Nilikuwa nasikia tu kwa wengine, leo yamenikuta

Nilikuwa nasikia tu kwa wengine, leo yamenikuta

mwambunnyara

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2013
Posts
518
Reaction score
208
Kwanza nianze kwa kuwasalimu ndugu zangu,na kuwashukuru kwa namna tunavyoshauriana katika mambo mbali mbali yanayogusa maisha yetu ya kila siku.
Kwanza naomba nisimulie kidogo historia fupi ya mahusiano yangu ili wengine muweze kujifunza.
Nlianza mahusiano kwa Mara ya kwanza Mwaka 2009,nikiwa na miaka 26,lakini kwa bahati mbaya mpnz wangu alihamia south Africa pamoja na familia yake,japo aliniahidi kuwa haweziniacha kwa kuwa nliamini tulipendana sana,lakini mambo yalikuwa tofauti,kwani baada ya miezi michache akanambia kwa mazingira yaliyofanya wao waihame nchi,hawawezi kurudi,hivyo we can just move on separately, ikawa hivyo.
Kiukweli iliniuma sana kumkosa mpnz wangu,lakini sikuwa na namna,ilipofika August ya mwaka 2010,nlijikuta mpweke sana,nikakutana na binti mmoja ktk moja ya vyuo vya elimu hapa nchini,kutokana na mazingira yaliyokuwepo tulijikuta tunafanya mapenzi pasipokutongozana,mara baada ya kumaliza tendo nilijiona mkosaji sana,kwa sababu yule binti hakuwa ananivutia kabisa,nliondoka eneo la tukio nikiwa mnyonge sana,baadaye akanitumia sms kwamba alivutiwa sana namm,na alijenga mazingira ya kufanya mapenzi nami siku ile kwa sababu kwa hesabu zake,ilikuwa ndo siku ya ovulation,kwa hiyo "nime-conceive!!"
Nlihisi amenidanganya,lakini kwa kadri muda ulivyozidi kwenda akawa anani update kila hatua anayoipitia ktk ujauzito wake.
Baada ya miezi kadhaa nikakutana naye tumbo likiwa kubwa,akanambia "kwa hesabu zangu nimekubebea mtoto wa kiume".
Nlikubali kumsapoti,japo nlikuwa na mashaka makubwa kama kweli mimba ile ilikuwa inanihusu au lah!!
Ulipofika muda wa kujifungua,nikamtumia pesa ya maandilizi yote kujifungu,akajifungua salama mtoto wa kiume,nkaanza kuhisi kuwa yawezekana kweli mtoto ni wangu,hilo likajidhihirisha miezi michache baadaye baada ya kwenda kumuona mtoto,alikuwa anafanana sana namimi.
Kwa kuwa sikuwa na mapenzi na huyu mzazi mwenzangu,nliamua kutafuta msichana mwingine nikiwa masomoni Mwaka 2012,mahusiano yetu yalikuwa ya furaha sana,nkimwambia mpnz wangu mpya ukweli juu ya yaliyotokea kabla sijaonana naye,alinielewa vizuri,na maisha yakaendelea.
Siku moja majira ya saa nne asubuhi,mpenzi wangu alinipigia simu kuuliza ratiba yangu ya siku hiyo,nikamweleza bila shida,(ilikuwa siku ya alhamisi),ambapo kwa mujibu wa ratiba ya chuo tulikuwa na practical ya anatomy and physiology kwa masaa manne,kuanzia saa nane mpaka saa 12 jioni,nlipokuwa natoka kwenda maabara kwa ajili ya practical,nlikutana na mpnz wangu akiwa amependeza sana,nlipomuuliza anakwenda wapi,aliniambia anakwenda kwa dean of students thereafter atarudi lecture room kujisomea,na akanitakia darasa jema,tukaachana hapo.
Tulipofika maabara instructor akatwambia hatutakuwa na practical siku hiyo mpaka j.mosi.
Nikiwa narudi kwangu kutokea chuoni,nikamuona mpnz wangu anaingia ndani ya tax na jamaa ambaye sikuwa ninewahi Kumuona machoni mwangu,lakini kabla tax haijaondoka,nlimuona huyo bwana akiongea na mtu ambaye namfahamu vema.
Taxi ilipoondoka nikamtext mpnz wangu "vipi mpnz umeshamuona dean?" Alijibu "yap dis time nipo lecture room najisomea"
Hapo mashaka makubwa yakaujaa moyo wangu,nikalazimika kumfuata jamaa aliyeongea na jamaa nisiyemfahamu,nikamuuliza kama anafahamiana na yule niliyehisi ameniibia mpnz wangu kwa siku hiyo,akanitajia majina ya yule jamaa.
Nikakariri majina then nkaendelea kuchart na mpnz wangu,nikamuuliza unasomea lecture room namba ngapi,akanambia"lr 7,but najiskia vibaya,ntatoka sio muda",nkamwambia poa,nakuja kukucheck Mara moja.
Akajibu poa,baada ya hapo nikajaribu kumpigia simu yake haikupatikana tena mpaka saa tatu na dk.58 usiku,nilishindwa kufanya jambo lolote kwa wakati ule coz moyo ukikuwa unauma sana!!.
Nlipomuuliza baada ya kupatikana,kuwa kwanini alizima simu ghafla na alikuwa wapi,alinibu very confidently "tumbo lilikuwa limeniuma ghafla,nkaenda kulala na sikutaka kukusumbua ukiwa kwenye practical!!!"nlikata simu nikalala.
Ntaendelea baadaye kidogo ngoja nipate dinner,ila mapenzi yanauma sanaaaa
 
Dah!! Aisee hapo mtu alienda kujegeja mzigo. I wonder if ulimrudia huyu demu.
 
Naona una kisa kama changu nilipokuwa chuo mwaka 2 nilikuwa na mpenzi wangu mhehe nilikuwa nampenda sana na yeye nilijua ananipenda na tulikuwa tunakaa karibu siku hiyo nilienda kwake jioni akapika tukala nikamuaga nikarudi kufika kwangu nikarudi kufuata notes sikumkuta nikauliza majirani wakaniambia ameondoka muda si mrefu nikarudi kwangu nikampigia simu akasema yupo nyumbani nikamuuliza sehemu gani mimi nipo kwako akadai ametoka kidogo atarudi nikamdanganya naenda kulala kwangu kumbe nimeingia ndani kwake nimelala kwa vile nilikuwa najua anatunza wapi ufunguo, Mpaka asubuhi alikuwa hajarudi akaja kama mida ya saa 2 kachoka mbaya nikamnyang'anya simu nilichokiona humo nusura nizimie na tangu siku hiyo sikugusa mwanachuo niligeuka padri ghafula.
wanawake hawa tuache tu ukiwaendekeza unaweza kufa siku si zako.
 
Kwa kawaida huwezi kujua thamani ya mapenzi kama hujaumizwa!! Ni wachache sana waliobahatika kujua thamani ya penzi bila kuumizwa, so tunapitia hali hii ili kupata experience!!
 
Kwa kawaida huwezi kujua thamani ya mapenzi kama hujaumizwa!! Ni wachache sana waliobahatika kujua thamani ya penzi bila kuumizwa, so tunapitia hali hii ili kupata experience!!

Mkuu usipime inauma kuliko kawaida.
 
mimi nilikuwa na wa kwangu kila wikendi alikuwa lazima aniage anaenda kwa wazazi wake. siku moja nikaamua kwenda kwa wazazi wake by surprise nikamkuta yuko na ex wake wanakula goodtime nilichoka.
 
Naona una kisa kama changu nilipokuwa chuo mwaka 2 nilikuwa na mpenzi wangu mhehe nilikuwa nampenda sana na yeye nilijua ananipenda na tulikuwa tunakaa karibu siku hiyo nilienda kwake jioni akapika tukala nikamuaga nikarudi kufika kwangu nikarudi kufuata notes sikumkuta nikauliza majirani wakaniambia ameondoka muda si mrefu nikarudi kwangu nikampigia simu akasema yupo nyumbani nikamuuliza sehemu gani mimi nipo kwako akadai ametoka kidogo atarudi nikamdanganya naenda kulala kwangu kumbe nimeingia ndani kwake nimelala kwa vile nilikuwa najua anatunza wapi ufunguo, Mpaka asubuhi alikuwa hajarudi akaja kama mida ya saa 2 kachoka mbaya nikamnyang'anya simu nilichokiona humo nusura nizimie na tangu siku hiyo sikugusa mwanachuo niligeuka padri ghafula.
wanawake hawa tuache tu ukiwaendekeza unaweza kufa siku si zako.

Ktk maisha kuna experience zingine ngumu sana
 
Back
Top Bottom