Nilijenga kwenye kiwanja cha mama mkwe,akachukua mkopo wakataka mie ndiye nilipe

Nilijenga kwenye kiwanja cha Mama mkwe, akaamua kuchukua mkopo kwa kutumia kiwanja hicho na wakataka mimi ndiyo nilipie!

Aliniambia tusijenge kwenye kiwanja changu kwa sababu ni mbali na mjini. Kwa kweli, niliona kama ni mbali, lakini akaniambia kuwa kuna kiwanja mama yake alimpa kama zawadi siku ya harusi yetu, hivyo tukibadilishe majina tukijenge. Sikuona zawadi hiyo ikitolewa rasmi, ila alinieleza kuwa mama yake alimpa kimya kimya. Kwa hiyo, niliongea na mama yake, naye akanithibitishia kuwa alipewa kweli.

Basi tukaanza mchakato wa kutafuta hati kwa ajili ya majina yetu. Yeye ndiye aliyekuwa anashughulikia kila kitu. Tulimaliza kila hatua, na mambo yalionekana kuwa sawa. Tukaanza ujenzi, nyumba ikakamilika na tukahamia. Lakini kila nilipomuuliza kuhusu hati ya nyumba, alinizungusha zungusha bila kunipa majibu ya kueleweka.

Siku moja nikiwa zangu nyumbani, nikashangaa kuona watu wakija kuangalia nyumba. Niliwauliza kulikoni, wakaniambia kuwa wao ni wafanyakazi wa benki flani na kwamba mwenye nyumba ametaka kuchukua mkopo. Nikamuita mke wangu, akaniambia, "Nilisahau kukuambia, mama alitaka kuchukua mkopo. Ujue kumbe mama alishachukua hati ya nyumba hii, na kwa sababu bado kule ardhi wanatusumbua kubadili majina, ameamua kuchukua mkopo ili afanye biashara na atalipa pole pole."

Nilishtuka, lakini sikujua nifanye nini kwa sababu nyumba haikuwa yangu rasmi. Nilimpigia simu mama mkwe, naye akaniambia, "Ina maana mwenzako hakukuambia? Basi mimi tayari nimeshajaza kila kitu. Kiwanja hiki ni changu, niliwapa tui la nachukulia mkopo nitalipa?” Alichukua mkopo ila alilipa marejesho matatu." Baada ya hapo, mke wangu akaniambia kuwa inabidi sisi tulipe mkopo huo kwa sababu mama amegoma kuendelea kulipa.

Nilijikuta sina kauli, na kwa kweli, niliona suluhisho pekee ni kaucha nyumba iuzwe ili kumaliza matatizo, kwelibenki waliipiga mnada wakachukua pesa yao. Sasa hivi tuko kwenye nyumba ya kupanga, tumeanza upya! Maisha yamekuwa magumu sana kwani nilikua na mikopo mingi, nimekata tamaa, na mke wangu kila siku ananidharau na kunipiga vijembe kuhusu ile nyumba kuuzwa. Sina amani kabisa, lakini tuna watoto, hivyo hata kumwacha siwezi.

MWISHO
sijamaliza kusoma yote mwanzo tu nimeona wewe ni kenge
 
Aisee, pole sana. Mungu akutie nguvu. Mimi nilijifunza siku nyingi cha mtu mavi, hata kiwe cha wazazi wako. Mkeo amelifanyia uhuni sana sana, sijui kwanini anakusimanga tena wakati kosa lake hakuwa mkweli? Hana utu hata kidogo
 
Mimi naona umetumia busara sana kuacha nyumba iuzwe, bado ingelipa deni ungesumbuliwa tu.

Bado naona pia umetumia busara kubaki na mkeo ili kutunza watoto.

Watoto wasipate shida kwasababu ya utapeli wa mama yao.

Endelea kupambana, mikopo itaisha utajipanga upya ujenge. Ila don't trust mkeo tena na usimruhusu akudharau kwa utapeli wake. Siku akikudharau mpe makofi ya maana au mwambie tu kile alichoona na kwanini umeamua kufanya vile...asikuone mjinga wakati umetumia busara sana.

Jifunze kutomwamini mtu mambo yako fanya mwenyewe uone kwa macho. Usiamini hata wazazi wako.

Usisikilize utopolo wa watz humu wanavokutakutana they are foolish and you are wise. Fanya vile moyo wako uliamua wala hukukosea.
 
Nilijenga kwenye kiwanja cha Mama mkwe, akaamua kuchukua mkopo kwa kutumia kiwanja hicho na wakataka mimi ndiyo nilipie!

Aliniambia tusijenge kwenye kiwanja changu kwa sababu ni mbali na mjini. Kwa kweli, niliona kama ni mbali, lakini akaniambia kuwa kuna kiwanja mama yake alimpa kama zawadi siku ya harusi yetu, hivyo tukibadilishe majina tukijenge. Sikuona zawadi hiyo ikitolewa rasmi, ila alinieleza kuwa mama yake alimpa kimya kimya. Kwa hiyo, niliongea na mama yake, naye akanithibitishia kuwa alipewa kweli.

Basi tukaanza mchakato wa kutafuta hati kwa ajili ya majina yetu. Yeye ndiye aliyekuwa anashughulikia kila kitu. Tulimaliza kila hatua, na mambo yalionekana kuwa sawa. Tukaanza ujenzi, nyumba ikakamilika na tukahamia. Lakini kila nilipomuuliza kuhusu hati ya nyumba, alinizungusha zungusha bila kunipa majibu ya kueleweka.

Siku moja nikiwa zangu nyumbani, nikashangaa kuona watu wakija kuangalia nyumba. Niliwauliza kulikoni, wakaniambia kuwa wao ni wafanyakazi wa benki flani na kwamba mwenye nyumba ametaka kuchukua mkopo. Nikamuita mke wangu, akaniambia, "Nilisahau kukuambia, mama alitaka kuchukua mkopo. Ujue kumbe mama alishachukua hati ya nyumba hii, na kwa sababu bado kule ardhi wanatusumbua kubadili majina, ameamua kuchukua mkopo ili afanye biashara na atalipa pole pole."

Nilishtuka, lakini sikujua nifanye nini kwa sababu nyumba haikuwa yangu rasmi. Nilimpigia simu mama mkwe, naye akaniambia, "Ina maana mwenzako hakukuambia? Basi mimi tayari nimeshajaza kila kitu. Kiwanja hiki ni changu, niliwapa tui la nachukulia mkopo nitalipa?” Alichukua mkopo ila alilipa marejesho matatu." Baada ya hapo, mke wangu akaniambia kuwa inabidi sisi tulipe mkopo huo kwa sababu mama amegoma kuendelea kulipa.

Nilijikuta sina kauli, na kwa kweli, niliona suluhisho pekee ni kaucha nyumba iuzwe ili kumaliza matatizo, kwelibenki waliipiga mnada wakachukua pesa yao. Sasa hivi tuko kwenye nyumba ya kupanga, tumeanza upya! Maisha yamekuwa magumu sana kwani nilikua na mikopo mingi, nimekata tamaa, na mke wangu kila siku ananidharau na kunipiga vijembe kuhusu ile nyumba kuuzwa. Sina amani kabisa, lakini tuna watoto, hivyo hata kumwacha siwezi.

MWISHO
Kumbe ukiwa na kiwanja tu, unaweza kupewa mkopo.
Kapeace hii kitu unaijua ?
 
Dalili ya chai huwa mtu anapost na kupotea.....

Ila kama ni kweli mkwe na mkeo wana roho mbaya sana.
 
Back
Top Bottom