Nilidanganywa kusoma PGM nitakuwa rubani, leo hii mpishi kwa Mhindi

PCM, PGM, PCB, usipokaza msuli haswaaaah, ndoto zote zinayeyuka na kugeuka hadithi.
Ila usijari ishi ndan ya hali uliyopo. Komaa utafanikiwa tyuuh.
Kuna maisha pia nje ya ndoto zako.
 
Na pgm yangu niliishia kusoma agriculture engineering sua pamoja na wani yangu Kali hakuna cha urubani wala mavi yake urubani
Poleeeeeh sana.
Kuna maisha nje ya ndoto zako. Kubali hali iliyopo kwa sasa kwako.
 
Kusoma urubani hadi kuja kuaminika urushe ndege yenye abiria inakost hela nyingi sana.
Sidhani kama board ya mikopo wanaweza kutoa mkopo wa aina hiyo.
Lakini kama umefaulu PGM una chances zingine siyo lazima urubani.
 
Mpaka hapo wewe ni rubani wa ugali.

Endelea kurubanisha ugali na ubwabwa wako
 
Hold on!, ina maana 2007 ulitakiwa uwe ume graduate chuo kama ulisoma digrii. Hii miaka ajira zilikua nje nje kwa fani za sayansi ilikuwaje ukaangukia upishini mkuu?, au ulitoka na Upawa hapo Mkwawa?? Au ulikosa mentor?? Ila vipi uliendelea na shule kwelii??
 

Hapo kwenye GPA na kazi labda kama anatafuta serikalini ila kwenye watu wanataka production ipande unaweza kuwa na GPA kubwa na ukatolewa nje na mtu mwenye 2.0 ambaye ni productive.

Ila haimaanishi watu wasitafute hizo GPA kubwa ila wajue wanataka nini baadae. Kama wanaitaji kuwa wakufunzi basi wakomae nazo tena sana.

Pia GPA kubwa inategemea na chuo pia hapa ndio balaa lilipo, ukiwa na GPA kubwa kutoka SAUT, TUDARCo, TUMA na vyuo vingine vya private unaonekana kama vile ni 'GPA yakupewa' hata kama umeiangaikia mwenyewe.

So GPA kubwa sokoni ina nguvu kutokana na umesoma chuo gani hili usisahau washauri.
 
Minilisomea masomo ya biashara Sasa hivi nimjasiriamali nimepitaaa mulemuleeee
 
Darasani mlikuwa wangapi?

Chukulia intake tano tu. Watakuwa wamemaliza watu wangapi na kufaulu hiyo PGM?

Tanzania ilikuwa na ndegena marubani wangapi wakati huo?

Ungeweza kupata picha ungekuwa rubani wa ndege zipi?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaaah, kuna mtoto wa kaka akitaka kusogoa ndo anafanya hvyo.
Yaan huwa nacheka had baas
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…