Sababu zangu kwa Conte.
1. Kuirudisha Juventus Top
Utakumbuka Juve kushushwa Daraja, waliporudi haikuwa Timu ile tuliyoizoea,
Mwaka 2009/10 Juve Alikuwa nafasi ya 7, mwaka 2010/11 pia Juve Akaendelea kuwa nafasi ya 7, kwa miaka zaidi ya mitano Inter na Ac milan wanatawala soka La italia, Conte akapewa Timu 2011, Yeye ndio akawatoa huko na kuwapa Ubingwa mfululizo mpaka anaondoka, hivyo kuitoa Timu nafasi Ya 7 na kuipa Ubingwa Mfululizo ni Achievement ambayo Pep hana.
2. Kuprove Nje ya Italia.
Alikuja Epl pia akawapa Ubingwa Chelsea, Huku akitumia wingbacks wake average kama Moses. Akaweka na Record ya Unbeaten kwa hichi kipindi.
3. Kuwashake Juve tena
Amerudi Tena Inter Milan, Tokea utawala Wa Juve uanze Inter anamiss top 4 mara nyingi sana, ila ndani ya Msimu mmoja amepunguza gap la point na mabingwa kuwa 1 tu, pia yupo fainali Europa.
Ukitoa Mafanikio ya ubingwa Conte pia Anabadili Average players kuwa wazuri, mfano ni Victor moses, Ashley young, Sanchez etc. Leo hii Ungeambiwa Young aliekuwa Kajichokea Man Utd watu wanamuona babu tayari anaweza kuwa top player usingeamini.
Ukimuangalia Pep ana mafanikio ila Anashindwa kufikia Malengo ya Vilabu anavyokwenda. Mfano Man City Pelegrini tayari Alikuwa na Nusu ya Uefa na Ubingwa wa Ligi, Pep akaletwa kuendeleza Alipoishia Mwenzake, Mpaka Leo pep hajatoboa Robo fainali Uefa Misimu minne, Same kwa Bayern Alipewa Timu ni Bingwa wa Uefa na Ligi na pia Alishindwa japo alikuwa na Kikosi bora.