Nilidhani wanaokimbia madeni wanafanya kusudi

Kuna baadhi ya wadoni wakikudai deni halikimbiliki kukimbia kwako ni kufa Tu....kuna mzee alikunywaga maji ya betri kisa 1.5mil nikamuona mzembe mno...
Lakini Leo laki moja(100k) ya TALA inaninyima usingizi mixa kutangazwa
 
Zamani nilikuwa najua watu wanao kimbia madeni wanafanya kusudi

πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
Ukipitia kipindi cha kudaiwa inafika muda na wewe ukiwa wadai watu unawaelewa.
Hapa kati nimekuwa nikisamehe madeni maana kuna muda unamwona mtu si kwamba hataki kulipa ila uwezo hana.
Kuna kipindi nlikuwa nadaiwa na sina ela ya kulipa mwisho nikapoteza marafiki na kuitwa tapeli kumbe sikuwa hata na mia mbovu.
 
Nadaiwa milioni 50 jumla yote.hapa nilipo naongea na benki zinazonidai na watu binafsi wanaonidai nione jinsi ya kuwalipa japo biashara zangu zote zimefilisika.
Tunatakiwa kuwa wavumilivu tunapodaiwa na wenye mali,tuvumilie matusi na kauli za unyanyapaa kutoka kwa ndugu na marafiki.
Mnaotudai hakika tunatamani kuwalipa lakini tumefilisika
 
Ukiishiwa rafiki na ndugu wanakutenga, hiyo hali naipitia mimi saizi.nimekimbiwa hadi na mwanamke kwakua nimefilisika
 
Pole mkuu 50M πŸ‘€πŸ‘€πŸ€”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…