Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Habari zenu wakuu,
Nimekuwa na mahusiano na binti mmoja,Ambaye tulikutana akiwa na miaka 18 nikiwa nimemzidi miaka 12 tukaishi naye pamoja (pika pakua) mpaka alipotimiza miaka 19 mapema mwaka huu.Naweza kumsifia kuwa ni binti ambaye hakuwa na makuu wala tamaa maana alinikubali na maisha yangu hata nikiwa sina sawa nikiwa nacho sawa pia alikuwa mchapakazi na mwenye kujituma sana katika kutafuta.
Siku za karibuni alipata ujauzito ila mahusiano yaliingia dosari baada ya kugundua kuwa alisaliti. Pia aina ya mawasiliano aliyokuwa akifanya na wanaume tofauti tofauti hayakuwa na afya kwa mahusiano. Roho iliniuma sana, Pamoja na ujauzito aliokuwa nao Nilimrudisha kwao nikamueleza kwamba hata huo ujauzito sina uhakika kama ni wangu. Amekuwa akilia na kubembeleza kuomba msamaha kusisitiza ujauzito ni wa kwangu, Yupo radhi hata DNA ihusishwe.
Sasa nimekuja kwenu kuomba ushauri,
Je, kwa umri huo kuna uwezekano wa kubadilika huko mbeleni?
Je, Ikiwa ujauzito ni wangu kweli (ninahisi hivyo baada ya kujihakikishia) itakuwaje?
Je, Ni kawaida kwa mabinti wa umri huo kuchepuka kwamba baada ya umri fulani atatulia?
Je, Nikubaliane kwamba mtoto apate malezi ya mzazi mmoja ? (japo roho inaniuma kuona mtoto wangu ataishi mbali na baba yake na sikutegemea nitawahi kuwa na mtoto wa nje)
Je, Malezi ya mtoto pasipo na wazazi wawili hayatakuwa na madhara kwa mtoto?
Nawasilisha.
UPDATE
Nimeendelea kuhudumia ujauzito na kwa jinsi tunavyozungumza anaonyesha kujutia mno kitendo alichokifanya na hata kulia na kutoa machozi kabisa akiomba msamaha.Sasa wakuu hii inaweza kuwa ni kutokana na ujauzito tu aliokuwa nao ndio unapelekea afanye hivyo au ni majuto kweli kutoka moyoni?
Nawasilisha