Nilikuwa natembea na mke wa mtu, nilinusurika kufumaniwa nikaamua kumuacha na kutubu ila nafsi yangu haina amani

Nilikuwa natembea na mke wa mtu, nilinusurika kufumaniwa nikaamua kumuacha na kutubu ila nafsi yangu haina amani

Anza kwa kumueleza ulichofanya, kisha muombe msamaha.
 
Ndugu yangu hapo yakupasa kufanya mambo matatu...
1. Jisamehe na jishukuru kwa kuweza kujitambua na kutambua unafanya kosa kubwa maana wapo wanaofukua wake za watu na hawajajaliwa neema kama wewe ya kujitambua.... watakuja kutambua siku wanafumaniwa na kupelekwa kwa baba au kufanyiwa mambo mengine ya fedheha...

2. Fanya hilo moyo unalokuambia ili kupata furaha ya moyo na faraja moyoni....

3. Endelea kuelimisha jamii ubaya wa kula wake za watu...

Asante
 
wanaume bana

yaani hukuona mwanamke mwingine yyte zaidi ya huyo mke wa rafiki yako??

au ndo ulitumia pesa zako kumrubuni mke wa mwenzako
Unataka kuniambia wanawake hawatembei na waume wa rafiki zao?Sikutumia pesa nilishawishiwa na yeye mwenyewe,na mumewe ananizidi kipato hata Kama namdai 550,000
 
Ndugu yangu hapo yakupasa kufanya mambo matatu...
1. Jisamehe na jishukuru kwa kuweza kujitambua na kutambua unafanya kosa kubwa maana wapo wanaofukua wake za watu na hawajajaliwa neema kama wewe ya kujitambua.... watakuja kutambua siku wanafumaniwa na kupelekwa kwa baba au kufanyiwa mambo mengine ya fedheha...

2. Fanya hilo moyo unalokuambia ili kupata furaha ya moyo na faraja moyoni....

3. Endelea kuelimisha jamii ubaya wa kula wake za watu...

Asante
Nimekupata vizuri mkuu
 
Usimueleze chochote. Punguza au futa kabisa urafiki na yeye. Kaa nae mbali, akikutafuta ongea nae kwa ufupi kuna mambo yamekubana, unaendeleaje, basi ntakucheki wakati mwingine n.k. Asikae akawa rafiki yako tena, hapo utakiwa na amani.
 
Katika vitu nimeapa kutokuja kuvifanya ni kutembea na mke wa mtu

Vishawishi vipo ila ninajitahidi kuvikwepa
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nilikuwa nafanya hicho kitendo kuanzia mwaka juzi na mwaka jana, katika mazingira fulanifulani almanusra nifumaniwe na kufedheheka,

Namshukuru Mungu alininusuru, ningepata fedheha ya milenia kwasababu mwenye nzigo ni mtu wangu wa karibu sana ni zaidi ya ndugu, hata wakati wa kupeleka mahari ukweni nilikuwemo kwenye msafara.

Baada ya kunusurika nikatubu na kuapa kamwe sitorudia tena, lakini pamoja na kutubu kote nafsi yangu haina amani kabisa najihisi mwenye hatia kila nikikumbuka, kibaya zaidi jamaa ananiamini sana mpaka mambo yake ya ndani huwa ananiambia

Mimi ni mshauri wake mkuu,nawaza nilipe faini pasipo yeye kujua ili niwe na amani, Kuna pesa namdai 550,000 aliahidi kunilipa tarehe 30 mwezi huu lakini jana kaja kujieleza hakufanikiwa kupata nisubiri mpaka 30 mwezi ujao,

Sasa mimi nataka hiyo pesa asinilipe nijitoze faini mwenyewe au kwa lugha nyingine nichangie mahari, naomba ushauri wenu wanaJF nipeni mbinu wanaJF nifanyeje ili yeye abaki na pesa na mimi nibaki na utulivu wa nafsi.
Kama wewe ni mshauri wake mkuu kwanini usimwambie ama kumshauri akupe shoo na mkewe ili nafsi yako itulie kuliko kukaa na wasiwasi siku zote?
 
Katika vitu nimeapa kutokuja kuvifanya ni kutembea na mke wa mtu

Vishawishi vipo ila ninajitahidi kuvikwepa
Kuna wake za watu akiona hushawishiki wanavua mpaka nguo,kimbilia ukimbiliako ile picha haifutiki kichwani, mwisho wa siku utajikuta unaanza kumtafuta mwenyewe,omba sana Mungu yasikukute.
 
Kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe
 
Nshakujua nmeisha nunua k y mkundu wako alari yangu kunya kimba gumu la mwisho maana nikisha dubukiza dyudyu basi utakuwa unakunya bira step
 
Vipi kama jamaa yupo humu anapitia huu uzi. Kuwa makini na mitandao itakuweka uchi.
 
Back
Top Bottom