Nilidanganywa kusoma PGM nitakuwa rubani, leo hii mpishi kwa Mhindi

Kupitia upishi huo huo ni fursa ya kuanzisha cafe yako kisha hotel nk.
Hata KFC na Macdonald walikuwa ni wapishi
 
Usikatishe watu tamaa mwanangu.. kama wewe umefeli kufikia Ndoto yako ni kutokana na kukata tamaa kwako.. wapo watu nawajua wamekuwa marubani bila hata hiyo PGM yani cha muhimu ni kupambania Ndoto tu

2001 kuingia jeshini ilikuwa very simple.. ungepambana uka apply ungefanikiwa vizuri sana
 
Kusoma si kutusua maisha mmoja ingawa unaongeza chance ya kutusua. Kuna wasomi ambao elimu bado haijawakomboa.

Shida elimu yetu ambayo ndo hasa wengi wanaipitia haimuandai mhitimu kujiajiri lkn pia mifumo yetu haipo kumsaidia mhitimu katika namna ya yeye kujiajiri, mfano kumwezesha mhitimu kwa mikopo ya fedha au vifaa kama mtaji ambavyo vingeweza kumfanya ajiajiri.

Mikopo ya asilimia 2 (Women &Youth Fund) inayotololewa na serikali kupitia LGAs ni midogo kuweza ku-accomodate wingi wa vijana wanaohitimu masomo vyuo vikuu na vile vyuo vya elimu ya kati.

Wengi wanaotusua utakuta ni wale maisha bora ambao wanakuta mitaji ilishakuwepo tangu enzi katika familia zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…