipoelekezwa. Kabla hajapiga hatua ya tatu anasikia sauti nyuma yake ikimuita si kwa jina lake.
Jamaa: Mrembo...! We Mdada!
Demu: (akiwa kageuka) Abeee!
Jamaa: Samahani, naweza kupata contact no. Zk?
Demu: (Akishusha pumzi), sorry sina simu Mimi.
Jamaa: (Kimya kilichoshahibizwa na kaupepo).
Mara ghafla wakiwa wamesimama Mlio wa simu kutoka katika mkoba wa Demu unasikika. Jamaa akanyanyua uso wake kwani alikuwa ameangalia chini.
Demu anasikia haya huku akiitoa simu mkobani.
Demu: Hee hello
Sauti kutoka simuni: Nimeshakuona tayari, angalia Mkono wako wa kulia(Ilikuwa sauti nzito kiasi ya kiume).
Demu anageuka mkono wa kulia kama alivyoelekezwa, Anakata simu baada ya kumwona Mwanaume aliyepo ndani ya gari ambaye bila shaka ndiye aliyekuwa anaongea nae. Anamuaga jamaa kwa kumpa Shukrani ya Punda huku jamaa akimtupia dua zake ambazo asilani hazimpati mwewe.
Jamaa anatoa kisimu chake cha kupanguza, anaonekana anaandika kitu kwa simu huku akiwa amekunja Uso.
Mimi napita namchungulia anachoandika, kumbe kaingia JF kutoa dukuduku lake.
Ameanzisha uzi wake Usemao "Nilidanganywa kumbe chuo hamna Mademu"
Sijafanikiwa kujua alichoelezea zaidi ya kichwa tuu.
Nasogea pembeni namimi Naingia JF ili nione atakachopost.
Hahaaaaaa!! kumbe ndio hichi.
Pole Mkuu Chuoni hakuna cha bure zaidi ya Salamu