Za siku wakuu.
Kosa nililofanya, niko njiani natokea likizo nyumbani naelekea kazini, ninakoishi pamoja na familia nikasema nichukue mipira ya kiume (condoms), ili nikifika nyumbani kwa mke tuweze kutumia kwa ajili ya kuzuia mimba.
Wakuu nimefika nyumbani wife kageuza kibao, anasema hizi condoms ulichukua za kufanyia nini?, namwelewesha hanielewi, ndani hapakaliki.
Anasema ulikuwa unafanyia mambo yako afu unasema umeleta tutumie. Haelewi kabisa.
Wakuu hii shida inatatulikaje, najuta ningeacha tu kufanya ivo.