Nilidanganywa kusoma PGM nitakuwa rubani, leo hii mpishi kwa Mhindi

Nilidanganywa kusoma PGM nitakuwa rubani, leo hii mpishi kwa Mhindi

Hiyo kazi yako ya sasa ina weza ikawa na faida kuliko huo urubani ambao ungeupata

Ungekua rubani kama n "me" ungegongewa sana mkeo,usingepata muda wa kukaa na familia

ila sasa unapata muda plus uhakika wakumuhudumia wife 24/7 upo,kwanini unajilaumu?

Tujaribu kuthamini vile tuvifanyavyo yawezekana ni bora kuliko matamanio yetu yatakavyo.
 
.
tapatalk_1571131754906.jpeg
 
Ikiwezekana vyeti ulivyonavyo vichane chane, hapo ulipo kwa kanjibai kaa kwa malengo, soma sana mapishi ya vyakula mbalimbali, vijaribu kupika hadi uweze kupika, lenga mbali zaidi kua someone kwenye upande wa mapishi ya vyakula vya kimataifa vinavyopikwa kwenye hoteli za kuanzia nyota tano, ikiwezekana uwe na dream ya kufungua hotel yako,
Nikipata muda ntakuja kuweka stori ya maisha ya mpishi maarufu nusr wa dubai
UK kuna mpishi mmoja anaitwa Jimmy Oliver mshahara wake hata rubani mkuu wa ATC haoni ndani. Kwa hiyo hauko pabaya unaweza toka kimaisha
 
Komaa Ndugu Kufikia Malengo Na umshukuru Mungu uko na uhakika ya kujipatia Ridhiki bado, Pia bado umedhiirisha ili yakua Tz Vijana Wengi tunaamini Maisha pasipo Elimu Hatuna Nafasi Tena na tunaishia kata tamaa Huu n Udanganyifu, Ukiwa unatumikishwa hapo nawe taratibu wekeza Pembeni kwa vijibiashara vdogovidogo Kufikia kubwa.
Wakati nasoma A-level, Mkwawa High School (1999-2001) ulipita uvumi kuwa tunaosoma PGM tunaandaliwa kuwa marubani lakini leo hii ninafanya kibarua kama mpishi kwa Mhindi Masaki.

Aisee elimu hii ovyo sana.
 
Wakati nasoma A-level, Mkwawa High School (1999-2001) ulipita uvumi kuwa tunaosoma PGM tunaandaliwa kuwa marubani lakini leo hii ninafanya kibarua kama mpishi kwa Mhindi Masaki.

Aisee elimu hii ovyo sana.

You shouldn’t regret, my friend! Aliyekuumba na kukuleta hapa duniani sio mbahatishaji kamwe. Alifanya hivyo kwa kusudi maalumu, ambalo lazima litimie kwa wakati uliopangwa.

Ujanja wa samaki ni kwenye maji na ujanja wa tumbili ni kwenye miti. Samaki ukimtoa kwenye maji ukamueka porini (ambako tumbili anaendesha maisha yake vizuri sana) atakufa kwa kukosa hewa. Tumbili naye ukimtoa kwenye miti ukamzamisha kwenye maji (ambako samaki anaendesha maisha yake kwa tija kubwa) atakufa kwa kukosa hewa vile vile!

Kama ulikusudiwa kuwa samaki, obviously, ujanja wa kukwea miti utausikia bombani. Hali kadhalika, kama ulikusudiwa kuwa tumbili, ujanja wa kuogelea na kuishi ndani ya maji utausikia bombani tu.
 
Back
Top Bottom