Nilifanya kosa la kununua mipira ya kiume, (condoms), njiani kwa matumizi ya nyumbani na mke, imekuwa ugomvi sana, nyumba haikaliki

Za siku wakuu.

Kosa nililofanya, niko njiani natokea likizo nyumbani naelekea kazini, ninakoishi pamoja na familia nikasema nichukue mipira ya kiume (condoms), ili nikifika nyumbani kwa mke tuweze kutumia kwa ajili ya kuzuia mimba.

Wakuu nimefika nyumbani wife kageuza kibao, anasema hizi condoms ulichukua za kufanyia nini?, namwelewesha hanielewi, ndani hapakaliki.

Anasema ulikuwa unafanyia mambo yako afu unasema umeleta tutumie. Haelewi kabisa.

Wakuu hii shida inatatulikaje, najuta ningeacha tu kufanya ivo.
Shida ya uelewa na ndio umaskiki wa mwafrika,zaidi asiyeamini kwenye sayansi ya afya
 
Umejipalia mkaa,,,,,mkeo ana haki ya kukuwashia moto,,, yaani usafiri, from no wwhere urudi na condoms alafu ujitetee ulinunua ili mzitumie? Unamuona yeye ni ndezi ? Hawez kukuelewa, labda ukute huwa mlishawah kutumia before,,,, Ngumu kumesa mzee
 
Za siku wakuu.

Kosa nililofanya, niko njiani natokea likizo nyumbani naelekea kazini, ninakoishi pamoja na familia nikasema nichukue mipira ya kiume (condoms), ili nikifika nyumbani kwa mke tuweze kutumia kwa ajili ya kuzuia mimba.

Wakuu nimefika nyumbani wife kageuza kibao, anasema hizi condoms ulichukua za kufanyia nini?, namwelewesha hanielewi, ndani hapakaliki.

Anasema ulikuwa unafanyia mambo yako afu unasema umeleta tutumie. Haelewi kabisa.

Wakuu hii shida inatatulikaje, najuta ningeacha tu kufanya ivo.
Siku nyingine toa taarifa kabla ya kununua na kupeleka icbm nyumbani. Mletee zawadi sasa akusamehe achana na kulalamika
 
Linakushida vipi jambo jepesi kama hilo. Watu tunakutwa na condom pc moja pekee, halafu tunaweza kuelezea mbili zimeenda wapi na mwanamke anaridhika. Acha uzembe
 
Mimi ndo maana ntachelewa kuoa!

Yaani kwenye ndoa huwezi kufanya maamuzi Binafsi na kufikia muafaka pasipo kumshirikisha mwenzio.

Ulitakiwa kumueleza Hilo jambo mapema ! Kwa akili ya kawaida fikiria wewe unarudi safarini Kisha unakuta ndani kwa mkeo Kuna condom!

Yaani alinunua pasipo kukushirikisha wewe! Muelewe ni binadamu pia.

Cha kufanya muoneshe huu uzi au kajisalimishe kwa kiongozi wa Kiroho akusaidie
Wakat naoa nilipata shida sana kwa mambo kama ukitaka kutoka uage,ukichelewa utoe taarifa,sjui ukitaka kufanya nn lazima umjulishe mwenzio,ni kaz sana kwa kwel
 
Na huwa mnatumiaga condom? nani huwa anakuwa mnunuaji wa hizo kondom?

Nje ya mada: hivi huwa mnawezaje kutumia kondom kwa mke kabisa sijawah mimi, kwanza mke wangu alisema hazipend tunatumia njia ya kalenda kupanga
 
Mwambie tu ukwel ulvokua huko ulizidiwa,ukajishindia katoto fulani sasa kumbe kana UTI sugu,nawewe imekuvaa sooooo unaogopa kumuambukiza🙂
 
Next time pangeni pamoja njia za uzazi wa mpango.
 
Kama ulikuwa na nia thabiti, amekataa mwambie basi kama hutaki. Akizidi nenda katafute mchepuko ununue nyingine utumie kabisa.
 
Za siku wakuu.

Kosa nililofanya, niko njiani natokea likizo nyumbani naelekea kazini, ninakoishi pamoja na familia nikasema nichukue mipira ya kiume (condoms), ili nikifika nyumbani kwa mke tuweze kutumia kwa ajili ya kuzuia mimba.

Wakuu nimefika nyumbani wife kageuza kibao, anasema hizi condoms ulichukua za kufanyia nini?, namwelewesha hanielewi, ndani hapakaliki.

Anasema ulikuwa unafanyia mambo yako afu unasema umeleta tutumie. Haelewi kabisa.

Wakuu hii shida inatatulikaje, najuta ningeacha tu kufanya ivo.

Babu zilikua ngapi? Kama tatu zote hazijatumika mwambie ni zako bibie.

Afu jifunze kushika siku za hatari za mkeo,ni kitu kama cha kiboya ila kinaokoa mambo mengi sanaaa
 
Fanya Yeye Ndio Anakuja Likizo Kwako Ulipo Na Condoms Alafu Aeleze Jinsi Uelezavyo,Je Kwa Upande Wako Ungemwelewa?
 
Wakat naoa nilipata shida sana kwa mambo kama ukitaka kutoka uage,ukichelewa utoe taarifa,sjui ukitaka kufanya nn lazima umjulishe mwenzio,ni kaz sana kwa kwel
Kweli mkuu!
Mimi nimejiapiza sitakimbilia ndoa kama Bado sipo tayari.
Ni lazima nikubali kuwa maisha ya ndoa katika swala la maamuzi linabadilika linakuwa si langu Bali letu
 
Za siku wakuu.

Kosa nililofanya, niko njiani natokea likizo nyumbani naelekea kazini, ninakoishi pamoja na familia nikasema nichukue mipira ya kiume (condoms), ili nikifika nyumbani kwa mke tuweze kutumia kwa ajili ya kuzuia mimba.

Wakuu nimefika nyumbani wife kageuza kibao, anasema hizi condoms ulichukua za kufanyia nini?, namwelewesha hanielewi, ndani hapakaliki.

Anasema ulikuwa unafanyia mambo yako afu unasema umeleta tutumie. Haelewi kabisa.

Wakuu hii shida inatatulikaje, najuta ningeacha tu kufanya ivo.
ulikutwa na mbili ,mkeo akakuuliza ile moja inayokaa peke yake iko wapi,?
 
Linakushida vipi jambo jepesi kama hilo. Watu tunakutwa na condom pc moja pekee, halafu tunaweza kuelezea mbili zimeenda wapi na mwanamke anaridhika. Acha uzembe
Hahaha, mkuu huyo mwanamke anayeridhika na maelezo yoyote yale utakayompa kwenye mazingira hayo mchunguze vizuri.
 
Hakika umekosea sana, Sasa cha kufanya muombe radhi yaishe na kama bado analeta kelele muulize anataka mlimalize vipi.
Kama utaona hitaji lake lipo ndani ya uwezo wako kubali ili yaishe, kwa sababu hauwezi ukambembeleza mtu ambaye hataki kuelewa.
 
Back
Top Bottom