Nilienda ku meet na mwana JF, kumbe ni pink panther

Nilienda ku meet na mwana JF, kumbe ni pink panther

bobby dolat

Senior Member
Joined
May 18, 2015
Posts
167
Reaction score
263
Jana nimeenda kuonana na mwanamke mmoja ambae tumekua marafiki kwa mwezi mmoja ndani ya JF, tulishapeana namba za simu siku nyingi na huwa tuna chat whatsaap. Sasa nikaingiwa na uroho wa kutaka kumgegeda maana tukiongea kwa simu huonesha mahaba katika kuchezea sauti yake.mara abane pua, na majina yetu yalishabadilika sasa tunaitana honey ingawa hatujaonana.

Mimi amekua akiona picha zangu whatsaap mara kwa kwa mara ila yeye hajawahi kuonesha picha. Sasa jana tukakubaliana tuonane jioni baada ya kazi wakati tukisubiri foleni iishe. Nikapaki City garden lakini sikushuka kwenye Gari, Mara naona Toyota Cienta nyeusi inapaki likashuka jimama moja mfano wa pink panther wa kwenye filamu ya Eddie Murphy, likashuka kwenye Gari huku likionekana kupiga simu na simu yangu ikaita nikapokea.

Likanimbia limefika nikasema poa, nikataka niondoe Gari nikimbie lakini nikasema sio vizuri nikamfuata pale tukaacha pale magari yetu tukatembea kwenda jojes nyuma ya NMB Bank house.Yaani kwa muonekano ni kama mama na mwanae nilisikia aibu ya aina yake. Halafu jimama lenyewe bahili kweli limekunywa bia 14 supu ya kuku, nyama ya mbuzi na ndizi za kuchoma mhudumu alipokuja kudai hela likajikausha likijifanya kuchati na simu nikalazimika kulipa ingawa mm nilikunywa bia tano tu na viroba vinne vya kujazilizia ulevi.

Sikutaka kula maana ugomvi wa mke wangu naujua iwapo nimekula nje.Tumeachana saa tatu usiku nikiwa na 500 tu mfukoni sina hamu nae na sitaki tena naomba wewe mama tulietoka Jana usinitafute tena. Mtu unakunywaje bia kumi na nne? Nimegundua kuwa kumbe ukiona demu wa JF anakushobokea ujue huyo ni mbaya hana mvuto kauawa sura. Ukiona post zake humu na jinsi anavyo pretend kama vile yupo juu kumbe ovyo.
 
Pole sana kwa yaliyokukuta;

Sasa mkuu unataka kumgegeda kwa kukutana siku moja tu??????

Hujui tabia yake, humjui jinsi alivyo, wewe umeshaweka nia ya kula kitumbua huenda kina mchanga utajuaje??

Chukua taahadhari.........!!!!!!!!!!!


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
We acha kashfa hizo kwani kuna mtu alikutuma kufanya hayo?
 
Haaa haaa kama vile nakuona vile halafu utakuta mshale wa unakimbilia E haaa haaa ndio ukome kushobokea wanawake hovyo.
 
Unaonekana mkuu wewe ni mzinzi sana una mke lakini bado macho waluwalu
 
duuu pole BOBY dolat, ungemwambia akutumie pic wasap. mi ndo mana cpendag haya mambo kugawa no ya cm bado sana urafiki unaishia pm basi. mana humu nifull maigizo. kuna mtu alinipm no yake na jina halisi akaomba sana nimpe no nikapotezea.

juzi kanitumia tena no ya cm ingne na na jina lingine tofauti na alotuma mwanzo nikabaki nacheka hata sir name alotaja sahiz na mwanzo ni tofauti. nikamwacha aendelee na drama zake akichoka atacha.
 
Hahaha next time simu yako weka either vibration au silent mode ukikuta mtu tofauti na expectations zako unauchuna atapiga simu akichoka ataondoka mwenyewe wewe kimya unasepa na wewe.
 
Mkuu ina maana hela zako zimeenda burebure......acha hizo bana,we fumba macho tu mtafune kisha uje utupe ripoti hapahapa.Usikute ni mtamu balaa........
 
hahaha nmecheka lakini haichekeshi.......wewe kama hutaki pink panther mie ndio ugonjwa wangu huoo,napenda kuona minyama ikitikisika mdebwedo......

kanywa bia 14 na wewe 5 na viroba juu....mhh mpaka saa tatu sitaki kuhamini labda kama mimi sio mnywaji pombe maarufu pale kisuma
 
avatar290004_3.gif
jamaa yangu bia 5 sio mchezo tena ukute ni Safari na viroba 4 vya Konyagi ni lazima wewe utabebwa
halafu yeye kanye bia 14 supu nyama choma ya mbuzi hapo humtoroki ni kabali na kipochi manyoya utakigegeda tu
 
Mjusi mtukutu, hulilia kia la gutu. ungejituliza na mkeo ukazisemea genye zako wala yasingekukuta.
 
Back
Top Bottom