Nilidhani mabinti wa dukani wanafanana, najuta kumpoteza binti aliekuwa ananifanya niagize mzigo kila wiki, nimebadili wawili ila biashara inasua

Umenikumbusha kuna wakati nilikua nasimamia tractor ya mama mmoja hesabu yake kwa siku nilikua nampa laki tatu na mimi nabakiwa na laki na nusu siku zingine kazi zikichanganya nabaki mpaka na laki mbili hapo ni baada ya kutoa matumizi yote ya siku na kianzio cha siku iliyofata

Sasa watoto wake baada ya kuona napiga pesa fitna ikaingia wakanitumbua ili wasimamie wao, msimu uleule tractor ilipaki juu ya mawe na haijawahi kutembea tena ni miaka sasa imepita
 
kipindi nafanya udalali wa magari nili experience hii kitu aysee hakuna washirikina kama madalali nikawa naingizwa kwenye deals tu ilimradi nihusike bila mimi kujua baadae nakuja kuskia story kuwa watafute mtu mwenye nyota sijui ya moto wana wakanizoom baada ya kuambiwa tabia za nyota ya moto mimi nikawa naona wananipendelea kumbe natumiwa lol
 
Ngoja kwanzi nicheke[emoji23].
 
Nyota yako inaendana na ID yako kabisa 😂
 
Biashara inategemea sana na upepo wa mtu yani. Kuna mtu akikaa biasharani anakuwa anakubalika na watu humiminika.
 
Tafuta mwingine mwenye kibali mweke hapo utoboe.
Wakati mwingine tunafanikiwa kupitia nyota za wengine
Umeisema kimkakati sana mkuu neno fupi sana KIBALI tu asomae na afahamu
 
Umefanya general assumption ila katika hayo maelezo yako kuna point unayo miss na ndio tatizo lilipo hapo, tatizo wala sio muuzaji?
 
Matinde aliondoka nikaleta mfanyakazi mwengine, miezi miwili mbele nilifunga Duka. Matinde rudiiiiiii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…