Hahahaa yaani huu uzi umenikumbusha eti Kuna mtu alikua na mchepuko Sasa mchepuko ukamuambia una mimba huyo jamaa kahudumia mpaka kajifungua, Sasa Kama siku kadhaa zimepita kaenda kumuona mwanae anafika ndani anakutana na njemba nyingine askari imejaa tele Kama pishi la ubwabwa anaulizwa vipi,eti nimekuja kumuona mwanangu, mwanao yupi ?? Mdada anaulizwa anasema ye hamjui kadi ya clinic imeandikwa jina la yule askari akachezea kichapo halafu kalazwa ndani karudi kwa mke wake asubuhi sura haitamaniki, Sasa mke wake anatusimulia anacheka maana hakulala nyumbani alivyomuuliza kamjibu shombo,Ila baada ya kurudi na manundu anaeleza bila hata kuulizwa yupo tu ndani anakandwa na mke wake akiambiwa kwenda hospital eti anaona aibu Sasa nilivyosoma tu Neno kufumaniwa nimekumbuka[emoji1][emoji1] Bora wewe haukupigwa