safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,837
- 17,412
Sahihi mkuu umenigusa sana uliposema kwamba kama ulipitia kipindi cha kudaiea inafikia muda na wewe ukiwadai watu unakuwa muelewa.Ukipitia kipindi cha kudaiwa inafika muda na wewe ukiwa wadai watu unawaelewa.
Hapa kati nimekuwa nikisamehe madeni maana kuna muda unamwona mtu si kwamba hataki kulipa ila uwezo hana.
Kuna kipindi nlikuwa nadaiwa na sina ela ya kulipa mwisho nikapoteza marafiki na kuitwa tapeli kumbe sikuwa hata na mia mbovu.
yani madeni yalinifanya nizidi kuwa muelewa kwa wengine,nikimuona mtu kajiua kwa madeni sishangai maana sometimes madeni yanafika kwenye koo.
Unashangaa mtu anakuwa mbabaifu halipi anachenga nyingi ila nikikumbuka na mimi nilivyokuwaga mpiga chenga bila kutamani kuwa mtu wa aina hiyo bas najikuta nachoka saana na kuwa mvumilivu.
Kuna wakati nilibadili mpaka laini ya simu ili wanaonidai wasinipate hewani na sio kwamba sitaki kuwalipa ila sasa sikuwa na hela ya kuwalipa na nimechoka kuwapa ahadi na kuwakera.
Leo hii ninayemdai akinizimis simu sishangai maana najua fika angekuws nayo angenilipa freshi tu,ila najus hana ndiio maana anapiga chenga nyingi.
Mtu akinijia na shida na akstaka kunikopa huwa nakumbuka mateso ya kudaiwa.
Alafu kuna wakati watu ambao unawaheshimu kabisa na haukutarajia kupoteza uaminifu kwao ndio unsjikuta unawapiga chenga kali huku nafsi inakusuta ila ndio maisha na wao wanakuvumilia ila huwa wanaelewa.
Kwenye haya maisha kuna nyakati lazima uwe mbabaishaji,lazims uwe mtu wa kona nyingi,lazima wanaokudai wasikuelewe vizuri,wakuone hautaki kuwalipa na wengine watajiuliza kwani hela anapeleka wapi ?
Hizo nyakati unakuwa hivyo ni mwili na hulka yako inajilinda ili ipite salama kwenye mazngira hayo.
KUna nyakati nakumbuka nilishamkwepaga sana konda ili nisilipe nauli na nilikuwa nafanikiwa then nauli hiyo naitumia kwa mambo ya msingi kama nyanya,yote ni madeni hayo ila moyoni nilijua kwamba hii sio tabia yangu😀😀😀