Leo ilikuwa nisafiri kuelekea Dar, siwezi kutaja kutoka mkoa gani, maana nitakuwa namweka wazi aliyenishauri.
Mkuu huyu wa vyombo vya ulinzi na usalama, ngazi ya mkoa, aliniambia kuwa siyo salama kusafiri leo. Nilimwuliza, mbona tumetangaziwa hali ni shwari, tuendelee na kazi za kawaida? Akaniambia, nakushauri kama ndugu yangu, hakuna mwenye uhakika na lolote.
Kwanza ukiwa njiani utapata usumbufu mkubwa sana, utasimamishwa kila mahali na kukaguliwa. Lakini kukitokea chochote, unaweza kushambuliwa na upande wowote kimakosa, wazuia maandamano au waandamanaji.
Na wakati fulani unaweza kushambuliwa na wenye hofu, ufahamu kuwa askari wetu wamekuwa katika mahangaiko kwa zaidi ya mwezi, aliyechoka anaweza kufanya chochote kwa sababu ya hofu au kukosa umakini.
Imenibidi niahirishe safari mpaka tarehe 9.
NB. Kama wakuu wa ulinzi wana hofu namna hii, ni nani mwenye uhakika wa usalama wa nchi hii kiasi cha kuendelea na shughuli kama ilivyo kawaida?
Tusiwalaumu wananchi walioamua kufunga maduka yao au kutulia tu majumbani kwao, na kuwaacha askari wakifanya maandamano kwa niaba ya waliokusudia kuandamana.