Nilifunga ukurasa wa kutapeliwa lakini nimetumbukia tena

Trinity

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2017
Posts
1,828
Reaction score
3,508
Nawasalimu kupitia jina kuu lipitalo majina yote.

Direct, Jana katika pita pita zangu Instagram nikakutana na page jamaa anauza vifurushi bei chee sana, moyoni nikasema hapa hapa nitaokoa gharama za pesa kununua bando la internet.

Kumbe sikujua nipo kwenye mdomo wa mamba hatimae Nilijipeleka mzima mzima nikapigwa, siumii Kwa kiasi cha pesa nilichotapeliwa lakini naumia Kwa nini sikusikiliza sauti iliyokua inaniambia chunguza Kwa makini usije ukatapeliwa kama ulivyotapeliwa milioni 1.4 mwaka 2014.

Baada ya kutapeliwa mwaka tajwa hapo juu, nilijiapiza siji tapeliwa tena abadani, nilifanikiwa sikuwahi tapeliwa zaidi sana nimekua nikiwatonya watu kibao waliokua wemeshaa wekwa kwenye target ya kutapeliwa.
Ila sasa yamenikuta, kuwa makini aisee vihuni bado vipo sana.!!
 
unachotakiwa ni kuepuka na kuacha kabisa tamaa,

bure ni ghali gentleman,
Zidisha juhudi katika kufanya kazi kwani mtaji ulionao ni nguvu zako mwenywe πŸ’
 
unachotakiwa ni kuepuka na kuacha kabisa tamaa,

bure ni ghali gentleman,
Zidisha juhudi katika kufanya kazi kwani mtaji ulionao ni nguvu zako mwenywe πŸ’
Upo sahihi, Nimejiridhisha hawezi maana nimeview hata akaunti yake testimony za kutumiwa bando zinajirudia kwenye post tofauti tofauti.
 
unachotakiwa ni kuepuka na kuacha kabisa tamaa,

bure ni ghali gentleman,
Zidisha juhudi katika kufanya kazi kwani mtaji ulionao ni nguvu zako mwenywe πŸ’
We acha tu, nilipitia comment za wadau pale chini nikaona wengi wanashukuru kwamba wametumiwa bando lkn kumbe inaonesha ni abortion tu maana katika post zake 4, comments utaona ni zilezile.
 
Upo sahihi, Nimejiridhisha hawezi maana nimeview hata akaunti yake testimony za kutumiwa bando zinajirudia kwenye post tofauti tofauti.
ni muhimu sana wengine sote kuchota darasa na angalizo hili muhimu sana lililokutokea wewe mara kadhaa na kuthibitisha pasina shaka tena kwa vielelezo kwamba utapeli upo mitandaoni πŸ‘ŠπŸ’ͺ
 
We acha tu, nilipitia comment za wadau pale chini nikaona wengi wanashukuru kwamba wametumiwa bando lkn kumbe inaonesha ni abortion tu maana katika post zake 4, comments utaona ni zilezile.
inawezekana ni yeye mwenywe na timu yake wanajaribu kuwahadaa watu, kuwaminisha na kuwavutia wengi zaid ili kuwatapeli πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…