Nilidanganywa kusoma PGM nitakuwa rubani, leo hii mpishi kwa Mhindi

Nilidanganywa kusoma PGM nitakuwa rubani, leo hii mpishi kwa Mhindi

Wakati nasoma A-level, Mkwawa High School (1999-2001) ulipita uvumi kuwa tunaosoma PGM tunaandaliwa kuwa marubani lakini leo hii ninafanya kibarua kama mpishi kwa Mhindi Masaki. Kea mshahara wa 250,000/= kwa mwezi

Aisee elimu hii ovyo sana.
pika tu mwanangu maana hakuna namna
 
Hivi kwanini huwa husomi umetulia mtoto wa kisukuma? Unakurupuka tu! Nasema mwanafunzi akiwa serious na masomo hawezi kukosa kutimiza ndoto zake. Hakuna visingizio. Magenius wataonekana NECTA si vijiweni
Tz haina na haijawahi kuwa na ma genius wanaopata one necta ni wale wanaokomaa kweli kweli
 
Hahaha unaweza zaliwa mshambuliaji ila maisha yakakuchezesha kama kipa
Kufikiri wewe ni mshambuliaji haimaanishi ndio umezaliwa hivyo

Huwezi kusema umezaliwa mshambuliaji eti kwa kuwa unapenda kuwa mshambuliaji

Mwisho wa siku kuna anayepanga wewe uwe nani

Wewe unafikiri umezaliwa mshambuliaji lakini mpangaji amepanga uwe kipa
 
Kwahiyo unapika pilipili tu huko Mshukuru Muumba muweza wa yote hapo Fanya kama steping stone make hela nenda chuo kasomee urubani

Mimi nilisoma PCM nikasoma accounts nikakopa hela bank mil.80 na nikatembeza bakuli nikatafuta scholarship nikaenda Australia nika graduate FPCTL sasahivi ni rubani Etihad airways nalipwa dola 12 elfu p/m.Yani in mwendo wa paris, london, Frankfurt, Bangkok, Usikate tamaa.
Million 80 ulikuwa unafanya kazi gani
 
Uliambiwa usome wewe ukacheza unafikiri nini? Lazima adhabu ya kutokusoma ikuandame. Ungalipata div one A physics, A maths ungeenda engineering tu. Angalia vyuo vya engineering vinavyohaha kutafuta wanafunzi. Rubani kwa taarifa yako ni dereva kama wa Passo ila yeye Passo yake inaruka angani.
Kumbe ni vyuo ndo vinahaha, nilidhani makampuni ndio Yana haha kutafuta maengineer , basi sawa
 
Back
Top Bottom