marcoveratti
JF-Expert Member
- Sep 21, 2017
- 1,019
- 1,824
Nimerejea tena kuitazama post yangu ya tarehe 2 June mwaka huu. Niliipa kichwa cha habari, "PEP GUADIOLA NI KOCHA WA KAWAIDAA MNOOO".
nilitoa mtazamo wangu kuhusu hyu kocha uchwara anae chukuliwa kama 50 cent wakati ana hadhi ya 20%
zimepita siku sabini toka niandike yale na nilipingwa sana na nikahisi labda nilikosea.
Nilianza kuhisi hivo ila siku niliyoona Man City ikiondolewa UEFA na Lyon ndio nika pigia mstari mawazo yangu.
Ilinibidi nisubiri muda upite, ili nitafakari vema kabla ya kuandika haya. Isiwe tu ni hisia za kunichania mkeka zimenikasirisha na kuamua kumhukumu[emoji1783]. Ila baada ya muda mrefu wa kutafakari, nimekubali tu kubadili mawazo. Huenda Pep Guardiola si kocha wa daraja la juu kama dunia inavomchukulia. Inawezekana.
Msimu wa nne mfululizo anashindwa kuivusha Man City robo fainali ya UEFA. Subiri kwanza, hii ndiyo timu iliyotumia fedha nyingi zaidi kusajili Ulaya kwa miaka minne iliyopita. Wamewazidi hadi PSG kwa pauni 200 milioni. Mafanikio makubwa aliyonayo ni mataji mawili ya ligi. Hivi kweli waarabu wanavunja benki kila msimu kumpa kila mtu anayemtaka kwa ajili ya mataji ya ligi? Sidhani.
Mara zote Pep alizoondoshwa UEFA, ameondoshwa na timu zilizotumia punje tu ya bajeti ya usajili aliyotumia yeye. Monaco, Liverpool, Tottenham na Lyon. Hakuna hata moja hapo inayoisogelea bajeti ya usajili ya Man City. Naelewa kuna kuteleza, ila kweli kuteleza kwa miaka minne? Sidhani.
Najua nitatajiwa mafanikio yake na Barcelona. Alichukua treble katika msimu wa kwanza na mataji 6 katika msimu wa pili akiwa na vijana tu aliowapandisha kutoka La Masia. Ni kweli, ila uliwahi kujiuliza wale vijana nani aliwapika? Guardiola aliwafundisha kwa miezi 9 tu kabla ya kukabidhiwa timu kubwa. Aliwatengeneza lini? Kazi nzima aliifanya Frank Rijkaard, ila hakuna anayemkumbuka.
Watu wanamuimba Pep tu, ila yeye alichofanya ni kuvuna tu shamba walilopanda wengine. Ndiyo maana kwa sasa, nimechagua kumuweka daraja tofauti. Asifananishwe hata na Klopp, alichukua ubingwa wa Ujerumani na Dortmund iliyojaa wavulana. Ameibadilisha Liverpool kwa bajeti ndogo tu, zaidi amefanikiwa nayo sana, sidhani kama Guardiola anaweza kufanya hayo. Ni maoni tu.