Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Hamjambo wote!
1. Nje ya kuandika na kusoma soma ninapenda Kuogelea.
2. Sasa Kila wiki ninakuwa na ratiba ya kwenda beach kukata Maji baharini. Kwa Upare wangu mara nyingi naendaga Beach za bure hasa Siku za katikati za kazi. Weekend sio rahisi kunikuta huko.
3. Napenda kuoga Ile kabla ya saa tatu asubuhi maji yakiwa ndio yanakupwa(yanaondoka), hapo nitaogelea kwa lisaa limoja mpaka lisaa limoja na nusu. Hapo itakuwa saa tano maji yameshaenda mbali.
4. Nitarudi zangu ufukweni. Hapo nitatulia nikiperuzi, na kama kutakuwa na mademu nitawachokoza kidogo. Unajua Beach kuna kuviziana viziana.
5. Mabinti wanavizia vijana, na vijana wanavizia mabinti.
6. Najua kuna Wezi, nafahamu kuna waiba nyota, najua kuna waoga dawa za kina Kinjektile Ngwale.
7. Niliwahi kupata mtoto wa kizungu kutokea Austria, akiwa na wenzake watatu waliokuwa wanaota jua kama mijusi kafiri(Ile yenye vichwa nyekundu) Kule kwetu Makanya, upareni tunaiita Goromonda.
8. Nisingeweza kufa bila kukutana na Mzungu, muarabu, hiyo ilikuwa kiapo changu wakati Niko mtoto.
9. Oooh! Mtibeli unatupanga. Wewe hujui kingereza. Uliwezaje kuongea kingereza kumshawishi mzungu huyo.
10. Hehehee! Kwanza wazungu hawahitaji Mambo na maneno mengi. Lakini kingine sio kwamba Mtibeli hajui kingereza.
Ninajua kwa kiwango kizuri tuu cha kuridhisha na ndio maana nilimng'oa yule Muaustria.
11. Oooh of course, yeah. I know, I'm so happy(diamond song), happy to you me and all. Hivyo nisingeshindwa bhana!
12. Nimesema naenda kuogelea, kisha kuvizia na kuviziwa, alafu pia naenda kufanya Meditation ndani ya bahari .
13. Meditation ya ndani ya bahari inanisaidia mambo mengi Sana.
14. Naenda kwenye maji yenye usawa wa kifua. Kisha naelea chali, tumbo juu. Uso ukiwa unaangalia Jua na mawingu angani.
15. Kisha hapo nitakuwa naelea nikiwa naangalia mawingu na jua. Na kuanza ibada zangu.
16. Nusu ya mwili itakuwa majini, nusu ya mwili utakuwa unaelea juu. Ni kwamba Maji ya bahari yatagawa masikio, Mabega, tumbo na miguu. Tako ndani ya maji. Tumbo juu ya uso wa maji.
17. Hapo nitaelea kwa nusu saa mpaka dakika 45. Mawimbi ya bahari yakinipiga na kunipeleka huku na huku.
18. Mbinu hii ni Mbinu ya kikulungwa, lakini pia inahusika na Spiritual care, Spiritual cleansing. Kujitakasa kinafsi.
19. Mbinu hii ya kimedani, utaitumia kulingana na Mwandamo wa Mwezi, hasa kwenye mwezi mchanga, yaani Siku ya Kwanza au Siku ya 14/15 kutegemea na mwezi.
20. Mbinu hiyo ya kikulungwa itakusaidia kiafya, lakini pia itakusaidia kwenye mambo ya kiuchumi, au kimahusiano.
21. Kama mkeo/mumeo au familia yako unaiona haina furaha basi Sisi Watibeli tuna baadhi ya formations tunazitumia.
22. Lakini pia kufanya nafsi yako iwe Safi kwamba unavutia watu wengi. Kila unachokifanya kinaenda bila shida kubwa.
23. Hayo yote usingeyajua. Na ungeyapata kwa kutoa pesa na kusujudia watu.
24. Tena huko Beach nikienda Siku nikiamua niutoroke mzimu wa kipare. Ninaamua niende Kula, yaani baada ya kuoga sasa nitaenda Kula chakula kizuri.
25. Utanigundua nimekuja Kula Siku hiyo kama nitakuwa nimejikoki. Nimeulamba. Kama mtu mashuhuri au msanii wa Hollywood
26. Sio mpenzi wa kuvaa. Yaani mimi sio Mvaaji. Lakini mara mojamoja najikoki. Labda mara mbili kwa Mwaka.
27. Siku hiyo nikiwa nimevaa suti ya ugoro, taxido Kali, kiatu kimenyooka. Hapo juu nimeweka nywele zangu ndefu Draid Safi kabisa. Kama kawaida lazima nivae mawani nyeusi. Hakika mwenyewe mpaka najisalimiaga.
28. Najiona kama Star wa Hollywood lakini nikikumbuka mfukoni Nina pesa ndogo wazo la kujiona wa maana linakata.
29. Nimechukua bolt mpaka Coco, nashuka pale mimi peke Yangu ndiye nimevaa suti ya kueleweka.
Usiwalaumu wabongo wenzako waliokuwa wananitazama kwa kustaajabu, kuogopa, kutetereka.
20. Walaumu wazungu ambao nao walikuwa wakijikuta wakiinua vichwa vyao. Alafu Mimi sijali wala nini.
21. Huyohuyo! Mimi huyooo. Watu haohao wananisindikiza kwa macho. Sasa itanipasa nitembee kwa umakini Sana ili mchanga usiingie kwenye viatu vyangu vyenye utukufu wa kifalme.
22. Nikapolewa na kidada hivi kilichokuwa kinajiongelesha kwa ukarimu kikibabaika.
23. Mimi nami kama MTU mwenye Majivuno, mwenye kuona Nina hadhi ya Ile suti. Sijali anachosema wala sisikii chochote. Nikakaa huku nikiwa naangalia polepole huku na huku kama mwekezaji hivi.
24. Sekunde kama dakika hivi. Namkumbuka Yule binti ambaye sasa amechoka kwa kupuuzwa lakini hana jinsi zaidi ya kunisikiliza High value customer. Nafikiri aliniona hivyo kwani Siku zingine hawanikaribishi hivyo😂🤓
25. Sasa round hii watakoma.
26. Sasa nikaanza kuongea kingereza cha Kizimbabwe.
27. Nikaona uso WA Yule binti ukikunjuka maradufu. Ni kama alijiambia uvumilivu wake muda sio mrefu utamlipa.
28. Akaongea omega hapo kingereza cha kuunga unga. Huku mimi nikiwa namtazama usoni hali inayomfanya akakanganywe na kingereza kiwe cha kuchechemea. Huku akiniomba msamaha
29. Nilikuwa najikaza nisicheke. Atakoma Leo. Yaani kama alivyokuwa ananiomba msamaha angekuwa anamuomba vile Mungu ninahakika angekuwa mwanadamu asiye na dhambi hata moja kwani angesamehewa na Mola hadi za za wakati ujao.
30. Basi nikamwambia menu iko wapi. Usisahau ni kingereza hapo. Tena cha Zimbabwe
31. Akasema menu blablah blah. Nikajua tayari ananiingiza kwenye Laini. Nikasema sawa tutaona.
32. Nikaagiza Wali Fulani hivi na Samaki mkubwa ambaye najua bei ya chakula nu 35k
33. Akaondoka huyo harakaharaka. Mimi nikawa nabonyeza simu. Dakika thelasini naletewa msosi. Nauchapa. Naagiza na kinywaji. Mpenzi wa sprite, wanasema zimeisha naagiza seven up.
34. Bills ananiletea Tsh 90,000.
Nauliza kivipi, naambiwa 85,000/= chakula kinywaji Tsh 5000/=
35. Basi mjadala ukaanza hapo. Mimi bado nipo kwenye uhusika wa kizimbabwe.
36. Wabongo wakanizunguka hasa wahudumu wa ule mgahawa. Wanavyojaribu kunielezea kwa kingereza ungecheka ufe.
37. Nikagundua ukitaka wabongo wasikupigie kelele zungumza nao kingereza. Yaani utasikia Sir sir. Bro bro listen, you this food more money, 🤣
38. Sasa nilipoona umati umekuwa vyakutosha. Wengine wananisema kwa Kiswahili wananitukana. Mamaaa!😀
39. Nilipooanza kuchanika Kiswahili tena cha chuga babaake!
Nikamwambia mhudumu mmoja aliyekuwa na mdomo kama filimbi,
40. Sikia bamnyogode, msitake kuniletea uree hapa arifu. Hii ni chuga bamnyogode. Hizi mbanga za kunipa flyover kwenye menu bamnyogode sio fresh. Chukua chapa hii"
41. Nikawapa 35k wanabaki wanabung'aa. Wengine wakaanza kucheka.
42. Ati baadaye wanasema ooh! Tulikosea. Mlikosea nini.
43. Vijana kuweni waaminifu.
Mimi nimemaliza.
Nawatakia Sabato Njema
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam