Kelela
Senior Member
- Nov 7, 2020
- 191
- 308
CRDB BANK:
Nilifungua account ya CRDB lakini nilikutana na mambo ya ajabu mpaka nikatelekeza account baada ya miaka 4.
Niliwahi kufanyia miamala ya kutoa pesa kwenye ATM za CRDB ndani ya mwaka mmoja tu baada ya hapo ikawa kila nikenda kutoa pesa ATM ya CRDB kadi inagoma inasema "This Card May not be used in This ATM".
Kwa kuwa ilikuwa ni MasterCard nikawa naenda kutolea pesa kwenye ATM ya NMB na ikawa inatoa pesa bila shida yoyote kwa takribani miaka miwili nilikuwa natumia ATM za NMB kutoa pesa na kadi yangu ya CRDB BANK.
Mwaka wa NNe nikahamia sehemu ambayo benki ya CRDB ipo karibu, Nikasema ngoja nikajaribu tena kutoa pesa kwenye ATM ya CRDB, alafu ilikuwa ni pesa ya dharura nayo na ilikuwa saa 1 1 alfajiri, ile kuingiza kadi tu, kadi ikamezwa (ikatumbukia moja kwa moja, haikurudi tena).
Nikakaa baada ya siku 2 nikaenda kwenye lile tawi kuomba kadi yangu, ndani nikakaa foleni takribani lisaa limoja na nusu ndio nikapewa kadi yangu.
Baada ya kupatiwa kadi na wakati huo nimechoka sana kwa kusubiri mule ndani Benki, Nikasema ngoja nipitie ATM nitoe pesa kidogo.
Kufika kwenye ATM nimeweka kadi tu, Kadi ikamezwa tena, aisee hasira nilizopata hapo nikaingia Simbanking nikahamisha pesa zooote. Tangu siku ile (ilikuwa mwaka 2020) mpaka leo sijaenda kuchukua kadi na wala sijaitumia tena account mpaka walipoamua kuifunga wenyewe.
Kuna mwengine aliwahi kupata changamoto kama hii au ni mimi tu?