Nilikuwa naangalia hapa ndo nimegundua Aiseee... Watu Wabaya wanapukutika sana

Nilikuwa naangalia hapa ndo nimegundua Aiseee... Watu Wabaya wanapukutika sana

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
14,762
Reaction score
32,386
Mnaukumbuka ule wimbo uliwahi pigwa marufuku miaka yetu ile?

" Wanawake wazuri wazuri wameolewa, yamebaki manungayembe yanahangaika"
"
WaTu wema wema wamebaki wanaishi ,wamekufa watu wabaya wamezikwa"

Leo nikisikia mtu amekufa nasema "Daaah.... Alikuwa mtu mbaya huyo" kwa mujibu wa Injili ya CCM 2022 kama ilivyondikwa na Mzee Makamba.

Nliwaza hadi kwenye hivi vitabu vya dini zote.... Nikaona Daaah ... Aisee.... Wale mitume na manabii walikosea wapi mwishoni Mungu akaamua kuwaua? Ila Shetani bado yupo hai... Nikagundua kwa mujibu wa Makamba....nikajumlisha, nikatoa, nikazidisha nikagawanya nikapata jibu nikaweka kwenye parandesi. Jamani tumezika sana....


Akina Kawawa, Nyerere, Bibi Titi, Sokoine... Karume.... Shariff Hamad.... Aisee.... Nlikuwa namwona Shariff kama anawapigania sana wazanzibar ni mtu mzuri. Kumbe hamna kitu.

Hii Dunia kwa sasa imejaa watu wema tu. Nafurahi kusikia hivi. Jamani wabaya wanapukutika. Si mchezo.
 
Hahahah unaweza shangaa akaanza Riz, Mwezi wa kwanza, halafu akaja tembo na Msog ili kamba ya katani ashuhudiw wakifa na yeye anakuja kifo kifo cha kuugua muda mrefu na hakuna wakumuuguza maana watu wa karibu wake wote wameshakufa
 
kwa hiyo ukifa ni mtu mbaya
 
Back
Top Bottom